Azania Secondari imebinafsishwa?

amba.nkya

JF-Expert Member
Jan 7, 2010
446
131
Shule ya Sekondari Azania iliyopo jijini Dar ni miongoni mwa shule za umma (serikali) hapa nchini.
Mkuu wa shule hiyo kwa sasa ni Mwl. Benard Ngoziye ambaye uongozi wake kwa muda mrefu unalalamikiwa na wanafunzi, waalimu,wazazi/walezi na hata waalimu wenzake wa sekondari nyingine kiasi cha kuhatarisha hadhi ya Sekondari hiyo kongwe.

Miongoni mwa malalamiko ya Mkuu huyo wa shule ni kamaifuatavyo:
1. Kuendesha shule hiyo kibabe na kujifanya yeye ni Mungu mtu kwa maana ya kutokuwa na mahusiano mazuri na waalimu na wanafunzi kutokana na kujiamuliwa mambo atakavyo.
2. Kutoitisha vikao vya wazazi na wanafunzi vya kujadili masuala ya shule hiyo kama ambavyo shule nyingine zinavyofanya
3. Kugawa vyumba vya bweni kwa rushwa ikiwa ni pamoja na kuwapa vyumba wanafunzi kutoka nje ya shule hiyo ilhali wanafunzi wake kukosa nafasi shuleni hapo.
4. Wanafunzi kulipishwa michango ya mahafali 20,000/= sawa na ada ya shule kwa mwaka mzima (kutwa)
5. Baadhi ya wanafunzi wamelipishwa michango kama ya vitambulisho, madawati, n.k lakini kwa takribani ni mwaka sasa hawajapata vitu hivyo bila kutolea maelezo.

Hayo ni baadhi tu ya malalamiko dhidi ya Mwl. Benard Ngoziye, Mkuu wa Sekondari ya Azania.
Kutokana na malamiko hayo ndio tunajiuliza Azania Secondari imebinafsishwa kutoka kuwa sekondari ya umma na kuwa mali ya Mkuu huyo wa shule?

Malalamiko hayo yamefanyiwa utafiti na yana ukweli, hivyo mamlaka husika zinapaswa kufuatilia na kuchukua hatua stahiki kabla ya wanafunzi wakishirikiana na wazazi/walezi wao hawajaamua nini cha kufanya dhidiya udhalimu wa Mkuu huyo wa shule.

Source: Wadau wa Azania Sekondari
 
Watu waache uoga wakae na mkuu wao waongee. Shule haitoi progress report za wanafunzi.
 
mhh, mi nilidhani imenunuliwa na matajiri, kumbe ni mchango wa mahafali....walimu wa sekondari siku hizi ni watoto watoto (masharubaru) hakuna haja ya kujadiliana kitu
 
mhh, mi nilidhani imenunuliwa na matajiri, kumbe ni mchango wa mahafali....walimu wa sekondari siku hizi ni watoto watoto (masharubaru) hakuna haja ya kujadiliana kitu

Hata mimi niliogopa kwani ni hapo nilipopata elimu yangu inayonisukuma mbele hivi sasa. Hakuna haja kama ulivyosema yawezekana ni chuki binafsi
 
mhh, mi nilidhani imenunuliwa na matajiri, kumbe ni mchango wa mahafali....walimu wa sekondari siku hizi ni watoto watoto (masharubaru) hakuna haja ya kujadiliana kitu
Ndumbayeye, mkuu wa shule ni mzee wala sio kijana a.k.a sharo
 
Hata mimi niliogopa kwani ni hapo nilipopata elimu yangu inayonisukuma mbele hivi sasa. Hakuna haja kama ulivyosema yawezekana ni chuki binafsi
sio chuki binafsi tuache uvuvi wa kufuatilia issues muhimu kama hizi na umeambia ni taarifa za kweli zilizofanyiwa utafiti kwa muda mrefu, otherwise, ungepita tu bila kuchangia.
 
suala la kugawa vyumba kwa wasiokuwa wanafunzi wa Azania limepitiliza viwango vya ufisadi. AONDOLEWE fasta.
 
aza pound au U.S.A(UNITED STUDENTS OF AZANIA) ya miaka ya tisini hadi 2000 sio hio ya sasa.shule imekuwa na masharobaro utafikiri ni watoto wa shebeduu au forodhani wa enzi hizo wapaka poda.
 
Enzi zile tulipokuwa tunasoma pale, sidhani kama huyo mkuu wa shule angeweza kufanya hayo yanayofanyika kwani wanafunzi tulikuwa na 'nguvu' kuliko hata walimu.
Muda huu angeku kashaomba ahamishwe kama si kuacha kazi.
 
Ila vijana wa siku hizi ni masharobaro na waoga kweli kweli!
Kweli mnashindwa kutandika kunji moja la nguvu adi huyo joka atoke pangoni kweli?
 
Ila vijana wa siku hizi ni masharobaro na waoga kweli kweli!
Kweli mnashindwa kutandika kunji moja la nguvu adi huyo joka atoke pangoni kweli?

watoto wa sasa wanamaliza darasa la saba na wanaingia sekondari wakiwa na umri mdogo ukilinganisha na huko nyuma, hivyo sidhani kama wataweza kufanya hiyo kunji.
 
Nimemkumbuka mkuu wangu wa shule enzi zetu mzee Andrew Kwayu. Mungu ikomboe Azania.
 
Back
Top Bottom