Askofu Mwamalanga: Tunalijua genge na kiongozi wake linalompangia Rais nini cha kufanya

THE BIG SHOW

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
16,365
12,823
Friends and Enemies,

Hali inazidi kuwa mbaya, katika mkutano wa CHADEMA na maaskofu katika suala lao la kulumbana na serikali juu ya masuala ya bandari maaskofu wamezidi kutema kauli zao ambazo ni tatanishi.

Amesikika kwa uwazi kabisa Askofu Mwamalanga akisema kwamba wao kama maaskofu wanalijua hilo genge,kiongozi wake na kila wanachokifanya katika kumwambia Rais nini afanye na nini asifanye.

Hilo genge linakula bila kulima,bila kupanda na halina kazi yeyote.

Hilo genge ndiyo linampangia Rais fanya hiki,Rais samia unategemea nini kulietegemea genge kama hilo?

My take; Haya ndiyo madhara ya kuchanganya dini na siasa ambayo chadema wanaanza kuyavuna.

Huyu Askofu na wenzake watueleze hili genge ambalo wao wanalijua kuwa lina mpangia Rais kazi ya kufanya ni genge lipi na wao wanalijua kwa utaratibu upi.

Imefikia hatua sasa chadema na maaskofu wanaona ni jambo la kawaida kabisa kushare majukwaa ya kisiasa na kuishambulia serikali tena kwa hoja za kipuuzi kama hizi ambazo ni kama suala baya ya kuligawa taifa.

Rais Samia ni msikivu na mvumilivu sana,lakini hali hii ambayo chadema wanaendelea kuitengeneza watakuja kuvuna matunda yao na wasije wakatafuta wa kumlaumu.
 
Siku zinavyozidi kwenda mbele unazidi kuwa mjinga tu.

Unajizima data hujui kama Kikwete ndio anayeharibu nchi?

Kwa akili zako za kuvukia barabara hujui kama Kikwete ndiye aliyemuibuwa Samia mpaka amefikia Urais?

Ubongo ukiganda udini unakuwa mpumbavu kabisa.
 
Back
Top Bottom