Asante CCM
JF-Expert Member
- Jun 22, 2023
- 346
- 1,301
Ni Askofu Severine Niwemugizi wa Jimbo Katoliki la Rulenge, Ngara ameandika kwenye ukurasa wake wa Facebook
===
Hiyo picha chini inaonyesha janga la uharibifu wa mazingira eneo la Segerea, mto Msimbazi! Miaka 27 iliyopita mto huu haukuwa mpana hivi. Palikuwa na daraja unavuka toka pale seminari kuja Sitakishari. Daraja halikuzidi mita kumi na tano. Nimerudi kuona leo hali nikakuta panatisha. Daraja liliondoshwa na maji na mto umepanuka vya kutisha.
Mmomonyoko umeshika kasi. Lakini ungekuwa huo tu ingekuwa nafuu. Lakini sasa kuna uchimbaji wa kutisha wa mchanga. Nimekuta mashine ziko pale na magari ya kuusomba. Nilipouliza kulikoni nikaambiwa ni kazi ya kusafisha kingo za mto! Na mamlaka za juu kabisa zimeruhusu. Lakini za ndani zaidi zinasema mchanga huo unachimbwa kwenye huo mto na kusafirishwa hadi visiwa vya Karafuu! Hakuna wa kuzuia kazi hiyo, asiyejipenda tu ndiye atajaribu kupiga kelele za kuzuia.
Kumbe mamlaka ya Seminari Kuu ya Segerea yamejitahidi bila mafanikio kuzuia uharibifu huo. Na hata vitisho vimekwisha tolewa kwa Mkuu wa seminari alipojaribu kufuatilia ili uharibifu huo ukomeshwe. Polisi Sitakishari wakataarifiwa juu ya vitisho na sasa ni kimya lakini uharibifu unaendelea!
Hapa kuna utata kidogo. Huu usafishaji wa kingo za mto unafanyika eneo moja tu la Segerea? Viongozi wetu wanazungumza sana juu ya utunzaji wa mazingira, lakini kwa pale sauti hizo zinanyamaa!! Kuna ruhusa rasmi ya kuharibu, kwa nini?
Wanaharakati wa mazingira hapo mmeishapaona? Kama bado nendeni mjionee na mfanye kitu tafadhali.