Baada ya mahojiano: Makosa yaliyomnyima Lema dhamana ni haya, kwa mujibu wa Mwanasheria wake

Status
Not open for further replies.
Mh. Lema na yeye ana kihere here sana kila kitu lazima aropoke yeye tu, tumechoka sasa watu wa arusha tunataka mbunge anayefanya kazi kama alivyoahidi sio kila siku mahakamani na polisi tu. 2015 itafika hajafanya lolote zaidi ya kushindana na polisi na kuandaa maandamano yasiyo na tija kwa jii la Arusha khaaa. Angetumia busara kuongea na wale wanafunzi wala haya yote yasingemkuta ropoka ropoka upunguze na usipende kudandia kila kesi na tukio saa zingine vitu vinakuwa framed ili uingie kichwa kichwa yakukute kama yaliyokukuta sasa!! Acha kukurupuka.
Ungejitahidi kuficha upumbavu wako ingekusaidia sana ukaheshimika badala ya kuuanika hadharani kama ulivyofanya. Kama hujui jambo sio lazima kuchangia, kukaa kimya yaweza kuwa hekima kuliko kuongea upuuzi
 
Ha ha ha ha me nashangalia sana kuwa mpaka ss hawajambambikizia kesi mbaya nilichofurahi kwa mashtaka haya hakuna kesi hapo tuombe Mungu akifishe J3 mahakamani na dhamana itakuwepo tu

Mdhamana atapewa na anastahili, lakini anayo kesi ya kujibu, uchochezi ni hujumu kubwa inayoweza kuleta madhara kwa maisha na mali kuteketea, as an MP he should know how to behave, but knowing Lema and his culture that is asking too much of him, some habits don't change.
 
Kweli mkuu kuna haja watz tufundishwe somo la uraia kama nyongeza kuhusu kazi ya mbunge, mkuu wa wilaya na mkuu wa mkoa katika situation ya fujo zinazohatarisha amani kwenye jamii kubwa, kimsingi huo ulikuwa ni mzigo wa mkuu wa wilaya ya Arusha mjini na endapo angeshindwa ndio angekwenda mkuu wa mkoa na kamati yake ya ulinzi na usalama wakiambana na viongozi mbalimbali. Najaribu kutafakari tu kwa umakini kuhusu hili sakata maana wakati mwingine hivi vitu tunavichukua kiushabiki bila kuangalia kiundani kumbe watu wanashindana kiitikadi tu kama ulivyosema Pwagu na Pwaguzi. Miaka ya nyuma tumekuwa tukigoma kwenye mashule kisa wali na vyuo kisa mikopo na mwisho wa siku wa siku atakuja mkuu wa wilaya na kundi lake kuweka sawa akiwa pamoja na viongozi wa eneo husika (mbunge, diwani n.k), kuna mazingira tunahitaji kufanya kazi kama team hata kama tuna tofauti za kiitikadi na baada fujo kupoa ndio kila mdau kutokana na ushawishi wake anatia timu kutuliza fujo na kuangalia namna ya kushughulikia matatizo na si kama hivi ilivyotokea ArushaKikubwa hapa ni kuangalia namna ya kutatua tatizo though approach iliyotumika ni tofauti kwa pande mbili pia, ninacholaumu hapa ni namna walivyomkamata huyu jamaa kwani ni mtu mwenye address na sidhani kama wangefuata taratibu za kawaida wangeshindwa kumkamata kwani mwisho wa siku watamwachia na hakuna mashitaka (hizi ni siasa tu though ningependa siku moja watu wakafanya kazi kama team ktk situation kama hii na si kwa style hii

Kabla ya kumfundisha mtanzania wa kawaida nadhani waanzie na viongozi wa serikalini maana hawa naona hawajatambua uwepo wa vyama vingi.
 
Hii ndio tanzania na hawa ndio viongoz we2 nchi hii inaendeshwa kidikteta na kuvi2mia vyombo vya ulinz na usalama kwa manufaa yao binafs kuendelea kukilinda chama!!mbona aliyetuma ujumbe kwenye cm kuwa atambambia kesi anayotaka wala hashughulikiwi?ee mwokoz njoo utuokoe watu wa tanzania tunaangamia
 
jaman hii serikali inadhani kua adi sasa watu hatujajua haki zetu na sheria.hivi tutafunga macho hadi lini na kuogopa hadi lini.muda umeshafika ambapo sasa lazima tulazimishe ukombozi wa nchi hii
 
Hii ndio tanzania na hawa ndio viongoz we2 nchi hii inaendeshwa kidikteta na kuvi2mia vyombo vya ulinz na usalama kwa manufaa yao binafs kuendelea kukilinda chama!!mbona aliyetuma ujumbe kwenye cm kuwa atambambia kesi anayotaka wala hashughulikiwi?ee mwokoz njoo utuokoe watu wa tanzania tunaangamia
Hapa kilichowatisha ni Lema kutoa message hiyo kwa umma wakaona dili liliishabumbulika. Yaani hapo Lema alifanya calculated pre-emptive strike
 
Mambo yaliyomfanya Mbunge wa arusha Godbless Lema akamatwe na kunyimwa dhamana jioni hii ni haya yafuatayo baada ya kuongea na Mwanasheria wa Lema wakili Humphrey Mtui

i)Kosa la kwanza ni kuwaambia wanafunzi wa chuo cha uhasibu alipoenda kuwatuliza kuwa ‘dhambi kubwa kuliko zote ni woga ‘.Haki hutafutwa na kupiganiwa ikiwa jambo unalipigania ni la msingi na linafaa kupiganiwa(Worth fighting for)

ii)Kosa la pili ni pale alipotamka kuwa ‘’Tumemtafuta mkuu wa mkoa juu ya Matatizo yenu na mlivyoshuhudia hapa amechukua muda mrefu na kuingia kama vile anaingia kwenye send-off.Hawa ndiyo viongozi wetu ambao hawajali matatizo ya wananchi’’Kwa hiyo huo ni uchochezi

iii)Kosa la Tatu ni pale alipotamka kuwaambia wanafunzi kuwa ‘’Mimi Mbunge wenu nipo sambamba nanyi hadi mpate haki yenu na ikiwa mkuu wa mkoa hatakuja hapa kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi wa mkoa nitawaongoza hadi ofisini kwake ili mpate majibu na haki yenu kwani ni haki yenu ya msingi kwa mujibu wa katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ambayo niliapa kuilinda Bungeni na pia inaruhusiwa kwa mujibu wa kikanuni na kifalsafa katika utekelezaji wa utawala bora wa kidemokrasia ambao msingi wake ni kusikilizwa na kulinda haki za binadamu’’Huu nao umeitwa kwamba ni uchochezi.

Sasa haya maneno hapo juu ndiyo yaliyosababisha jeshi la polisi kuvamia nyumbani kwake usiku wa manane na kuzua taharuki maeneo hayo na ndani ya nyumba yenye ndugu jamaa na hata mtoto mwenye miezi mitano huku polisi wakitumia nguvu na kukiuka sheria

Huo umeitwa uchochezi baada ya mkuu wa mkoa kumtumia ujumbe wa mkononi kupitia simu yake kupitia namba 0752960276 aliyotishia kumbambikizia kesi anayoitaka yeye.

Sasa hayo waliyoita makosa ya uchochezi ndiyo yaliyomnyima haki ya dhamana leo.tutafakari kama Arusha itatawalika kwa hali hii.

Hebu tupime makosa hayo matatu kama yanaweza ku-justfy mambo yote yaliyotokea
.

Mleta uzi si wa kumuanini kutokana na habari kwa sababu ni kutoka Chadema na pia chanzo cha habari ni cha upande mmoja, yaani wakili wa Chadema. Kwanini tusiamini mnataka kutengeneza mazingira ya kuaminisha umma kile mnachokitaka.Acheni michezo hii ya kizamani iliyokuwa ikifanywa na CCM. Wewe ndiye mshitakiwa na unajaribu kujikwamua halafu eti wewe ndiye chanzo cha habari za suala hilo, wapi na wapi..... (conflict of interest).
 
Ungejitahidi kuficha upumbavu wako ingekusaidia sana ukaheshimika badala ya kuuanika hadharani kama ulivyofanya. Kama hujui jambo sio lazima kuchangia, kukaa kimya yaweza kuwa hekima kuliko kuongea upuuzi

usijidai una heshima wewe ndio mpumbavu usiejua kuchanganua mambo na kudandia vitu kama huyo Mbunge wetu Lema kila kukicha polisi. Lazima tuseme this time kachemka, period. Rejea zile clip uone jinsi alivokuwa anaongea pumba na wanafunzi bora angebaki kwa mkewe.
BTW: Heshima yako siihitaji na hainiongezei wala kunipunguzia chochote, kamuheshimu bwanaako anaekuweka mjini usihadhirike.
 
can you be serious!?
Mh. Lema na yeye ana kihere here sana kila kitu lazima aropoke yeye tu, tumechoka sasa watu wa arusha tunataka mbunge anayefanya kazi kama alivyoahidi sio kila siku mahakamani na polisi tu.
Leornado
Join Date : 12th November 2010

Location : Papua New Guinea

Posts : 1,378
Rep Power : 712
Likes Received104
Likes Given127
 
huu ndo uongozi wa mkwele wa b.o tuchunge sana na bado uchaguyi mkuu haujafika 2015 mbona tutaona c zetu macho
 
Nawapa pole CCM maana mwisho wa siku wao ndio watalia.Sijaona kosa la Lema hata ningekuwa mimi bado ningweza kwenda mara moja kwenye tukio na kuwasikiliza wanafunzi,kuwashauri na kuwakataza kuandamana.Hakufanya kosa lolote.Mkuu wa mkoa alitakiwa kuona umuhimu wa kuitwa kwake na kiongozi mwenzake ili wasaidiane kutatua matatizo,bdala ya kuomba kipaza sauti angeomba wanafunzi wachague kamati ndogo ili wakae na mkuu wa mkoa na viongozi wengine ili kujua suluhu inapatikanaje.

Tatizo la mkuu wa mkoa hata muonekano wake ulionyesha dharau kwa wanafunzi, na ikumbukwe chuo hakichukui wanafunzi waliomaliza sekondari tu,wanachukua hata wafanyakazi na watu wenye familia zao.Kwa kweli hata kama watu hawampendi Lema lakini haki yake tumpe.ALiweza hata kuwaambia wanafunzi waache kwenda kwenye madisko usiku,amefanya kosa lipi?

Tujiulize polisi walikuwa na sababu gani ya kutupa mabomu mahali ambapo hakuna fujo?Nina wasiwasi na polisi pia,inawezekana wanafanya yote haya kuidhalilisha serikali makusudi,viongozi wa polisi waliangalie hili,polisi inajidhalilisha hasa kimataifa.Kwa ufupi Tanzania DEMOKRASIA ya vyama vingi hakuna.
 
Presidaa yupi unayemaanisha? Mstaafu, marehemu au wa sasa?

JF_Logo.png
Have the right of your own to ask nosenses!!!
 
kweli hizo ni kauli za uchochezi bila ubishi na kwa hali ilivyo kuwa pale .Ila tukumbuke uhusiano mbovu kati ya lema na mulongo ndio question mark???????????
Kaka, what matters ni matokeo ya alichofanya Lema. Hata wananchi wanapolalamika nchi kutafunwa si kwa sababu ya kutafunwa Bali ni kwa sababu ya matokeo ya kutafunwa - umasikini uliokithiri. Lema atabeba masalaba wake, hakuna wa kumbebea. Kuhusu Mulungo Kama alijua hilo kwa nini ajilengeshe kwenye 18 zake?!
 
Hivi kweli Mwinyi na Mkapa mmeshindwa kutoa nasaha zenu kwa uongozi huu uliopo madarakani??!! Tumekua nchi ya kusadikika na kutamalaki kwa mate do ya watawala!!

Hakika Nyerere alikua ni Baba wa Taifa,I wish angefifuka japo ahutubie Taifa hili japo mara moja,huenda waafidhina wangefumbia ibongo wao!!
Nyerere ni CCM sidhani kama angaliweza kuwa upande wa Lema.
 
Hapo huyo mkuu wa mkoa,anajaribu kumuonyesha lema kwamba yeye ni nani....kumbe polisi wanapokea orders kutoka kwa mkuu wa mkoa.
 
UPDATES KUTOKA MAHABUSU LEO 27/04/2013:

Taarifa za uhakika muda huu kutoka Mahabusu kituo cha polisi Arusha ni kwamba Mbunge wa Arusha Mh.Godbless Lema ameendelea kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji alipopelekewa kifungua Kinywa na ndugu zake asubuhi hii

UDHALILISHAJI
-Mke wake alimpelekea Mswaki na Dawa ya meno lakini polisi wamekataa kabisa kwamba hairuhusiwa.Kama mjuavyo Mswaki hauruhusiwi kuingia nao ndani mahabusu kwa hiyo Lema alikua ametoka kwenye chumba cha mahabusu na kanuni hazimfungi au kumzuia kutumia Mswaki katika kujiweka katika mazingira mazuri kiafya.Hili ni jambo la kawaida kwa mwananchi yeyote na ni haki ya mahabusu
-Pia wakati huo huo askari walianza kuikagua chai aliyoletewa kwa kutumia fimbo aliyokua nayo jambo lililomchukiza Leman a kuhoji hii humiliation ni ya nini?Kama vile haitoshi askari akaendelea kumshinikiza kuwa wamempa dakika mbili za kunywa chai kitu ambacho kimezua mabishano na Lema akagoma na kudai kwamba ni lazima sasa Mwanasheria wake aje kwanza amfafanulie kama kweli haki zake hazijakiukwa.
-Pia ameletewa magazeti na akiwa ameshika gazeti la Mwananchi askari polisi alimnyang’anya na kumwambia ahairuhusiwi hata kupata taarifa zozote
Lema amemuta Mwanasheria wake

KESI YA MAUAJI INASUKWA KUTUMIA UJUMBE ALIOTUMA RC
Wakati huo huo kuna taarifa nyeti kabisa na za uhakika kwamba muda huu jeshi la polisi likishirikiana na ofisi ya mkuu wa mkoa wanafanya jitihada za kubadili uamuzi wa kumfungulia kesi ya uchochezi kama nilivyoweka hapa jana baada ya kuongea na mwanasheria wake jana na sasa wanataka kumfungulia kesi ya mauaji kwa kuzingatia ujumbe ule wa simu uliotumwa na mkuu wa mkoa.Lengo ni kumnyima dhamana na hili ni kumkomoa kuhusu kauli yake kuwa Rais Kikwete ni Mdini.
Tunaendelea kufuatilia kwa karibu na JF kitakua chombo cha kwanza kabisa kuhabarishwa yanayojiri.Katika muda wote huu nitalinda heshima ya JF kwa habari za ukweli na uhakika kama nilivyofanya nilipothibitisha taarifa za kufuatiliwa gari ya Dr.Slaa ambazo zimekuja kuthibitishwa baadae kuwa ni kweli.
 
Mambo yaliyomfanya Mbunge wa arusha Godbless Lema akamatwe na kunyimwa dhamana jioni hii ni haya yafuatayo baada ya kuongea na Mwanasheria wa Lema wakili Humphrey Mtui

i)Kosa la kwanza ni kuwaambia wanafunzi wa chuo cha uhasibu alipoenda kuwatuliza kuwa ‘dhambi kubwa kuliko zote ni woga ‘.Haki hutafutwa na kupiganiwa ikiwa jambo unalipigania ni la msingi na linafaa kupiganiwa(Worth fighting for)

ii)Kosa la pili ni pale alipotamka kuwa ‘’Tumemtafuta mkuu wa mkoa juu ya Matatizo yenu na mlivyoshuhudia hapa amechukua muda mrefu na kuingia kama vile anaingia kwenye send-off.Hawa ndiyo viongozi wetu ambao hawajali matatizo ya wananchi’’Kwa hiyo huo ni uchochezi

iii)Kosa la Tatu ni pale alipotamka kuwaambia wanafunzi kuwa ‘’Mimi Mbunge wenu nipo sambamba nanyi hadi mpate haki yenu na ikiwa mkuu wa mkoa hatakuja hapa kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi wa mkoa nitawaongoza hadi ofisini kwake ili mpate majibu na haki yenu kwani ni haki yenu ya msingi kwa mujibu wa katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ambayo niliapa kuilinda Bungeni na pia inaruhusiwa kwa mujibu wa kikanuni na kifalsafa katika utekelezaji wa utawala bora wa kidemokrasia ambao msingi wake ni kusikilizwa na kulinda haki za binadamu’’Huu nao umeitwa kwamba ni uchochezi.

Sasa haya maneno hapo juu ndiyo yaliyosababisha jeshi la polisi kuvamia nyumbani kwake usiku wa manane na kuzua taharuki maeneo hayo na ndani ya nyumba yenye ndugu jamaa na hata mtoto mwenye miezi mitano huku polisi wakitumia nguvu na kukiuka sheria

Huo umeitwa uchochezi baada ya mkuu wa mkoa kumtumia ujumbe wa mkononi kupitia simu yake kupitia namba 0752960276 aliyotishia kumbambikizia kesi anayoitaka yeye.

Sasa hayo waliyoita makosa ya uchochezi ndiyo yaliyomnyima haki ya dhamana leo.tutafakari kama Arusha itatawalika kwa hali hii.

Hebu tupime makosa hayo matatu kama yanaweza ku-justfy mambo yote yaliyotokea
.

UPDATES KUTOKA MAHABUSU LEO 27/04/2013:

Taarifa za uhakika muda huu kutoka Mahabusu kituo cha polisi Arusha ni kwamba Mbunge wa Arusha Mh.Godbless Lema ameendelea kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji alipopelekewa kifungua Kinywa na ndugu zake asubuhi hii

UDHALILISHAJI
-Mke wake alimpelekea Mswaki na Dawa ya meno lakini polisi wamekataa kabisa kwamba hairuhusiwa.Kama mjuavyo Mswaki hauruhusiwi kuingia nao ndani mahabusu kwa hiyo Lema alikua ametoka kwenye chumba cha mahabusu na kanuni hazimfungi au kumzuia kutumia Mswaki katika kujiweka katika mazingira mazuri kiafya.Hili ni jambo la kawaida kwa mwananchi yeyote na ni haki ya mahabusu
-Pia wakati huo huo askari walianza kuikagua chai aliyoletewa kwa kutumia fimbo aliyokua nayo jambo lililomchukiza Leman a kuhoji hii humiliation ni ya nini?Kama vile haitoshi askari akaendelea kumshinikiza kuwa wamempa dakika mbili za kunywa chai kitu ambacho kimezua mabishano na Lema akagoma na kudai kwamba ni lazima sasa Mwanasheria wake aje kwanza amfafanulie kama kweli haki zake hazijakiukwa.
-Pia ameletewa magazeti na akiwa ameshika gazeti la Mwananchi askari polisi alimnyang’anya na kumwambia ahairuhusiwi hata kupata taarifa zozote
Lema amemuta Mwanasheria wake

KESI YA MAUAJI INASUKWA KUTUMIA UJUMBE ALIOTUMA RC
Wakati huo huo kuna taarifa nyeti kabisa na za uhakika kwamba muda huu jeshi la polisi likishirikiana na ofisi ya mkuu wa mkoa wanafanya jitihada za kubadili uamuzi wa kumfungulia kesi ya uchochezi kama nilivyoweka hapa jana baada ya kuongea na mwanasheria wake jana na sasa wanataka kumfungulia kesi ya mauaji kwa kuzingatia ujumbe ule wa simu uliotumwa na mkuu wa mkoa.Lengo ni kumnyima dhamana na hili ni kumkomoa kuhusu kauli yake kuwa Rais Kikwete ni Mdini.
Tunaendelea kufuatilia kwa karibu na JF kitakua chombo cha kwanza kabisa kuhabarishwa yanayojiri.Katika muda wote huu nitalinda heshima ya JF kwa habari za ukweli na uhakika kama nilivyofanya nilipothibitisha taarifa za kufuatiliwa gari ya Dr.Slaa ambazo zimekuja kuthibitishwa baadae kuwa ni kweli.

Nawe uliyeweka thread hii JF ni Mchochezi!!!!!!
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom