#COVID19 Askofu Gwajima: Rais alisema chanjo ni hiari. Mawaziri Mollel na Dorothy, wanasema 70% wasiotaka kuchanjwa ni wajinga

The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
7,951
12,536
Video imebeba ujumbe wote.

Hapa chini akimjibu Spika na barua yake ya wito kumtaka atokee mbele ya kamati ya maadili, kinga na haki ya Bunge la JMT...

Amesema, atakwenda Dodoma kesho J'3 tarehe 23/8/2021 kama barua inavyosema.

Aidha kasema haogopi chochote, hayumbi ktk misimamo yake bila kujali chochote na daima atasimama katika kweli na sasa atakwenda kusema na mengine ambayo hata hatujawahi kuyasikia.

Aende akatoe ushahidi Muheshimiwa Raisi kahongwa na nani na kiasi gani?

Atoe ushahidi kuwa chanjo ni sumu.

Akatoe ushahidi wa nanomilimita? Iliyomo kwenye chanjo ambayo inasaidia kuwacontrol waliochoma.

Akatoe ushahidi kuwa muheshimiwa raisi aliwadanganya watanzania kwa kuchoma maji badala ya chanjo ya jensen.
 
Kwani aliyasema akiwa bungeni?Au hayo uliyoyaorodhesha yanahusu hadhi ya bunge?
 
Uzuri huwa sipendi kusimuliwa,nafuatilia mwenyewe,nimemsikia mwenyewe Gwajima!

Na Leo ndo nimeona clip ya Moleli naibu waziri akiongea kuwa chanjo haifai kipindi cha hayati Magufuli,aisee sijaamini nilichokiona na kukisikianashukuru Gwajima ali tuwekea tujionee before and after Magufuli!.

Hakika usimwamini mwanasiasa!
 
Uzuri huwa sipendi kusimuliwa,nafuatilia mwenyewe,nimemsikia mwenyewe Gwajima!
Na Leo ndo nimeona clip ya Moleli naibu waziri akiongea kuwa chanjo haifai kipindi cha hayati Magufuli,aisee sijaamini nilichokiona na...
Hata Gwajima mwenyewe aliwahi kusema hawezi kugombea ubunge, maana ana hadhi kubwa kuliko ubunge.

Vipi hiyo video nayo ameiweka?

Heri mwanasiasa muongo kuliko kiongozi wa kiroho mnafiki.
 
Labda asilimia 70 ni ya wale misukule wake, asituchanganye na sisi wenye akili timamu.
 
Back
Top Bottom