Ntemi Kazwile
JF-Expert Member
- May 14, 2010
- 2,182
- 307
Kitendo cha Kanali Gadafi kuwashambulia raia wake kwa mizinga na ndege za kijeshi ni kitendo cha aibu na kinatakiwa kipingwe na wapenda demokrasia wote.
Baada ya kuona wenzake wa Tunisia na Misiri wakiondolewa madarakani kwa nguvu za wananchi Gadafi aliamua kutumia nguvu zote za kijeshi alizonazo kuwalazimisha wananchi wake wasipate haki yao ya kikatiba ya kuchagua kiongozi wanayemtaka.
Kitendo hiki kingeruhusiwa kuendelea kingejenga precedence ya watawala wa kiafrika kutumia nguvu ya majeshi kuendelea kukaa madarakani, tumeshuhudia jinsi chaguzi nyingi Afrika zinavyovurugwa na majeshi kwa lengo la kuwalinda wanasiasa waliowapatia nafasi na wanaowarushia marupurupu yatokanayo na ukwapuaji wa rasilimali za nchi zao.
Kwa kuzuia mashambuliza ya anga na matumizi mengine ya ziada dhidi ya raia wa Libya napenda kuwapongeza viongozi wa USA, UK, Ufaransa na wengine wote wanaounga mkono nguvu za kijeshi kumzuia Gadafi kuwashambulia raia wake. Hii itasaidia sana ukuaji wa demokrasia Afrika kwani viongozi wengine ambao hawapendi kuona wakipingwa na wananchi wao kuogopa kushambuliwa pindi watakapotumia nguvu za kijeshi kuzuia wananchi hawa kutumia haki yao ya kidemokrasia kuwapinga (kuandamana).