Awamu hii kuna displacement kubwa inakuja hasa Wilaya za Simanjiro, Longido na Monduli

SOVIET UNION

JF-Expert Member
Sep 2, 2017
455
1,283
Kuna wimbi la Wazungu wanapigana vikumbo kutaka hekari na hekari za maeneo kwenye wilaya za Monduli, Simanjiro na Longido, na sana Simaniro na Longido ndizo wilaya zinaweza poteza robo tatu ya vijiji vyao kwa kupewa wazungu.

Kwa walio Simanjario nazani kazi ishaanza muda sio mrefu utasikia wamasai wanatafutiwa eneo labda Lindi huko au Mtwara.

Wilaya ya Longido kuna uwezekano ikafutwa kabisa kwa sababu robo tatu yake inahitajika na tajiri wa Kimarekani ili kuifanya kuwa hifadhi private, hivyo kwa sehemu inayo bakia ni ndogo sana ambapo ni Longido mjini pale, Namanga na West Kilimanjaro maeneo ya Olimologi.

Hizi ni habari za chini ya kapetu, ila kwa walioko kwenye systeam wanazijua sio tetesi bali ni mambo yanangoja muda tu, mtakumbuka Olesendeka Mbunge wa Simanjiro aliwahi tamka Bungeni kwamba Serikali inataka kuwahamisha wamasai wote wa Wilaya za Simanjiro, Longido na Sehemu ya Monduli.

Na Sababu ya kwa nini Wamasai wa Ngorongoro hawakupelekwa wilaya za Simanjiro na Longido pamoja na kuwa na eneo kubwa ni kwa sabanu hizi wilaya nazo raia wake watahamishwa, kumbuka wilaya ya Simanjiro ni kubwa kiliko Mkoa wote wa Kilimanjro.

Binafisi naunga mkono uwekezaji ila sikubaliana na uwekezsji wa kuua vijiji na kuhamisha raia ili kupisha uwekezaji, na raia wa hizi wilaya wasipo amua kufia kwenye wilaya zao watahamishiwa hata Lindi huko au Mtarwa.
 
Kama ni kweli yote haya basi serikali nzima imeoza. Zanzibar wao hawaruhusu mtanganyika mumiliki ardhi lakini huku wakipata vyeo wanaanza kuuza mapande mapande makubwa ya ardhi!Hii haikubaliki kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tuna eneo kubwa sana, kama maslahi Yao hayatakiwa compromised wahamishwe tu bila..

Hata Mimi nikipata mwekezaji kwenye eneo langu nakuuzia fasta maana unakuta eneo potential harafu Sina pesa ya kuendeleza nabania la nini?

Vuta mpunga fanya mambo mengine.

Tahadhari, huo uwekezaji uhusishe Mali zilizo Juu ya Ardhi tu na sio vinginevyo maana kesho na kutwa wanaweza gundua Madini chini ya Ardhi ila mkikodisha kienyeji tutabakia Wapenzi watazamaji na Mali zinasombwa..
 
Awamu hii imejaa uovu.

Ila Mungu atawalaani wao na familia zao milele.

Wakiwagusa tu hao wamasai Mungu awalaani na vizazi vyao .
 
Back
Top Bottom