Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 914
- 4,264
Leo kwenye gambe nimekutana na mwanangu anayefanyakazi kwenye moja ya mfuko wa kijamii. Nilipopiga naye stori moja mbili kuhusu kikototoo mwana kateleza ukweli kwamba wastaafu ambao ni watumishi wa umma wasipojiandaa mapema wakategemea pensheni watakufa kwa presha.
Kwanza anasema mifuko ya kijamii haipo tayari kuweka wazi kwa watumishi formula ya kukokotoa mafao.
Pili mifuko hii haipo tayari kufanya ulinganisho wa pensheni kati ya Kikokotoo cha zamani na kipya.
Tatu, watumishi wenyewe wanaofanya kazi kwenye mifuko baada ya kuona giza kwenye kustaafu wamejiwekea utaratibu wa mishahara na marupurupu mazuri na wanahimizana kukamilisha mambo ya msingi kabla ya umri wa kustaafu. Aidha mikopo yao ni minono ukilonganisha na wakatwaji mfano waalimu na Kada ya Afya ambao ni wengi nchini.
Kilichonishtua, baada ya kuunganisha mifumo wamebaini baadhi ya data za watumishi hazipo sawa. changamoto hii anadai inachangiwa na mambo mawili.
Kwanza, kumbukumbu za makato ya watumishi za miaka ya nyuma zimevurugika na nyingine hazikuhifadhiwa vizuri. Maelekezo waliyopewa, kuanzia mwaka jana akijitokeza mtu anastaafu wakabaini kumbukumbu hazipo sawa wanamtengenezea mstaafu namba wanalazimisha alipe madeni ambayo hayaonekani kwenye mfumo ndipo wamalipe pensheni kama hataki aache.
Pili, wamebaini baadhi ya taasisi za serikali zilikwapua makato ya watumishi na kuyatumia vibaya au wengine kutumia makato hayo kujipongeza (wizi). Kwa kuwa ni vigumu kumwajibisha mwajiri au yule aliyekula makato ya pensheni za watu msalaba unaangushiwa kwa watumishi.
Watumishi wanalazimishwa kulipa makato yao ya miaka ya nyuma na kulipa makato yaliyopaswa kufikishwa kwao na mwajiri ambayo ni serikali.
Kupitia Stori hizi nikasema watumishi wa umma wa Tanzania wana matatizo ya fikra na tukiendelea hivi tusitegemee maendeleo ya sekta zetu. Kama toka mwaka Jana watumishi wanalipishwa madeni yaliyopaswa kulipwa na serikali na wanalipa tuwasaidieje?
Lakini nikaenda mbali zaidi kujua suala hili Lina baraka ya wizara ya fedha? Mwana gambe akasema wizara ya fedha haina taarifa kwamba watu wanatozwa madeni yaliyopaswa kulipwa na serikali. Maana yake wapo watu kwenye mifuko ya kijamii wanataka kumgombanisha mama na watumishi wa umma.
Mwisho, hizi taarifa zinaweza kuwa zina usahihi kwamba watumishi wanajilipia makato yaliyotafunwa na walafi fulani. Lakini pia naamini hizi pesa zinazolipwa na watumishi wanaotaka kupata mafao na kusafisha data zao zitaombwa hazina Kwa mgongo wa nyuma na watu wanazipiga.
Sijawahi kusikia bungeni serikali ukisema watumishi wajilipie cash makato ya pensheni, taarifa za waliopo serikalini zinasema haya makato ufanywa automatic kwenye salary. Mama yangu kastaafu ten years back hakuwa anachangia fedha cash, Waziri mwenye dhamana fuatilia.