Avumaye Baharini ni Papa: Kagera Sugar wahamia ShyTown kisa, ushirikina!

Makoye Matale

JF-Expert Member
May 2, 2011
6,491
2,104
Soka letu la Bongo liko katika msukosuko mkubwa wa imani za kishirikiana. Mara kwa mara Yanga imekuwa ikitajwa kujihusisha na vitendo vya ushirikina hasa baada ya Kavumbagu (akiwa Yanga) kugombania taulo la Ivo Mapunda likidaiwa kuwa linawazuia Yanga kupata magoli, vile vile kasi ya kuituhumu Yanga imeongezeka baada ya shabiki mmoja kuondoka na gloves za kipa wa timu moja ya Zanzibar na muda mfupi Yanga ikaandika bao moja la ushindi.

Kagera Sugar kutoka wilaya ya Missenyi mkoani Kagera nao wameingia katika rekodi za wanaoamini ushirikina baada ya kuukimbia uwanja wa CCM Kirumba uliopo Jijini Mwanza kwa madai kuwa wanarogwa na Toto Africans ya Mwanza. Kagera Sugar wamekimbilia katika uwanja wa CCM Kambarage uliopo katika Manispaa ya Shinyanga. Uamuzi huo umefikiwa baada ya timu hiyo kupoteza michezo mitatu mfululizo dhidi ya Mbeya City Council FC, Azam FC na Ndanda FC.

Uongozi wa Kagera Sugar umeamua kuhamia mkoani Shinyanga na kuachana na Uwanja wa CCM Kirumba kwa kile kilichotajwa kurogwa na wenyeji wa uwanja huo, Toto African, kwa sababu zilizotajwa kuwa waliapa kuhakikisha Kagera haitoki na pointi uwanjani hapo.

Chanzo cha bifu lao ni kwamba Toto wanalipiza kisasi cha Kagera kuwabania misimu miwili iliyopita ambapo iliwafunga katika mchezo wa mwisho, kichapo kilichowashusha daraja Toto African licha ya Kagera tayari ilikuwa imejihakikishia pointi za kubaki ligi kuu.

Kagera Sugar ilihamishia maskani yake kwenye Uwanja wa Kirumba, kutokana na uwanja wao wa nyumbani, Kaitaba, kuwa katika matengenezo lakini vichapo vitatu mfululizo kutoka kwa Azam, Mbeya City na cha juzi dhidi ya Ndanda vimewatia shaka.

Chanzo cha habari kutoka ndani ya Kagera, kimesema kuwa wamekubaliana kuhamia mkoani Shinyanga ambapo mechi zao zote watachezea mkoani humo.

"Waswahili wanasema lisemwalo lipo, sawa, hakuna mwenye uhakika na kinachosemwa, lakini kadiri mechi zinavyokwenda, tunazidi kuingiwa na hofu. Tulianza kusikia watu wa Toto wakisema hivyo katika mechi ya kwanza na Mbeya, maneno hayo yakaendelea kwenye mechi zilizofuatia, lakini sasa tumeanza kuamini. Kila mmoja anaujua uwezo wa Kagera, kabla ya kuja Mwanza ilikuwa imepoteza mechi moja tu kati ya nane.

"Hivi kweli sisi ndiyo wa kufungwa mechi tatu mfululizo? Haijawahi kutokea timu hii ifungwe namna hii, tumeanza kuamini imani za kishirikina kama siyo mbinu chafu za wenyeji wetu wanazotuambia hadharani," alisema mtoa habari.

Alipotafutwa Mratibu wa Kagera, Mohammed Hussein, alikiri kusikia maneno hayo na kuongeza kuwa tayari wamehamishia makazi yao mkoani Shinyanga.
"Ni kweli nimeyasikia maneno hayo si mara moja na tumeamua kuhamia mkoani Shinyanga ambapo mechi zote tutakuwa tukichezea huko," alisema Hussein.

Chanzo: SALEH JEMBE

Chanzo: KISA SUALA LA USHIRIKINA, KAGERA SUGAR YAKIMBIA KIRUMBA - SALEH JEMBE

Wadau wa soka mnasemaje kwa maamuzi kama haya? Je, ni kweli Toto Africans wanawaroga Kagera Sugar ili wapoteze michezo yao hapo CCM Kirumba? Kama Toto Africans wana uchawi mkali kama huo kwa nini haukuwasaidia kuzifunga timu zote zilizocheza CCM Kirumba ili wasishuke daraja? Viongozi wa timu wenye maono, imani na maamuzi kama haya wanalipeleka wapi soka letu?
 
Sishangai kwani Toto Africans ni ndugu na nani vile? Embe halianguki mbali na mti wake.
 
Mkuu hujatumia weledi hata kidogo, Toto Africans wanatuhumiwa, wanaotuhumu ni Kagera Sugar, hao unawaambia nini?
 
Mkuu mimi nawatuhumu wachawi. Na narudia embe halianguki mbali na mti wake.Like father like son.
 
Kagera walizoea ka uwanja kao ka fitna sasa wameenda kirumba uwanja bomba wameshndwa kufanya fitna zao
 
Hata kama kweli Toto Africa ni wachawi bado hainingii uwanjani kwa nini wawaroge Kagera Sugar? Wao Toto wanafaidika na nini endapo Kagera wakifungwa na hata kama watashuka daraja? Kwa nini kama uchawi huo wanao walishindwa kuutumia msimu uliopita ili wasishuke daraja au kuutumia kwa sasa kwenye mechi zao ili wajihakikishie kupanda daraja mapema kabla hata ligi haijaisha?

TFF inalea uozo na kama kweli Kagera watahama uwanja kwa sababu hiyo na kusababisha kuanza kupangua ratiba (naamini kuna mechi ambazo ziko siku moja kwa Kagera na Stand wote wakiwa wenyeji) ili tu Kagera na Stand ziwafae tutakuwa hatuna uongozi wa shirikisho. Kila siku tumekuwa tukisikia timu fulani imepigwa faini kwa sababu ilionyesha vitendo vinavyoashiria ushirikina je kwa timu kuhama uwanja kwa sababu ya ushirikina na TFF na bodi ya ligi kuruhusu basi inabidi nao wote watatu wapigwe faini kwa kujihusisha au kubariki vitendo vya kishirikina. Na siku ikitokea timu nyingine imekataa kwenda kucheza uwanja fulani kwa sababu imeshaona kuna dalili za kufanyiwa ushirikina basi TFF na bodi ya ligi waone ni jambo la kawaida na ikiwezekana hito mechi iahirishwe na kupangiwa siku nyingine na uwanja mwingine.
 
Walipoifunga Simba sc hapa dar walitumia uwanja wa kaitaba ?

Tatizo ni moja. Simba walifungwa na kukubali kimchezo. Hawakuja na falsafa za kulogwa. Mpira una matokeo matatu.Kushinda,kudroo na kufungwa. Mbona waliposhinda hatusikia hekaya za😈uchawi?
 
Hata kama kweli Toto Africa ni wachawi bado hainingii uwanjani kwa nini wawaroge Kagera Sugar? Wao Toto wanafaidika na nini endapo Kagera wakifungwa na hata kama watashuka daraja? Kwa nini kama uchawi huo wanao walishindwa kuutumia msimu uliopita ili wasishuke daraja au kuutumia kwa sasa kwenye mechi zao ili wajihakikishie kupanda daraja mapema kabla hata ligi haijaisha?

TFF inalea uozo na kama kweli Kagera watahama uwanja kwa sababu hiyo na kusababisha kuanza kupangua ratiba (naamini kuna mechi ambazo ziko siku moja kwa Kagera na Stand wote wakiwa wenyeji) ili tu Kagera na Stand ziwafae tutakuwa hatuna uongozi wa shirikisho. Kila siku tumekuwa tukisikia timu fulani imepigwa faini kwa sababu ilionyesha vitendo vinavyoashiria ushirikina je kwa timu kuhama uwanja kwa sababu ya ushirikina na TFF na bodi ya ligi kuruhusu basi inabidi nao wote watatu wapigwe faini kwa kujihusisha au kubariki vitendo vya kishirikina. Na siku ikitokea timu nyingine imekataa kwenda kucheza uwanja fulani kwa sababu imeshaona kuna dalili za kufanyiwa ushirikina basi TFF na bodi ya ligi waone ni jambo la kawaida na ikiwezekana hito mechi iahirishwe na kupangiwa siku nyingine na uwanja mwingine.

kweli kabisa na haya mambo watu hufanya makusudi wakijua tff haiwez kuwakemea.. Tff ikiwaruhusu kucheza shinyanga nitaamini bw Malinzi anaamini ktk ushirikina
 
Kagera sidhani wataadhibiwa. Watu wanachunga alliances za uchaguzi. Sitegemei lolote la maana kutoka uongozi wa TFF unaongozwa na uoga,upendeleo na kutowajibika.
 
Hata kama kweli Toto Africa ni wachawi bado hainingii uwanjani kwa nini wawaroge Kagera Sugar? Wao Toto wanafaidika na nini endapo Kagera wakifungwa na hata kama watashuka daraja? Kwa nini kama uchawi huo wanao walishindwa kuutumia msimu uliopita ili wasishuke daraja au kuutumia kwa sasa kwenye mechi zao ili wajihakikishie kupanda daraja mapema kabla hata ligi haijaisha?

TFF inalea uozo na kama kweli Kagera watahama uwanja kwa sababu hiyo na kusababisha kuanza kupangua ratiba (naamini kuna mechi ambazo ziko siku moja kwa Kagera na Stand wote wakiwa wenyeji) ili tu Kagera na Stand ziwafae tutakuwa hatuna uongozi wa shirikisho. Kila siku tumekuwa tukisikia timu fulani imepigwa faini kwa sababu ilionyesha vitendo vinavyoashiria ushirikina je kwa timu kuhama uwanja kwa sababu ya ushirikina na TFF na bodi ya ligi kuruhusu basi inabidi nao wote watatu wapigwe faini kwa kujihusisha au kubariki vitendo vya kishirikina. Na siku ikitokea timu nyingine imekataa kwenda kucheza uwanja fulani kwa sababu imeshaona kuna dalili za kufanyiwa ushirikina basi TFF na bodi ya ligi waone ni jambo la kawaida na ikiwezekana hito mechi iahirishwe na kupangiwa siku nyingine na uwanja mwingine.

Mkuu kwa wiki hii umebobea. Keep it up!
 
Yan wakae hostel za wanafunzi wa SAUT na kula chakula cha mama ntilie wanategea wacheze vizur!! Yan chips na juice ya elfu 3 ushinde kwel?? HAPANA...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom