BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,020
Wapendwa Watanzania!
Tunapenda kuwahakikishia kuwa Jumuiya ya Kimataifa itafuatilia kwa umakini na ukaribu sana Kampeni yetu kupitia "Matembezi ya Hiyari" kwa nchi nzima ya kuuhamasisha umma kuhusu umuhimu wa kuunda Tume Huru ya Uchaguzi na kuandika Katiba Mpya!
Orodha ya viongozi wanaokiuka haki, demokrasia, haki za binadamu, na kudhurumu haki ya wengine kuishi nchini Tanzania ipo katika nchi za Jumuiya ya Kimataifa. Jana nchi ya Marekani ilitangaza kuweka vikwazo kwa viongozi hao na kuonya kuwa hatua nyingine zitafuata. Tunaamini kuwa nchi nyingine zitaungana na Marekani katika kuwabana zaidi watu hawa!
Ni kwa sababu hiyo, tunatoa wito kwa watu wote wanaoguswa na masuala ya haki katika nchi hii kujiandaa na kujitokeza kwa wingi kushiriki "Matembezi ya Hiyari"! Msitishwe na watu ambao tayari wapo katika hofu kubwa kuliko ninyi! Huu sio wakati wa kuendelea kunung'unika pasipo kuchukua hatua!
Tutatangaza tarehe ya kuanza kwa "Matembezi ya Hiyari" muda wo wote kuanzia sasa mara baada ya kuweka sawa mambo muhimu. Tunatoa wito kwa watu kujitokeza kuchapa T'Shirts na Kofia zilizoandikwa TUME HURU YA UCHAGUZI au KATIBA MPYA na kuanza kuzisambaza nchi nzima! Vyama vya siasa na taasisi nyingine mbalimbali wawe huru kukutana, kuweka mikakati na kuhamasisha wafuasi wao kwa nguvu zote!
Tunapenda kuwati moyo na kuwakikishia kuwa tunao ujasiri mkubwa zaidi kuliko ilivyokuwa hapo awali! Mungu ametutia ujasiri sisi tulio wadhaifu ili kwa pamoja kwa umoja wetu tuikomboe na kuikwamua nchi kutoka katika mkwamo mkubwa wa kisiasa ambao haujawahi kushuhudiwa tangu kuzaliwa kwa taifa letu! Tuchukue hatua! Tusisubiri mashujaa ambao hawajazaliwa! Tukiunganisha nguvu kwa umoja wetu tuna nguvu zaidi na kishindo kikuu kuliko mashujaa wachache watakaozaliwa baadaye!
Tukizindua Dar es Salaam tutakwenda mikoani na wilayani. Tutakuwa na muda wa kutosha kufika kila kona ya nchi! Wanaotuzomea leo, kesho watafurahia kwa kutoa machozi ya furaha baada ya mapambano yetu kuleta ushindi wenye heshima! Wanaotutukana leo, kesho wataungana nasi kushangilia mwisho mwema! Wanaotuonea kinyaa leo, kesho watapenda kutukaribisha katika nyumba zao!
Ninasisitiza kuwa nitavaa majoho ya Kiaskofu wakati wote nitakaoongoza "Matembezi ya Hiyari"! Sambaza ujumbe huu ili uwafikie watu wengi zaidi!
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula