Money Stunna
JF-Expert Member
- Aug 9, 2011
- 13,054
- 6,289
NI mtafutano! Staa mkubwa wa sinema za Bongo, Blandina Chagula Johari ameingia kwenye vita ya maneno na bosi wa Mtanashati Entertainment, Ostaz Juma Namusoma ikiwa ni siku chache tangu jamaa huyo alipotangaza kumuoa mwanadada huyo.
MADAI YA AWALI YA OSTAZ
Katika maelezo yake ambayo yapo kwenye rekodi zetu, Ostaz alidai kuwa Johari anajua kila kitu kwani walifahamiana kitambo hata kabla ya mrembo huyo kujuana na Ray.
Hakuishia hapo, Ostaz alidai kuwa tayari amemfungulia Johari kampuni ya kutengeneza sinema pamoja na vifaa vyote hivyo yupo kwenye mishemishe za kumuoa.
JOHARI SASA
Ili kuondoa utata huo, Hohari alitafutwa na kutaka kujua undani wa ishu hiyo ambayo imezua maswali mengi hasa kwa mashabiki wake.Johari: Sijawahi, sina na wala siwezi kuwa na uhusiano na mtu mpuuzi kama yule (Ostaz Juma). Mwanzoni nilidhani utani, nashangaa imekuwa ishu kubwa.Ni kweli Ostaz alikuwaga anakuja pale Kaole tulipokuwa tunafanya mazoezi lakini si yeye waliokuwa wanakuja ni wengi. Hakuwahi kunitongoza ila kila nilipokutana naye nilikuwa najua kwa kumwangalia tu machoni. Alikuwa anaonesha kabisa ananitaka lakini hakuwahi kunitamkia.
Hajawahi kuniambia anataka kunioa. Kwanza mimi ni Mkristo. Sina ndoa mbili. Siwezi kuolewa mke wa pili na mpuuzi kama yeye.Kwani kupiga picha na mtu ndiyo tayari mmekuwa wapenzi au wachumba? Labda yeye anachukulia hivyo kwamba ukishapiga picha na mwanamke tayari anakuwa mpenzi wako.
Mh! Achana na kampuni au vifaa, hata simu tu hajawahi kuninunulia, kwanza hana fedha. Halafu ajue kabisa kwamba mimi ni tofauti na hao wasanii wengine wanaoishi kwa kutegemea kuhongwa. Mimi ni super woman, siku hizi huwa fedha kwangu ni makaratasi. Huyo Ostaz ana fedha gani?
Haniwezi, mimi siyo kama hao watoto anaowadhalilisha kwa kuwapigisha magoti na akome kabisa kutumia jina langu kama daraja. Hakuna kitu ninachochukia kama mtu kutaka kutumia jina langu kujitafutia umaarufu, ana hadhi gani ya kuwa na mimi, akome kabisa,Mimi ni mwanamke niliyekamilika. Nina mchumba na soon nitamtambulisha kwa mashabiki wangu. Lakini ijulikane kuwa siyo Ostaz kwani hawezi kuwa mchumba wangu