Auawa baada ya kukataa kulipia gongo aliyokunywa

FOE

Member
Sep 21, 2009
87
6
JESHI la polisi linamshikilia mwanamke wa Kitongoji cha Manyata Kijiji cha Nyichoka Kata ya Kyambahi wilayani hapa, kwa tuhuma za kumuua mteja wake kwa kumchoma kisu.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara, Lebaratus Barlow aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa, mtuhumiwa huyo alimchoma kisu Mapinduzi, Thomasi Bisoti (32) na kufa papo hapo.

Alisema tukio hilo lilitokea Septemba 21 mwaka huu, saa 4:00 usiku nyumbani kwa mtuhumiwa huyo, ambako marehemu alikuwa akinywa pombe ya kienyeji aina ya gongo.

Alisema chanzo cha mauaji hayo ni Bisoti, ambaye alifika kilabuni hapo akiambatana na mwanamke mmoja aliyedaiwa kuwa hawara yake, kunywa pombe na kugoma kulipa.

“Kulitokea kutoelewana kati yao, kuhusu malipo ya Sh1,000 hali iliyopelekea mtuhumiwa huyo, ambaye alikuwa akiuuza gongo na aliyekiri kosa kumchoma kisu kifuani upande wa kushoto hadi kwenye moyo na kufa papo hapo,”alisema Kamanda.

Kamanda alieleza kuwa baada ya tukio hilo wanywaji waliokuwepo walimkamata na kumfikisha polisi na anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote kujibu tuhuma zinazomkabili. source: Mwananchi 27/09/2009
 
Back
Top Bottom