Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 50,956
- 22,148
Atumia mtandao wa Facebook kuwalawiti wanafunzi wenzake
Anthony Stancl Tuesday, February 10, 2009 8:21 AM
Mwanafunzi mmoja aliyejifanya msichana anayetafuta mpenzi katika mtandao wa Facebook na kuomba picha za utupu za wanafunzi wenzake na baadae kuwatishia kuzisambaza shule nzima picha hizo wasipokubali awalawiti amekamatwa baada ya kuwalawiti wavulana 7
Taarifa zilizotolewa zilisema kwamba Anthony Stancl mwwenye umri wa miaka 18 alijifanya msichana katika mtandao wa Facebook na kujaribu kutumia kila njia kuwavutia wanafunzi wenzake ili wamtumie picha zao za utupu na baadae kuwatishia wanafunzi hao kuzianika picha zao shule nzima iwapo hawatakubali matakwa yake.
Stancl mkazi wa New Berlin Wisconsinite, nchini Marekani amekamatwa na anashtakiwa kwa makosa ya kujifanya msichana,kubaka, kuwatishia wanafunzi wenzake wa kiume na kumiliki picha za ngono za watoto.
Stancl alianza mchezo wake huo mwaka 2007 baada ya kujisajili kwa jina la kike katika mtandao wa Facebook akijiita Emily na kuweka picha nzuri za kike akijifanya yeye ni msichana aliyekuwa akitafuta mpenzi.
Kwa mujibu wa polisi, baada ya kupata picha hizo za wanafunzi wenzake wavulana Stancl aliwatishia kuzisambaza picha hizo shule nzima na kuwataka wafanye naye mapenzi.
Stancl alifanikiwa kupata picha za utupu za wanafunzi wenzake 31 na alifanikiwa kuwalawiti wavulana saba kati yao.
Inasemekana Stancl alifanya uovu wake huo kwenye mabafu ya shule, sehemu za kuegesha magari na wengine alidiriki kwenda majumbani mwao na kuwafanyia uovu wake huo.
Mtandao wa Facebook umewataka wanachama wake wawe makini na marafiki wanaojiunga nao kwenye mtandao huo na imeahidi kutafuta njia za kuzuia matatizo kama hayo yasitokee tena baadae.