Azam Fc Vs Yanga, 12/06/2023, Match ya kisasi, Ubabe na heshima

Beberu

JF-Expert Member
Jan 26, 2017
3,945
7,947
Habari ya muda huu ndugu msomaji wa Jamiiforums,

Baada ya kuwafunga Watoto wa tajiri namba moja hapa Tanzania (According to Forbes) kwa mabao 2-1, vijana wa tajiri asiependa kelele hapa mjini SSB Azam Fc walijihakikishia nafasi ya kucheza mchezo wa mwisho (Final) ya michuano inayodhaminiwa na baba yao (Azam FA cup).

Upande wa pili Beka mkubwa na Beka mdogo nao walivaana ambapo Beka mkubwa akapata ushindi wa 1-0 hivyo kujihakikishia nafasi nao ya kucheza mchezo wa mwisho (final) wa Azam FA cup kwa mwaka huu 2023 pale jijini Tanga. Hawa ni Yanga (Beka mkubwa)

Picsart_23-06-06_18-49-38-817.jpg

Fainali ya msimu huu ni kati ya Azam fc dhidi ya Yanga SC

Kwa Tanzania hapa ukitoa derby ya Kkoo bas match nyingine yenye hisia za chuki, ubabe, undava na kila kitu ni hii ya Azam Fc Vs Yanga, Ugomvi wao ulianzia mbali na mimi kidogo naomba nikukumbushe baadhi ya vitu vinavyochochochea ugomvi na kufanya match hii kuwa ya Kisasi, Ubabe na heshima

#1. Issue ya Ngassa, Azam ndo walianzisha ugomvi kwa kumchukua mchezaji tegemeo kipenzi cha Yanga tena akiwa kwenye ubora wake, Huyu ni Mrisho Khalifan Ngassa, walimpa mshahara wa 1.2M (kipindi hicho watu wanalipwa aftatu, hivyo hii ilikuwa kufuru) na kisha kuwapa yanga 58M (hii nayo record kwa wakati ule. Yanga bado wanaumia, wanaona walidhalilishwa sana na Azam 💔 ( ina ukweli hii).

Picsart_23-06-06_19-04-43-558.jpg

Mrisho Ngasa akiwa azam Fc alipewa jersey ya Yanga akaibusu, hii ilisababisha hasira kwa matajiri hao wakaamua kumpeleka Ngasa Simba SC

#2. Issue ya Israel Nkongo, kwa watoto wa Juzi, ngoja niwasilimue bana, ilikuwa ni March 11 mwaka 2011, pale taifa kulikuwa kulikuwa na match ya matajiri wa Chamazi dhidi ya vijana wa Africa (Young Africans) siku ile kulikuwa na hali ya mvua kidogo hapa Dar, ile match Mwanzo ulikuwa ni mchezo mzuri uliokuwa wa vuta nikuvute kwa kila upande lakini mambo yalibadilika mara baada ya Azam kuandika goli la kwanza,
Mchezaji Haruna Niyonzima wa Yanga alionekana kumlalamikia refa mara kwa mara jambo ambalo refa alimuonya mara kadhaa lakini, hata hivyo Niyonzima aliendelea baada ya muda akalambwa kadi nyekundu, jambo ambalo lilizua tafrani uwanjani huku makonde yakirushwa hovyo, baadae naye mchezaji Nadir Haroub Canavaro alipewa kadi nyekundu kutokana na vurugu hizo na kuzua tifu lingine uwanjani ambapo wachezaji wa Yanga walimshambulia sana refa wa mchezaji ule Israel Nkongo na hivyo kupelekea kupigwa faini na TFF. Mchezo uliisha kwa yanga kuchabangwa bao 3-1
Yanga hawajawahi sahau hii issue na daima wanahisi walionewa, hivo kila wakikutana na Azam lazima wacheze kwa hasira sana na kujituma wakiamin wanahitaji kulipiza kisasi kwa ajiili ya match ile 😂😂
Picsart_23-06-06_18-54-03-124.jpg

Wachezaje wa Yanga wakimpa kipondo mwamuzi

Licha ya kuwa yapo mambo mengi baina ya vijana hawa wa Dar Es Salaam yanayopelekea match yao kuwa ya Jasho na damu lakini match yao ni moja kati ya match ambazo zinatawaliwa na ufundi mkubwa, na ni match nzuri sana kuzitazama (Match ya simba na Yanga huwa sio nzuri kuitazama, haina ufundi sana).

Tarehe 12.06.2023 ni zamu ya nyasi za dimba la mkwakwani Tanga kuumia wakati miamba hii ya jiji la Starehe na laana watapoumana hapo kupigania kombe la Azam Sports Federation Cup.

Azam anataka kushinda ili aonekane ni mkubwa na ajione mbabe, wakati Yanga nae anataka kulipa kisasi kwa madhira yote ambayo Azam amewahi kumfanyia.

Kwa kifupi ni match ya
KISASI, UBABE NA HESHIMA ,

usipange kuikosa match hii, huwa ni match tamu sana.

Nakaribisha maoni yako, wew unaiona hii match ikiwa na matokeo gani 🤔 nani atashinda?

Binafsi ni mshabiki mkubwa matajiri wa Chamazi Azam Fc
Wenu yule yule Beberu J
 

Attachments

  • Picsart_23-06-06_18-49-35-901.jpg
    Picsart_23-06-06_18-49-35-901.jpg
    311.5 KB · Views: 8
Azam WAKIFUNGWA FAINALI nalala NAO MBELE.

Hii Mechi nitauomba uongozi ssc waiingilie kati.

HAIWEZEKANI Azam wapoteze Huu mchezo.
Mashabiki wa simba mnatakiwa kuwa watulivu katika hiki kipindi kigumu mnachopitia. Hamtaki Azam wapoteze, na wakati nyinyi wenyewe mlipoteza kwao! Tena muuaji akiwa ni yuleyule wa siku zote, Prince Dube?

Si mngewafunga hao Azam kwenye mchezo wa nusu fainali ili muambulie hata medali tu za mshindi wa pili!! Hivi mnajisiakiaje kumaliza msimu wote wa ligi huku mkiwa hamna hata kikombe kimoja?
 
Azam kwa Yanga hawana mwendo, huwa wanatepeta km sio wao vile.

Walipigwa na Namungo majuzi kati hapa, aaah
Wanakuwaga na bahati ya kuifunga simba tyuuh.
Sio kweli mkuu, tafuta H2H ya Azam Vs Yanga match 15 zilizopita ndo utajua kuwa hii match hainaga mwenyewe
 
Azam WAKIFUNGWA FAINALI nalala NAO MBELE.

Hii Mechi nitauomba uongozi ssc waiingilie kati.

HAIWEZEKANI Azam wapoteze Huu mchezo.
Match itakuwa ngumu, Yeyote atashinda, undava mwingi utafanyika
 
Mashabiki wa simba mnatakiwa kuwa watulivu katika hiki kipindi kigumu mnachopitia. Hamtaki Azam wapoteze, na wakati nyinyi wenyewe mlipoteza kwao! Tena muuaji akiwa ni yuleyule wa siku zote, Prince Dube?

Si mngewafunga hao Azam kwenye mchezo wa nusu fainali ili muambulie hata medali tu za mshindi wa pili!! Hivi mnajisiakiaje kumaliza msimu wote wa ligi huku mkiwa hamna hata kikombe kimoja?
Simba vibonde 😂
Sema na niny Yanga mtapigwa tu fainali 😂😂
 
Sio kweli mkuu, tafuta H2H ya Azam Vs Yanga match 15 zilizopita ndo utajua kuwa hii match hainaga mwenyewe
Azam hana ubavu kwa Yanga, hata ukisema tufatilie hizo records, sasa mie ndo nakuambia Yanga atashinda tena ndani ya dkk 90, afu huo mchezo utakavyokua utakuja uniambiee.
 
Back
Top Bottom