Baada wa Watendaji wa Serikali za Mitaa Kawe 'Kutimka Mbio' Kuogopa 'Chatu' aliyeko katika pori la Chuo cha Tiba Lugalo msaada unahitajika

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
57,157
110,627
Taarifa ambazo GENTAMYCINE nimethibitishiwa na Mamlaka ya Ofisi za Serikali ya Mitaa Kawe na Mtendaji Mwandamizi kutoka Jeshini Kambini Lugalo kilipo Chuo chao cha Tiba cha MCMS ni kwamba kuna uwepo wa Chatu mkubwa kiasi cha Kutishia Maisha ya Watu.

Kwa takribani Siku tatu zimepita Wakazi wa Kawe (hasa eneo yalipo Makaburi) zamani kulikuwa ni Hostel na sasa Jeshi (JWTZ) limejenga Chuo chake cha Tiba Mamlaka ya Serikali ya Mitaa Kawe imekuwa ikipita Kuwatangazia Watu kuchukua Tahadhari (hasa kwa Watoto) na Watu waliokuwa na Mazoea ya Kukatisha huko Makaburini (zamani Hostel) kuelekea Coca Cola na Mwenge kutopita tena hiyo njia ili wasije kufanywa 'Kitoweo' Kitamu cha Chatu huyo.

Baada ya kupata Taarifa hii GENTAMYCINE niliamua kutembelea eneo la Makazi ya Watu ambapo nilibahatika Kukutana na Vijana Wawili ambao hupenda kupita hiyo njia ambao walinithibitishia kuwa ni Kweli Chatu huyo yupo na ni Mkubwa sana ambapo mara nyingi hupenda Kukaa juu ya Makaburi yaliyopo hapo.

Kumekuwa na Taarifa mbalimbali juu ya uwepo (ujio) wa huyo Chatu hapo ambapo wapo wanaosema kuwa alianza Kuonekana tokea mwaka juzi akiwa bado Mdogo baada ya Kutupwa huko Porini (Msituni) Lugalo na Wasukuma waliokuwa wakiwafuga wengine na kuwatumia katika Ngoma zao za Kitamaduni.

Watu wengine wanasema kuwa kuna uwezekano Chatu huyo akawa ameletwa na Maji ya Mto Mlalakuwa yanayopita hadi jirani na Kambi ya Lugalo, kule Golf Club mpaka JKT Mlalakuwa hivyo akanasa na kuamua kuanza Maisha yake eneo hilo.

Katika hali isiyokuwa ya Kawaida baada ya Watendaji wa Serikali ya Mtaa Kawe ( yenye Ofisi zake jirani na Soko jipya la Kawe ) walipotaarifiwa 'walijitutumua' kutaka kuonyesha 'Ushujaa' ambao hawana kwa kuamua kwenda 'Kavu Kavu' huko Msituni ( Porini ) Lugalo ( zamani Hostel ) ili Kumdhibiti.

Ila walipofika huko na Kumuona ndani ya dakika Moja mpaka Mbili hakuna aliyebakia hapo ambapo wote 'walitimka mbio' kwa kila Mtu kupita njia anayoijua ila Wote wakaja kukutania Ofisini huku wote wakiwa wameshika Viatu vyao Mikononi na wengine wakiomba Funguo za kwenda Msalani ( Chooni ) kujikagua kama wakati wakikimbia vile kwa Uwoga wa Kumuona Chatu labda kwa kutokujua ( Kihoro ) walijisaidia 'Kibaiolojia' vile walivyovihifadhi katika 'Vitambi' vyao.

Tafadhali naziomba Mamlaka husika hasa ya Jeshi (JWTZ) na Serikali ( kupitia Maliasili ) kulifuatilia hili upesi na Kumtoa upesi huyo Chatu hapo Porini ( Msituni ) kwani wengine ( GENTAMYCINE ) katika hayo Makaburi ( ya zamani Hostel ) nimemzika Mama yangu Mdogo na nilikuwa napanga kwenda 'Kumfagilia' na Kumsalimia 'Kimaombi' Siku za Usoni.

Lakini Taarifa hii imenishtua na Kuniogopesha kwenda huko ili Chatu asije 'Kuupiga Mwingi Kwangu' na nikawa Historia hapa JamiiForums na hata nikaikosa 'Derby' ya Jumapili ijayo huko Mkoani Kigoma ambapo najua Mugalu, Boko, Chama, Kagere na Miquissone wanaenda 'Kuninyooshea' na Kunifundishia Watu Adabu kwa Kipigo cha Mwana Ukome.

Kwa wale wenye Blogs zenu na Media zingine mbalimbali tafadhali siwazuii Kuichukua hii Taarifa yangu na Kuitumia ila nawaomba tu mkiitumia toeni 'Credit' kwa Mtandao huu wa JamiiForums na Mimi GENTAMYCINE niliyeileta ( iweka wazi ) na acheni Kudanganya kuwa mmeitafuta nyie kwani mnakuwa hamtendi Haki na Kutuvunja Moyo Watu tunaopenda Kutafuta Taarifa na Kuzianzishia hapa JamiiForums mzijue hata kama hakuna tunacholipwa ila tunajua tutalipwa vikubwa (zaidi) na Mwenyezi Mungu Siku moja atakayoipenda na kuichagua Yeye.
 
Jeshi tena?
Sasa watamuuwa tena kama yule

Kama ametupwa na watu walioshindwa kumhudumia
Wamkamate wampeleke Zoo badala ya kumuuwa
Mwisho wataisha kama kila mmoja akionekana anauwawa
Au unasemaje
Nami nimeshauri wasimuue bali waombe Msaada wa Watu wa Maliasili ili wamkamate na wampeleke huko katika hizo 'Zoo' zenu na najua hili litafanyika.
 
Eti mtu aliyekimbia ajali Goba anawacheka watu waliokimbia Chatu😂😂..Kuna mambo yanashangaza kwakweli
 
samaki mkunje angali mbichi, alikuwa anakula Nini hapo siku zote, isije ikawa katafuna mifupa ya ndugu yako😄😄😄😄
Hilo eneo lenye Pori ( Msitu ) hapo Lugalo ( zamani Hostel ) kulikuwa na Tumbiri wengi na sasa hawaonekani tena huenda ndiyo alikuwa akiwala.

Hata hivyo Mimi bado napatwa na Mashaka makubwa kwani japo sina Utaalam wowote ule wa Wanyama ila niliwahi kusikia kuwa Chatu huwa hapendi Kukaa sehemu zenye Kelele na hilo eneo pembezoni mwa Msitu huo ( Pori hilo ) huwa kunakuwa na Pilikapilika nyingi za Kibinadamu na Kelele kibao tu.

Natamani sana Uzi huu uvamiwe na Wataalam wa Wanyama ili wanipe Elimu zaidi juu ya hili ila Mimi nilivyoambiwa tu kuwa kuna Wasukuma waliokuwa wakiishi Jirani hapo haraka sana kwa Kuwajua Wasukuma na Mahaba yao kwa Nyoka ( hasa Chatu ) kwa 'Ndumbaism' yao nikajua huenda huyu Chatu alikuwa ni Mlinzi ( Bodyguard ) hapo walipokuwa wakiishi.

Na kinachonishtua zaidi japo inasadikiwa kuwa yupo hapo kwa muda ila hatujasikia ama Binadamu yoyote au Mfugo wowote Kupotea kwa 'Kuliwa' nae na hata waliomuona wanasema hupenda Kukaa juu ya Makaburi kisha kutokomea na hazuru hivyo sijajua labda ameshiba Kala Kitu au pengine ni Chatu Mwanadamu Mwenzetu.
 
Eti mtu aliyekimbia ajali Goba anawacheka watu waliokimbia Chatu😂😂..Kuna mambo yanashangaza kwakweli
Wewe Pimbi naona ule Uzi wangu wa Mimi kutoka Baru ( Kukimbia ) eneo la Ajali Goba umekukaa mno Kichwani na hutosahau Maishani mwako au?

Sijashangaa hawa Watendaji wa Serikali za Mitaa Kawe Mzimuni Kukimbia hivyo ila kilichonishangaza tu ni kwamba walipotaarifiwa uwepo wake Chatu huko 'walijimwambafai' na 'kujitutumua' kuwa 'wanammudu' ila walipofika huko na Kumuona kwa mbali wakaanza kugawana Mitaa ya Kawe Mzimuni kwa 'Kukimbia' japo kwa muda mfupi wote walikutania Ofisini huku kila Mmoja akielezea Spidi aliyotumia na dakika alizotumia pia.
 
nakumbuka kijijini tushawahi ona chatu akinyonya maziwa ya ng'ombe, watu wakasema ametumwaaaaa, akaishia kula kichapo na kuokwa motoni
 
Hilo eneo lenye Pori ( Msitu ) hapo Lugalo ( zamani Hostel ) kulikuwa na Tumbiri wengi na sasa hawaonekani tena huenda ndiyo alikuwa akiwala.

Hata hivyo Mimi bado napatwa na Mashaka makubwa kwani japo sina Utaalam wowote ule wa Wanyama ila niliwahi kusikia kuwa Chatu huwa hapendi Kukaa sehemu zenye Kelele na hilo eneo pembezoni mwa Msitu huo ( Pori hilo ) huwa kunakuwa na Pilikapilika nyingi za Kibinadamu na Kelele kibao tu.

Natamani sana Uzi huu uvamiwe na Wataalam wa Wanyama ili wanipe Elimu zaidi juu ya hili ila Mimi nilivyoambiwa tu kuwa kuna Wasukuma waliokuwa wakiishi Jirani hapo haraka sana kwa Kuwajua Wasukuma na Mahaba yao kwa Nyoka ( hasa Chatu ) kwa 'Ndumbaism' yao nikajua huenda huyu Chatu alikuwa ni Mlinzi ( Bodyguard ) hapo walipokuwa wakiishi.

Na kinachonishtua zaidi japo inasadikiwa kuwa yupo hapo kwa muda ila hatujasikia ama Binadamu yoyote au Mfugo wowote Kupotea kwa 'Kuliwa' nae na hata waliomuona wanasema hupenda Kukaa juu ya Makaburi kisha kutokomea na hazuru hivyo sijajua labda ameshiba Kala Kitu au pengine ni Chatu Mwanadamu Mwenzetu.
Huyo ni mtu wa kusaka utajiri,
 
Nitasikitika sana kusikia chatu kauliwa kisa maliasili walichelewa kupata taarifa
Nasikia kwa Sheria zilizopo Kuuliwa na Chatu au Mamba ni rukhsa ( bahati mbaya ) ila Wewe Mtanzania ukiwauwa ni Kesi ya Uhujumu Uchumi kwa Kuharibu Nyara za Serikali.
 
Wewe Pimbi naona ule Uzi wangu wa Mimi kutoka Baru ( Kukimbia ) eneo la Ajali Goba umekukaa mno Kichwani na hutosahau Maishani mwako au?

Sijashangaa hawa Watendaji wa Serikali za Mitaa Kawe Mzimuni Kukimbia hivyo ila kilichonishangaza tu ni kwamba walipotaarifiwa uwepo wake Chatu huko 'walijimwambafai' na 'kujitutumua' kuwa 'wanammudu' ila walipofika huko na Kumuona kwa mbali wakaanza kugawana Mitaa ya Kawe Mzimuni kwa 'Kukimbia' japo kwa muda mfupi wote walikutania Ofisini huku kila Mmoja akielezea Spidi aliyotumia na dakika alizotumia pia.
😀😀Aisee kutokana na story zako humu miaka yote huwa naamini wewe ni bonge la jasiri na unaweza kupita na roho ya popoma yoyote anayepita kwenye anga zako...ila ule uzi umeniprove wrong na sitousahau kamwe
 
Inasikitisha sana!! Wasimuue wamkamate na kumpeleka zoo ,yule mwanajeshi aliyemuua chatu inatakiwa akamatwe! Lugalo nimekaa ila Hostel sisijui zipo wapi.
 
Anakaa juu ya makaburi kuota jua kwakua nyoka hiyo ndiyo namna yake ya kupata joto.

Hivyo jua la alfajiri na jua la jioni litakua linamkuta juu ya makaburi.
 
Genta buana

Maneno mengiii kazi kidogo
Nina 'Style' yangu ya Uandishi na Uwasilishaji wake Wewe inakuuma nini? Kama huvutiwi nao huwa unahangaika nini Kusoma hadi Kujibu 'threads' zangu hapa JamiiForums?

Hujaanza 'Kuwashwawashwa' nami leo na inaonekana kuna unalolitafuta Kwangu hivyo endelea tu na utalipata sawa? Hujajaa vizuri katika 'Frame' nasubiri ujae ili nikupe 'Kitu' cha Kukufanya si tu Ukasirike bali Unichukie na Uichukie Milele hii ID yangu.

Nakustahi kwa Upako wa Ibada ya Jana.
 
Back
Top Bottom