Athari za Uvutaji wa Sigara kwa afya

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,554
Sigara huzalisha kemikali za uraibu (Nicotine) ambazo husababisha maradhi yanayo husisha mifumo mbalimbali ya mwili wa binadamu iliwemo ile ya damu, moyo na upumuaji. Pia, ni chanzo cha aina mbalimbali za saratani zikiwemo za Kinywa na koromeo, utumbo mkubwa, kongosho na mapafu.

Kwa mujibu wa Shirila la Afya Duniani (WHO) bidhaa hii isiyo na kiwango chochote cha usalama kwa afya husababisha vifo vya zaidi ya watu milioni 8 duniani kila mwaka.

Huzalisha pia kemikali za Hydrogen cyanide, Formaldehyde, Lead, Arsenic, Ammonia, Carbon monoxide na Benzene ambazo ni sumu mwilini.

Athari hizi huwapata pia watu wanaopumua hewa iliyochanganyikana na moshi wa sigara, hivyo ni muhimu kukaa mbali na watu wanaotumia bidhaa hii.

Kwa wanawake wajawazito, huongeza nafasi ya kuharibika kwa ujauzito, kujifungua kabla ya wakati, kujifungua watoto wenye tatizo la mdomo sungura, wenye uzito mdogo na walio na matatizo kwenye mapafu. Aidha, baadhi ya watoto hufariki siku chache baada ya kuzaliwa kutokana na sababu zisizo wazi sana (sudden infant death syndrome-SIDS)

Chanzo: WHO/CDC/American Cancer Society
 
UVUTAJI WA SIGARA NI HATARI KWA AFYA YAKO KWA MAELEZO ZAIDI ENDELEA KUVUTA
 
Nmesoma huku nauangalia ubalozi unavoungua taratiiiibu...
Tutaacha tu. Mpunguze kutusema sasa..😒
 
Ishinde nafsi yako, sigara ni sumu, acha sasa, mkataze na mwengine, sigara ni ulevi, sigara ni hasara, shtuka okoa maisha na waokoe wengine
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom