Awamu ya Tano imekwisha kwama, Imejitia ulimi puani...

Kila mtu sasa ni mchambuzi wa sayansi ya siasa. Matokeo yake ndio haya.
Ndugu nimesoma sayansi ya siasa na uchumi kiwango cha juu hatua za mwanzo chini ya prof Mkandara,Samweli Mushi,Max muya ,Sirku Heltein,Mkangara na wengineo kabla ya kufanya MBA na docorate si mpuuzi mwenzio.
 
Wasio angalia mambo kwa kina wanaweza wakakutukana.
Mkuu umesahau kuna wale vijana 46 alosema mkwere wapo humu..kazi yao ndo hiyo ya kutukana.

hivyo usishangae kwa jambo muhimu kama hili Wao hawana muda wa kufikiri..ni kutukana tu
 
Angalia mikakati yake ya kiuchumi na Angalia dhamira yake na kumbuka anazo bado miaka 4 na siku 260. Ukishafanya hivyo tulia mpaka mwaka kesho desemba ufanye tena tathmini yake.
jenga amani kwa siasa safi imarisha uhusiano wa kimataifa utâenda. Kiburi cha ndani na cha kimataifa kitaturudisha nyuma uwe ccm uwe ukawa
 
Mbona hayo unayoyasema ni matatizo ya muda mrefu ambayo hata yeye jana kayazungumzia? Hivi kweli hayo ni matatizo ya kutatua ndani ya siku 100 katika nchi ilokwisha kuoza kila mahari? Mimi nafijiri haya tumhukumu baada ya miaka mitano kuisha. Tuone kama naye atarudi kwetu kutuomba kura 2020 akatatue matatizo ya wanafunzi kukaa chini na wagonjwa kulala chini au kukosa madawa.
Uliwahi kukosoa awamu ya nne? si ulikua unazuia na kutukebehi? kwa malipo?mchangia hoja wa kulipwa si mtumwa tu? hujui unatulaza sakafuni?
 
mkuu unayoyaongea yataka jicho la tatu wengi hawatakuelewa hii ni nchi ya Sanaa (maigizo) na kusadikika
 
Wavaa tisheti na kofia na wazee wavivu wa pale Lumumba ndiyo wanao mpigia makofi Dr JPM ila wale wenye jicho la tatu bado tunaona ni mkorogo tu,
 
Mbwembwe za kutumbua majipu, sioni hata jipu alilotumbua. Yeye mwenyewe jipu (nyumba za serikali). Kipindi cha kampeni tukaambiwa amesusia chakula alichoandaa Chenge kwakuwa ni fisadi, lakini leo nashangaa Chenge ni Mwenyekiti wa Bunge letu Tukufu. Unafiki ni mbaya sana.
 
Magufuli ni total disaster mpaka sasa hajatengeneza mfumo wowte wa kuongeza njia za uchumi zaidi yakutafuta sifa tuu yote anayoyafanya sasa yaliongewa na wapinzani kwenye ripoti zao, na kamati za bunge sasa atatekeleze kusahihisha lakini sio kujifanya yeye hakuwa sehemu ya uzo wakati miaka ishirini yumondani ya serikali mbona hakujiuzuru kama ni mwadilifu kihivyo he is just a camera monger very pity
 
Hela anazojidai nazo magi eti anazibana unafikiri nani anazilipa?Ni kodi zetu. Kwahiyo jibu unalo. Siku 100 za awamu ya tano watz tumelipa kodi. Swali kwako. je magu na serikali yake wamezifanyia nn hizo kodi zetu ndani ya siku 100
Magu na team yake wamezikusanya na wanazitumia kwa ajili ya huduma zingine, so endelea kulipa kodi.
 
kutegemea mabadiliko ndani ya CCM ni sawa na kutafuta bikra ndani ya wodi ya wazaz
 
Nafikiri basi wala haujaelewa jinsi mfumo mzima wa nchi yetu ulivyo, ni hivi tuna mfumo kwa CCM unaitwa wa kupokezana vijiti na kila Raisi anachukuwa alipoachia mwenzake na mafanikio ya Raisi mmoja siyo ya kwake binafsi bali yanatokana na sera za Chama yaani CCM hivyo kama Raisi Kikwete alijenga daraja Raisi Magufuli ana kila sababu ya kumsifia na kujivunia na ndiyo maana analiendeleza mpaka mwisho, na hakuna tatizo lolote hapo na isitoshe Raisi Magufuli ana miezi 3 madarakani usisahau hilo, kwa maana inawezekana umaarufu wa Raisi ukakufanya kusahau kwamba ana siku 100 tu!
Sera za ccm ni wizi na unafiki
 
USIDHANI KUWA KUNA WACHACHE NI WENGI TUSIOPENDA AINA YA SIASA ZA AWAMU HII ndio tafsiri ya kujitia ulimi puani .CUF pekee ni jamii pana . Huwezi kuwa ignore. Waumini wa democracy ni wengi pia.Wasiopenda vitisho ni wengi mno bila kujali vyama
Pole sana, naamini kwa uwezo wa rais wa awamu ya tano, wewe utabaki na maumivu moyoni kwa miaka 10, kwa hiyo inabidi uanze kuzoea hii hali, hakuna namna ya kukusaidia.
 
Back
Top Bottom