ATCL: Mh Kawambwa, iko wapi ripoti ya Kashoro?

Pundamilia07

JF-Expert Member
Oct 29, 2007
1,439
54
Kawaida wananchi tunawakilishwa bungeni na waheshimiwa wabunge, lakini pia namna gani mbunge anatuwakilisha huko bungeni, inabaki kuwa ni kitendawili.

Mh. Dr. Shukuru Kawambwa, ninachukua fursa hii kujiwakilisha mwenyewe:

Swali: Je iko ile ripoti ya Prof. Kashoro juu ya ATCL? Unakumbuka kuwa ulisema utaitisha kikao na waandishi wa habari mara tu tume ya Kasoro itakapomaliza kazi yake? Je, umeshafanya hivyo au ni lini utafanya hivyo?
 
Last edited:
Imekuwa ndio style ya serilkali ya TZ kuwa wako so fast kuunda tume ila uozoo wanaupataa toka kweneye tume hawataki kusema hadharani wakati lengo lilikuwa ni hilo......wajuaa tume zinakula saana pesa....ukute hata hiyo imekula si chini ya 200m....halafu wanaficha au ndio style ya kuwatuliza wananchi wachimba chumvii..mzuka wao???haipendezii hata.....hakuna hata siku moja wakasema kwenye tume labda ya Mwakyembe....tuu..sasa alijiundia yeye ile tume?ina maana gani??no action plan baada ya tume...mmekaa mnalindana ujinga ujinga tu.
 
Ni Prof Mshoro sio prof kashoro.
inasikitisha shirika kubwa la serikali kufilisika.
serikali inabidi ifanye jitihada za kulinusuru kwa kuajiri wataalamu wa ndani au nje ya nchi waache siasa.inasikitisha sana.
 
Aliwaita waaandishi wa habari siku anapokea hiyo ripoti, nadhani ndicho alichokimaanisha kwa sababu ingenishangaza sana kama alimaanisha kuwaita kuwaeleza kilichomo ndani ya ripoti
 
Hiyo report ipo kulekule zinakoendaga ripoti kama hizi - I think zinaelea somewhere in the stratosphere huku zikipishana taratiiiiiibu na zile ripoti 5(5!) za madini, ya dual citizenship, etc, among many other!

OR, it may be collecting dust in some government office somewhere, just like the above mentioned ones! Maybe they should just forget about these tumes before they become bigger jokes!!
 
Kawaida wananchi tunawakilishwa bungeni na waheshimiwa wabunge, lakini pia namna gani mbunge anatuwakilisha huko bungeni, inabaki kuwa ni kitendawili.

Mh. Dr. Shukuru Kawambwa, ninachukua fursa hii kujiwakilisha mwenyewe:

Swali: Je iko ile ripoti ya Prof. Kashoro juu ya ATCL? Unakumbuka kuwa ulisema utaitisha kikao na waandishi wa habari mara tu tume ya Kasoro itakapomaliza kazi yake? Je, umeshafanya hivyo au ni lini utafanya hivyo?

Mheshimiwa Rais alishamwamini na kumteua DG wa ATCL kuwa mjumbe wa bodi ya shirika lingine kabla ya ripoti kutolewa.

Vipi kama ripoti ya Mh. Waziri inakinzana na imani aliyonayo Mh.Rais kwa DG kuongoza mashirika ya umma?

Of course Muungwana alishaiona hiyo ripoti na hata kama kuna chochote kinachomkandamiza rafiki yake, lazima wameshaandaa utetezi
 
IKO AHERA MH PUNDAMILIA 07,ACCORDING TO MA RECORD NI TUME YA ""zOMBE"" TU NDIO ILIOTOA MAJIBU NA KUFANYIWA KAZI.,,,TENA KWA SHINIKIZO LA HAKI ZA BINADAMU................
 
Mkuu Pundam....., mambo ndio yameshatoka hivyo mkuu!! Yaani sijui hata tuendapo ni wapi lakini kwa mapenzi ya Mungu twaweza fika japo kwa kutambaa!!
 
Wafanyakazi wa ATCL wanafanyiwa Medical checkup wapi? Nasikia hata makato ya NSSF yana mashaka? Wadau tupeni data?
 
Ushikaji na uswahiba unaua hii nchi......period!!!!!!!!!JK na kundi lake wote wazushi tu wanaendesha nchi kisanii na kimazoea...na kulindana.
 
Swali: Je iko ile ripoti ya Prof. Kashoro juu ya ATCL? Unakumbuka kuwa ulisema utaitisha kikao na waandishi wa habari mara tu tume ya Kasoro itakapomaliza kazi yake? Je, umeshafanya hivyo au ni lini utafanya hivyo?
 
Wadau kama madesa mengine yalipatikana hapa JF, iweje hio ripoti hadi sasa haijafika hapa JF?wale watu wa nyeti hawapo tena? maana breaking news hazipo siku hizi...?

Kimsingi Kawambwa aambiwe asipoitoa ripoti hio....??????..aache kuwahadaa watz..tumechoka na Longolongo...!!!!
 
Nina wasiwasi mkubwa kuwa hii ripoti imekaliwa kwa makusudi na serikali. Lakini hata hivo Mh. Waziri ameonesha udhaifu mkubwa wa kutotimiza ahadi aliyoitoa. Binafsi mimi ninamuweka katika kundi la watu wasioaminika. Na wasiwasi wangu unazidi kupata nguvu kutokana na low profile aliyonayo huyu Mheshimiwa. Nadhani tusipomfuatilia sasa tutakuja kujuta baada ya kuwa too late huko mbele ya safari. inawezekana sasa hivi anaboronga tu pale wizarani.
Haya, hii thread yangu nitakuja kuitafuta siku ya siku, August 2010 si mbali, na safari hii mambo yote ni kwenye matawi tusilaumiane, tunatwanga na kupepeta wenyewe, safi hiyo!!!
 
hiyo ripoti ni muhimu sana iwekwe wazi ili tujue uozo uko wapi? kuna minong'ono radio mbao, kuwa mkurugenzi mmoja wamemwaga, ila shirika lenyewe ndio liko taabani sana hata huduma za afya kwa wafanyakazi zimesitishwa, baada ya ATCL kushindwa kulipa Medical Insurance kwa kampuni ya Momentum, wafanyakazi wanatakiwa kujaza forms za medical checkup, wanaambiwa wajitegemee ili wapewe refund, ambayo hawarudishiwi, hata makato ya NSSF nayo nasikia ni mgogoro ikiwa Dr. Masau wa THI aliwekwa ndani kwa kutowasilisha makato je Mataka kwanini analindwa ? Wadau tunaomba data ili tusafishe uozo huu
 
Back
Top Bottom