Auction MArts wapigwa STOP kufunga na kukamata magari

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,840
Kampuni zote zinazojishughulisha na ukamataji na ufungaji magari yaliyoegeshwa kiholela zimepigwa marufuku kutokana na malalamiko mbali mbali ya wananchi yakiwemo ya kuharibiwa magari,rushwa pamoja na kampuni hizo kufanya kazi kinyume cha sheria.source ITV
 
Hili ni vema wakalisomamia siyo wametamka tu then hakuna utekelezaji. Kuna siku moja nilikuwa mitaa ya soko kuu Arusha, kuna bwana mmoja alipaki gari akawa amegusa mstari kidogo, jamaa wakaja wakalifunga minyororo. Yule bwn anarudi anakuta gari yake imepigwa mnyororo, basi aligungua mlango wa gari akatoa shoka na kukatakata minyororo na ile triangle akavipakia kwenye gari kaondoka. Lkn wale vijana walionyesha dalili la kumsogelea jamaa ili awape rushwa lkn jamaa alikuwa na sura ya mbuzi wakamuogopa.
 
Mwaka wa uchaguzi za serikali za mitaa chama cha matapeli watakataza kila siku watu wameumizwa miaka mine sasa wamelia na kusaga meno walikuwa wapi

Hata bange itaruhusiwa mwaka huu
 
Walikuwa wanasababisha usumbufu mkubwa hasa kwa wageni maana maeneo mengi hayana alama za kuzuia kupaki.
 
Kwa hiyo mjingamjinga yeyote akikupiga cheni unamtolea mashine tu, au siyo?!! safi sana.
 
Wakazi wa DAR kwa muda mrefu wamekua wakilalamikia Auctions mart ambao walikua wanafunga magari hovyo hovyo, na likifungwa tu ni rushwa 50,000 au gari inaenda yard unalipa 150,000.

Leo, nimesikia mkuu wa mkoa wa Dar amepiga marufuku hawa jamaa kufunga magari.

Ingawa umekuja umechelewa lakini huu ni moja kati ya uamuzi bora kabisa kuwahi kufanywa na viongozi wetu, i wish wangeenda a step further na kuchunguza nani alikua akifaidika na ile biashara haramu, na ikiwezekana waathirika, wao weza kuonyesha uthibitisho wa malipo, mimi mmoja wapo, warejeshewe pesa zao.


Hawa jamaa walifikia wakati wanafunga gari hata kama dereva yuko ndani ya gari, mimi siku nafungiwa jamaa alikua ananitaza, sijafika hatua tatu mbele naona jamaa wanafunga gari, yaani wananitizama wakati nasimama ili wafunge wapate pesa, walikua ni MWAMKINGA AUCTION MART
 
Kuna siku mimi walikua wanafunga gari iko silence na niko ndani! Wale jamaa na kazi walisimama maana na ma stress ya siku ile nikawa kichaa kidogo!
 
ingefika wakati na sisi tukiona gari lao tunalifunga mnyororo mkubwa lishindwe kutoka na kufunga mnyororo huo na kufuli fungua tunatupa mbali.
wanakera hawa jamaa kama polisi aina ya tigo wanavyowakera watu haswa bdbd vibajaji na hata magari madogo binafsi
 
Kuna siku mimi walikua wanafunga gari iko silence na niko ndani! Wale jamaa na kazi walisimama maana na ma stress ya siku ile nikawa kichaa kidogo!

Kama ningekua weneo la tukio, ningekuja kuongeza nguvu...WANAKERA SANA!
 
Mwaka wa uchaguzi za serikali za mitaa chama cha matapeli watakataza kila siku watu wameumizwa miaka mine sasa wamelia na kusaga meno walikuwa wapi



Chama hicho Mkuu kinajua kucheza na akili za watu jamani kuna mambo mengi hufanywa kwa maslahi yao wenyewe ama kwaajili ya watu wachache tu. Unakumbuka habari ya Noah mara Bungeni Waziri katangaza vingine huku wasimamiaji wa sheria SUMATRA hawana habari lengo likiwa ni kuwahaada wananchi tu
 
Hii biashara inawalipa sana,kutwa nzima watu wazima na tai zao wanazunguka na machuma kuvizia madereva,zile stk zinazopaki pale nmb bank house au pale kwa makufuli mbona hawagusi?
 
Back
Top Bottom