Atheists tulionekana wa ajabu sana!

Wakuu salama, Kwanza kabisa nianze kwa kusema Elimu pekee ndio itakayomkomboa Mwanadamu katika sayari hii, Uwezo wa kutatua changamoto upo ndani yake mwenyewe, Hakuna Msaada wowote utakaotokea anga za juu kuja kusaidia hapa Dunia Hivyo Binadamu ni Mungu tosha kabisa ni Maarifa na yanazidi kupanuka na kukiweka Huru kiumbe Hichi, Miaka kadhaa nyuma Baadhi ya sisi atheists humu tulionekana watu wa ajabu kwa imani Yetu kuwa Hakuna Mungu, Mkuu Kiranga ana thread moja imefikisha almost 3K Comments za Believers wakimshambuliwa kwa matusi nae akiwajibu kwa hoja.

Taswira ya Jf sasa iko tofauti kabisa Watu kiukweli wametoka kwenye vifungo na kwa sasa wengi ni Free thinker ata kama Anaamini katika Mungu ila yuko tayari kusikiliza sera za wasio amini na kuchambua kidogo.

Tuliwahi ongea apa kwamba Mungu huyu tunaemsoma makanisani au Misikitini Hawezi kuwepo hata kwa bahati mbaya mana sifa tunazomjaza hayuko nazo hata punje .NakaribiSha mijadal zaidi.

Cc Free ideas Doyi Kiranga nusuhela @Areta ludovick Kifyatu

"Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu;Wametenda uovu wa ufisadi na kuchukiza,Hakuna atendaye mema."

Mwisho wa kunukuu zaburi 53:1. Na Zaburi 14:1.

Samahani kwa Mimi sina muda mchafu wa kujadili. Kama wewe huamini kwamba kuna Mungu kaa kimya na Imani yako au utueleze imani yako hiyo inafanya nini. Ni kosa kwa mtu yeyote kukashifu imani ya mtu mwingine ILA kumueleza taratibu na sio kusema huyo Mungu wako hayupo!! so what where is your god? NI JAMBO LA FURAHA NA SHANGWE KWETU SISI TULIO NA MUNGU NA KUAMINI MUNGU WETU YUPO, Ni huzuni na hofu kwa ninyi msioamin.

Unajua mimi ninashangaa sana UPUMBAVU WA WATU WENGINE eti wanaamini uwepo shetani na majini lakini hawaamini kwama Mungu yupo? Duuuuuuu!!!
 
vipi siku hizi hamuonekani wa ajabu?
There is only one point which I real don't understand and I will not understand.... ukimkuta mkristo utamuona anatetea Dini yake umuelezi kitu na huyu amemezeshwa kutambua kwamba bible iko sahihi na si quran, ukienda upande wa pili nao utamkuta muislamu umuelezi kitu kuhusu dini yake, na yeye amemezeshwa the same way as christians hamuelezi kitu kuhusu quran na yeye atakuambia wale makafiri wanaenda motoni.... embu jiulize. How did christian choose bible over quran if the quran is the truth and why muslims choose quran instead of bible if bible is the truth.... when I think of this I always come with a conclusion that neither muslims not christians know the truth... but they have inherited what they believe from their parents. The bad thing ni kwamba dini inafundishwa ukiwa na umri mdogo mpaka ukija kuwa matured ni ngumu sana kuhoji ni ngumu sana kuelewa kwamba ulidanganywa.... u will always think ulichoambiwa ni sahihi na kitaendelea kuwa sahihi. U can not prove something happened long time ago just by reading scriptures.... how can u prove illogical arguments??? How can u prove God will use fire to punish us... and why i have to go to hell because i never pray, go to church or mosque, kama siwezi kusibitishiwa kuwepo kwa moto... why should everyone believe the existence of hell or paradise. ( je malengo ya kuishi duniani ni kuwaza imaginary things, kwamba usipoamini imaginary things unakufuru, how???) aje mtu akulazimishe uamini kwamba kuna maisha kwenye galaxies nyingine usipoamini umepotea....
 
Hawa watu ni wa ajabu mno, muislam akimuona mkristo anakula kitimoto anasema Satan at work,
Mkristo akimuona muislam anaoa wake wanne na kutukuza majini, anasema Satan at work,

Mkristo na Muislam wakimwona mtu asiyemwamini huyo Mungu wao, wote kwa pamoja wanasema Satan at work......Sasa kwanini Muumba wa vyote aliumba kitu haribifu kama Shetani?
Alafu kamuumba ana nguvu kuliko binadam mwenyewe.... kila mtu anaonja joto shetani.... akibaka mbuzi eti ni shetani huyo pumbavuu.
 
Alafu kamuumba ana nguvu kuliko binadam mwenyewe.... kila mtu anaonja joto shetani.... akibaka mbuzi eti ni shetani huyo pumbavuu.
Kitu kinachonishangaza eti Mungu alimuumba Lucifer akiwa na uwezo mkubwa sana kiasi cha kujaribu mapinduzi Mbinguni.Badala Mungu amwangamize, yeye alimbadilisha jina kuwa Shetani na kumtupa Duniani ili binadamu dhaifu apigane naye,.....Hivi Mungu anaelewa anayoyafanya kweli?
 
Uthibitisho?
Hivi we jamaa unajielewa kweli?......hata siku moja hujawahi kuweka msimamo wako wazi juu ya Mungu kama yupo au lah!

We unasigina ya wengine kwa kuonesha double standards......Ukiulizwa Mungu yupo au lah!? unaogopa kutoa jibu la kueleweka, kwanini?
 
Kama suala la kutokuwepo mungu si nadharia tu unadhani hadi leo watu wangekuwa wanaendelea kuamini mungu?
Kama Mungu angekuwepo, pasingekuwepo na nadharia juu ya aidha kuwepo au kutokuwepo kwake.

Mbona hatuna nadharia juu ya uwepo au kutokuwepo kwa Mt. Everest?

Watu wanaoendelea kumwamini Mungu, wengi[kama siyo wote] wanafanya hivyo kwa hofu maana walishaambiwa wasipomwamini watapatwa na mabaya na mwisho wata tupwa motoni.

Cha ajabu hakuna aliyewahi kushuhudia hayo matokea ya kutokuamini kama vile Jehanamu.
 
Hivi we jamaa unajielewa kweli?......hata siku moja hujawahi kuweka msimamo wako wazi juu ya Mungu kama yupo au lah!

We unasigina ya wengine kwa kuonesha double standards......Ukiulizwa Mungu yupo au lah!? unaogopa kutoa jibu la kueleweka, kwanini?
Wengi humu mnabishana kimisimamo ila mi nimeomba uthibitisho.
 
Ndivyo mnavyojibaragua na imani zenu, kwanza mnapingana each other.... mmepoteza uhalisia wa mambo husika. Sasa mnaabudu matakwa yenu.
umesha close mind ndugu sioni haja ya kubishana na wewe all you listen is what you want to listen
Free your mind..... good luck
 
Kama Mungu angekuwepo, pasingekuwepo na nadharia juu ya aidha kuwepo au kutokuwepo kwake.

Mbona hatuna nadharia juu ya uwepo au kutokuwepo kwa Mt. Everest?

Watu wanaoendelea kumwamini Mungu, wengi[kama siyo wote] wanafanya hivyo kwa hofu maana walishaambiwa wasipomwamini watapatwa na mabaya na mwisho wata tupwa motoni.

Cha ajabu hakuna aliyewahi kushuhudia hayo matokea ya kutokuamini kama vile Jehanamu.
Mara kwa mara huwa nasema kuwa suala la mungu ni la imani,lakini huwa hamnielewi mnasema imani sio tatizo.

Lakini kama imani isingekuwa tatizo kwenu usingesema et kama mungu angekuwepo(suala la imani) kusingekuwepo nadharia za kuwa hakuna mungu,yani ulitaka suala la imani ya mungu liwe sawa na mtu aseme kuwa anaamini kuwa rais wa Tz ni Magufuli.

Watu kuamini au kutoamini mungu isikuchanganye maana hili ni jambo la imani,kinachotakiwa ni kwani unaamini au kwanini hauamini.
Hivyo wewe kutoamini mungu sikwamba una akili sana.
 
kata tiketi ya ndege, mkiruka mkiwa juu kabisa, halafu itokee hitilaf kidogo.... chungulia dirishani.... hali izidi kuwa mbaya ... ukiwa huna matumaini tena..... utajikuta unatamani kuwa karibu na huyo unaejidanganya hayupo.. utajikuta unatoa matamshi ya sauti na kimoyomoyo ya kumuomba akuokoe.

nnachojaribu kukuambia ni kwamba hata kama utapenda iwe hivyo,binadamu hayuko huru ,amefungwa na matakwa ya Muumba wake. ruka ruka wee na hako kaubongo ulikojikuta tu unako, utarudi tu kwake.
God is Real.
 
Hawa watu ni wa ajabu mno, muislam akimuona mkristo anakula kitimoto anasema Satan at work,
Mkristo akimuona muislam anaoa wake wanne na kutukuza majini, anasema Satan at work,

Mkristo na Muislam wakimwona mtu asiyemwamini huyo Mungu wao, wote kwa pamoja wanasema Satan at work......Sasa kwanini Muumba wa vyote aliumba kitu haribifu kama Shetani?
......MUNGU hakumuumba shetani ili autese ulimwengu bali ni baada ya shetani kuasi ndipo laana ya MUNGU ikashuka juu yake,
Kumbuka uharibifu wa kwanza ulianzia mbinguni na hii ni baada ya Shetani kuasi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom