Athari za kiafya na kisaikolojia mara tu baada ya kujifungua

ZionTZ

JF-Expert Member
Oct 6, 2009
1,283
538
lbwbaby.jpg
Mara baada ya kujifungua mama anaanza ukurasa mpya wa maisha ya malezi. Anaanza wajibu mpya wa kulea, akili yake na mwili wake unakuwa tayari umejijenga kulea mtoto.
Mama ana kazi ya kumuangalia mtoto kwa karibu ikiwapo kumnyonyesha. Hapa pamoja na mama kuwa na uangalizi wa karibu kwa mtoto naye pia anatakiwa aangaliwe kwa karibu, apewe matunzo mazuri na baba wa mtoto au ndugu wa karibu, afarijiwe na aangaliwe afya yake mara kwa mara. Matatizo ya kiafya ni kama vile magonjwa mfano malaria, kifua na maumivu ya mwili, maambukizi ukeni, kidonda kama alizaa kwa upasuaji, maambukizi kwa njia ya mkojo, kutokwa na damu kwa muda mrefu na maumivu ya tumbo, kupata shinikizo la damu na kifafa cha mimba baada ya kujifungua.
Shinikizo la damu mara nyingi huanza taratibu na mama anaweza kuwa kwenye dozi ya matatizo haya ya presha ama asiwe nayo. Presha kuwa juu mara nyingi huanzia mimba ikiwa na umri wa majuma 20 na kuendelea. Kitaalamu kama hakukuwa na tatizo hili tangu awali, tunaita “Pregnancy Induced Hypertension” au “PIH”.
Athari za kisaikolojia baada ya kujifungua hupelekea mama akapata matatizo ya kimwili kipindi hicho cha majuma sita mara tu baada ya kujifungua. Kipindi hiki tunakiita “Puerperium period”. Hapa mama anaweza kuchanganyikiwa “Pueperal pyschosis”, akapata homa kali “Pueperal Pyrexia” na maambukizi ukeni “Pueperal Sepsis”, kwa hiyo kama ilivyo kwa mama anavyomuangalia mtoto, ndivyo anavyotakiwa aangaliwe na atuzwe.
Chakula bora na cha kutosha kwa mama kutamsaidia apate nguvu, atoe maziwa ya kutosha na arudishe afya yake na pia mwili unapata kinga dhidi ya maradhi mbalimbali.

Imeandaliwa na Dkt. Chale






source:Athari za kiafya na kisaikolojia mara tu baada ya kujifungua
 
Back
Top Bottom