Attitude bila control huchangia umaskini!

payuka

JF-Expert Member
Jun 17, 2010
829
127
Unataka ku- spend zaidi ya kipato. Kisha tu umeshindwa kujizuia na kuzoea kunywa pombe, kwenda club, kuhonga malaya, kula sehemu za kifahari, ku drive gari lenye fuel consumption kubwa, kupanga sehemu expensive, kupiga party za kujionesha kwa marafiki kwamba unazo, kuafanya shopping sehemu usizokuwa na uwezo nazo n.k

Matokeo yake ni nini?
Siku zote earnings zikizidi spending lazima utatafuta jinsi ya kufidia hilo gap. Jinsi ya kufidia gap inaweza kuwa ni katika monetary or non monetary terms ( I.e. Kujiuza cheaply kwa mamen). Kuhusu monetary terms: ndo unasikia mtu kaenda kukopa katika rate ya juu, kauza nyumba, gari, shamba n.k

Nini kifanyike? Badili tabia yako ASAP. Punguza marafiki ambao hawana tofauti na kupe. Tabia si rahisi kuacha kama unavyofikiri, lakini ukidhamiria utaweza.

Cha msingi jua ya kwamba maisha ni safari! Safiri kwa akili na Mungu atakujaalia kufika unapotaka. Ukisafiri kiuwendawazimu consequences zake utazipata mapema na kufupisha safari yako.

Kwa leo ni hilo tu wadau. Kama manapenda niwaandalie somo pana la mambo ya budgeting kwa mazingira yetu ya Tanzania mtanifahamisha. Asanteni.
 
Niseme asante hata kwa hayo machache. Tuandalie mada mkuu tupate ujuzi!
 
Back
Top Bottom