BAADA YA RAIS WA AWAMU YA NNE KUITWA DHAIFU NA MBUNGE NA MAWAZIRI WAKE KUITWA MIZIGO NA KATIBU WAKE WALIJISAHIHISHA.

1000 digits

JF-Expert Member
Oct 16, 2012
6,260
7,936
Serikali tuliyo nayo leo ni matokeo ya Kukosolewa na kujisahihisha kwa Chama Cha Mapinduzi.

Baada ya Mbunge J.Mnyika Kusema kuwa Rais wa awamu ya nne alikua dhaifu katika kushughulikia Mafisadi. CCM na serikali yake wakati huo hawakumpa misukosuko wala kumwandama Mbunge huyo bali Chama kilijipanga na Kumleta Rais wa awamu ya Tano Jasiri,Imara,Mwenye misimamo isiyoyumba na mzalendo kwa Taifa lake.
Mh .Rais JPM naye kwa kuzingatia Kauli ya Katibu mkuu wakati huo Komredi Kinana ya kuwakosoa kwa kuwaita baadhi ya mawaziri kuwa ni Mizigo , aliamua kufanya kazi na CAG Jasiri na mwadilifu,wakuu wa mikoa na wilaya wachapa kazi na mawaziri Wachapa kazi na kuwaondoa wale walioshindwa kwenda na kasi na Kauli yake ya Hapa Kazi tu.

N B :
Ulikua ni wakati muhimu sana kwa Spika wa Bunge kufanyia kazi maoni ya CAG kuhusu udhaifu wa Bunge kwa kuwapa semina ya kuwapa uwezo wa Bunge wake wa Chama cha Mapinduzi namna ya kuisimamia serikali kisawasawa.
Tumeona mijadala ya muhimu kwa Taifa letu ikipuuzwa na kufanyiwa mipasho na wabunge na matokeo yake sheria mbovu kupita bila kufanyiwa uchambuzi wa kina.

Ningependa kuona Bunge letu likimwita CAG "dhaifu" ,Siku akishindwa kuweka hadharani madudu ya watendaji wa serikali katika masuala ya Fedha.

Watanzania tusipo Kosoana wenyewe kwa wenyewe tumtegemee nani aje kutukosoa kwa lengo la kujisahihisha !?

Anayekosa ameaminiwa na kupewa kazi na kulipwa kwa kodi zetu wrote.
...Anayekosolewa naye tumemtuma na kumlipa kwa pesa za Kodi zetu.
Anayekosoa na kukosolewa wote ni watu wetu tunaowalipa kwa kodi zetu.
Heshima bora kabisa ni ile inayotoka kwetu sisi tulio watuma na sio wao kutaka kujikweza na kugombania heshima wao kwa wao.

Wanajenga nyumba moja kwa nini wanagombania Fito?
Mchezaji wa timu moja akimkosoa mchezaji mwenzake kuwa anaonyesha udhaifu kwenye kufunga magoli kwa pasi anazopewa kwenye nafasi ya wazi kabisa kufunga goli ,sio sababu ya kuzira kabisa kupokea pasi zake na kumwomba Kocha amtoe nje mkosoaji.
Kwenye soka Mchezaji akimkosoa mwenzake anakua na lengo la kuimarisha timu na kuleta ushindi.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: M18
Back
Top Bottom