Baadhi ya njia unazoweza kutumia kupata wazo bora la biashara (Business Idea)

Kwenye biashara kuna watu wenye mitazamo miwili tofauti 1. Idealists: wanaamini kwanza uwe na wazo vingine kama mtaji vifuate. 2 materialists: wanaamini kwanza uwe na vitu mfano mtaji baadae wazo lifuate.

Mlengo wangu ni kuwa na wazo kwanza. Mimi ni mjasiliamali. Nilianza kuwa na wazo la ufugaji. Nikaanza na jogoo moja na matetea watatu. Kuku akitotoa namwacha na vifaranga kwa wiki mbili kisha namyang'anganya. Baada ya muda mfupi anaanza kutaga tena.

Hivi sasa nina kuku zaidi ya mia moja wa kienyeji na zaidi ya mia tatu wa mayai.

Nimekuwa nikifunga mayai na kupanda nayo kwenye daladala bila kuona aibu. Baada ya muda nimenunua kigari kidogo cha kubebea mizigo ninachokitumia kubeba chakula cha kuku na kupeleka mayai kwa wateja.

Ninachotaka kusema ni kuwa unaweza kuanza ujasiliamali kwa kiasi kidogo sana cha pesa. Tusifikirie lazima tuwe na mamilioni.
 
Siku zote nimewambia jamaa zangu wanaosema hawana cha kufanya kuwa wangekuwa na vision kupata mtaji si priority. mimi nimejifunza sana coz wapo ambao wameomba mitaji na wamepewa lakin leo hawana chochote.

Niliwahi kukutana na mmiliki wa shule moja maarufu jijin arusha miaka ya nyuma kidogo akanieleza historia ya maisha yake. Alianza kumilki nursery school aliyoiendesha kwa mshahara wake mdogo alokuwa analipwa kama mwalim, huku familia ikilazimika kukosa hata chumvi lakin leo hii tunazungumzia shule yenye thamani zaid ya bil 12!!
 
siku zote nimewambia jamaa zangu wanaosema hawana cha kufanya kuwa wangekuwa na vision kupata mtaji si priority. mimi nimejifunza sana coz wapo ambao wameomba mitaji na wamepewa lakin leo hawana chochote.
Niliwahi kukutana na mmiliki wa shule moja maarufu jijin arusha miaka ya nyuma kidogo akanieleza historia ya maisha yake. Alianza kumilki nursery school aliyoiendesha kwa mshahara wake mdogo alokuwa analipwa kama mwalim, huku familia ikilazimika kukosa hata chumvi lakin leo hii tunazungumzia shule yenye thamani zaid ya bil 12!!

Dah, Ni kweli mkuu, Mtaji mkubwa ni commitement yako, watu tunatumia kukosa mtaji kama ngao, ila ukweli sio hivyo.
 
Nakubaliana na wewe mkuu, nakumbuka kabla sijaanza kusoma yaani elimu ya chuo niliwahi kuuza duka kama miezi miwili hivi yaani niliona fursa nyingi

1: unaweza ukaanza na mtaji mdogo na kutajirika
2: unaweza ukaanzisha biashara nyingine ya kipato kikubwa ndani ya biashara yako. Ni hayo tu wakuu ila nami nikimaliza masomo lazima nirudie biashara maana inalipa sana naomba kuwasilisha
 
Shukrani sana kaka kwa uzi huu wa ukweli. Nitalifanyia kazi hili kwa undani zaidi coz nilishaanza kujiajiri na nikasuasua kidogo lakini kwa uzi huu najua nirekebishe wapi.

Keep it up :smile-big:
 
Unacho sema Mama Joe ni kweli kabisa, Kuna Rafiki yangu Juzi alikuwa ananipatia full story za Maisha ya Wachina, kwa kweli Tanania tunayo kazi sana Bila kubadilika maendeleo tutayasikia kwenye redio, Wachina wana nidhamu ya Hali ya Juu kabisa katika maswala ya fedha na kwa wachina Familia nzima ni lazima ifanye kazi si kwamba Baba na Mama waende kutafuta Huku nyuma watoto wanabakia kula tu ma kutazama TV kutwa nzima, China Kijana akimalzia Chuo ni lazima achacharike hata kwa kuuza pipi, na si kwamba auze pipi then pesa ale no ni pesa ya familia,

- Chiana biashara ya kupigana offa hawaijui
- China Biashara ya kutafuta sifa kwenye Mavazi na magari hawaijui, kuna public transport na zinatosha kabisa sasa garila nini
-
Watanzania kwenye swala la Saving tunaweza kuwa tunaongoza Duniani na si dhani kama kuna nchi nyingine ambayo wanachi wake wana poor Money managment kama sisi.

- Unaweza amka asubuhi kwenda kazini bila kuwa na plan ya kununua chocjote lakini utarudi na viatu kisa tu umekutana na Machinga akiuza viatu,
- Offa zakutafuta sifa
- Sifa za kumilika Gari, unakuta kuna staff Buss lakini mtu anaona bora aende na gari lake mwenyewe kuliko kupanda staff bus

So katika ile wealth Equation bado tunakazi sana

Unaweza ukanisaidia wealth equation mkuu?
 
Back
Top Bottom