Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula: Wapendwa Watanzania

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,020
Wapendwa Watanzania!

Tunapenda kuwahakikishia kuwa Jumuiya ya Kimataifa itafuatilia kwa umakini na ukaribu sana Kampeni yetu kupitia "Matembezi ya Hiyari" kwa nchi nzima ya kuuhamasisha umma kuhusu umuhimu wa kuunda Tume Huru ya Uchaguzi na kuandika Katiba Mpya!

Orodha ya viongozi wanaokiuka haki, demokrasia, haki za binadamu, na kudhurumu haki ya wengine kuishi nchini Tanzania ipo katika nchi za Jumuiya ya Kimataifa. Jana nchi ya Marekani ilitangaza kuweka vikwazo kwa viongozi hao na kuonya kuwa hatua nyingine zitafuata. Tunaamini kuwa nchi nyingine zitaungana na Marekani katika kuwabana zaidi watu hawa!

Ni kwa sababu hiyo, tunatoa wito kwa watu wote wanaoguswa na masuala ya haki katika nchi hii kujiandaa na kujitokeza kwa wingi kushiriki "Matembezi ya Hiyari"! Msitishwe na watu ambao tayari wapo katika hofu kubwa kuliko ninyi! Huu sio wakati wa kuendelea kunung'unika pasipo kuchukua hatua!

Tutatangaza tarehe ya kuanza kwa "Matembezi ya Hiyari" muda wo wote kuanzia sasa mara baada ya kuweka sawa mambo muhimu. Tunatoa wito kwa watu kujitokeza kuchapa T'Shirts na Kofia zilizoandikwa TUME HURU YA UCHAGUZI au KATIBA MPYA na kuanza kuzisambaza nchi nzima! Vyama vya siasa na taasisi nyingine mbalimbali wawe huru kukutana, kuweka mikakati na kuhamasisha wafuasi wao kwa nguvu zote!

Tunapenda kuwati moyo na kuwakikishia kuwa tunao ujasiri mkubwa zaidi kuliko ilivyokuwa hapo awali! Mungu ametutia ujasiri sisi tulio wadhaifu ili kwa pamoja kwa umoja wetu tuikomboe na kuikwamua nchi kutoka katika mkwamo mkubwa wa kisiasa ambao haujawahi kushuhudiwa tangu kuzaliwa kwa taifa letu! Tuchukue hatua! Tusisubiri mashujaa ambao hawajazaliwa! Tukiunganisha nguvu kwa umoja wetu tuna nguvu zaidi na kishindo kikuu kuliko mashujaa wachache watakaozaliwa baadaye!

Tukizindua Dar es Salaam tutakwenda mikoani na wilayani. Tutakuwa na muda wa kutosha kufika kila kona ya nchi! Wanaotuzomea leo, kesho watafurahia kwa kutoa machozi ya furaha baada ya mapambano yetu kuleta ushindi wenye heshima! Wanaotutukana leo, kesho wataungana nasi kushangilia mwisho mwema! Wanaotuonea kinyaa leo, kesho watapenda kutukaribisha katika nyumba zao!

Ninasisitiza kuwa nitavaa majoho ya Kiaskofu wakati wote nitakaoongoza "Matembezi ya Hiyari"! Sambaza ujumbe huu ili uwafikie watu wengi zaidi!

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
 
Sio wakati muafaka wa kufanya matembezi hayo ingawa ni kweli lengo ni zuri! Acha Taifa lisonge mbele "kimaendeleo ya vitu" na kisha maendeleo ya watu yatafuata!
 
Kwenye katiba hakuna kipengele kinachosema kwamba kuna wakati muafaka wa Watanzania kudai haki zao mbali mbali. Taifa haliwezi kusonga mbele ikiwa Watanzania tunanyimwa haki yetu ya kikatiba kuchagua viongozi tuwatakao kwa hila mbali mbali ikiwemo wizi wa kura, kura fake, vitisho na hata mauaji.

Maelezo yangu yameegemea zaidi katika ukweli kuwa, jamii yetu haijajengwa katika ujasiri wa kusimamia na kudai haki zake kwa njia inayopendekezwa ya matembezi! Chukulia mfano wa Wabunge wa viti maalum waliofikuzwa uanachama wa CHADEMA lakini Katiba imevunjwa na leo wanaongoza Kamati nzito nzito kule Bungeni! Huoni hapa kuna tatizo zaidi ya vile Askofu anavyojiaminisha!

Tuanze kutatua tatizo la Watanzania kukosa ujasiri wa kuisimamia Katiba iliyopo na kisha tudai hiyo inayoitwa Katiba Mpya!!
 
Kukosa ujasiri si sababu ya kukaa kimya ili kuwapa Watanzania ujasiri wa kudai haki zao za kikatiba hasa ukitilia maanani matukio ya wakati wa kampeni za uchaguzi, siku ya uchaguzi na baada ya uchaguzi.

Hao COVID19 hawana vyama hivyo ni katika mtiririko ule ule wa kuvunja/kudharau katiba kwa kuwaingiza bungeni watu ambao si wanachama wa chama chochote kile Nchini.
Maelezo yangu yameegemea zaidi katika ukweli kuwa, jamii yetu haijajengwa katika ujasiri wa kusimamia na kudai haki zake kwa njia inayopendekezwa ya matembezi! Chukulia mfano wa Wabunge wa viti maalum waliofikuzwa uanachama wa CDM lkn Katiba imevunjwa na leo wanaongoza Kamati nzito nzito kule Bungeni! Huoni hapa kuna tatizo zaidi ya vile Askofu anavyojiaminisha!
Tuanze kutatua tatizo la Watz kukosa ujasiri wa kuisimamia Katiba iliyopo na kisha tudai hiyo inayoitwa Katiba Mpya!!
 
Sawa mchungaji bandekule aka bak
Wapendwa Watanzania!

Tunapenda kuwahakikishia kuwa Jumuiya ya Kimataifa itafuatilia kwa umakini na ukaribu sana Kampeni yetu kupitia "Matembezi ya Hiyari" kwa nchi nzima ya kuuhamasisha umma kuhusu umuhimu wa kuunda Tume Huru ya Uchaguzi na kuandika Katiba Mpya!

Orodha ya viongozi wanaokiuka haki, demokrasia, haki za binadamu, na kudhurumu haki ya wengine kuishi nchini Tanzania ipo katika nchi za Jumuiya ya Kimataifa. Jana nchi ya Marekani ilitangaza kuweka vikwazo kwa viongozi hao na kuonya kuwa hatua nyingine zitafuata. Tunaamini kuwa nchi nyingine zitaungana na Marekani katika kuwabana zaidi watu hawa!

Ni kwa sababu hiyo, tunatoa wito kwa watu wote wanaoguswa na masuala ya haki katika nchi hii kujiandaa na kujitokeza kwa wingi kushiriki "Matembezi ya Hiyari"! Msitishwe na watu ambao tayari wapo katika hofu kubwa kuliko ninyi! Huu sio wakati wa kuendelea kunung'unika pasipo kuchukua hatua!

Tutatangaza tarehe ya kuanza kwa "Matembezi ya Hiyari" muda wo wote kuanzia sasa mara baada ya kuweka sawa mambo muhimu. Tunatoa wito kwa watu kujitokeza kuchapa T'Shirts na Kofia zilizoandikwa TUME HURU YA UCHAGUZI au KATIBA MPYA na kuanza kuzisambaza nchi nzima! Vyama vya siasa na taasisi nyingine mbalimbali wawe huru kukutana, kuweka mikakati na kuhamasisha wafuasi wao kwa nguvu zote!

Tunapenda kuwati moyo na kuwakikishia kuwa tunao ujasiri mkubwa zaidi kuliko ilivyokuwa hapo awali! Mungu ametutia ujasiri sisi tulio wadhaifu ili kwa pamoja kwa umoja wetu tuikomboe na kuikwamua nchi kutoka katika mkwamo mkubwa wa kisiasa ambao haujawahi kushuhudiwa tangu kuzaliwa kwa taifa letu! Tuchukue hatua! Tusisubiri mashujaa ambao hawajazaliwa! Tukiunganisha nguvu kwa umoja wetu tuna nguvu zaidi na kishindo kikuu kuliko mashujaa wachache watakaozaliwa baadaye!

Tukizindua Dar es Salaam tutakwenda mikoani na wilayani. Tutakuwa na muda wa kutosha kufika kila kona ya nchi! Wanaotuzomea leo, kesho watafurahia kwa kutoa machozi ya furaha baada ya mapambano yetu kuleta ushindi wenye heshima! Wanaotutukana leo, kesho wataungana nasi kushangilia mwisho mwema! Wanaotuonea kinyaa leo, kesho watapenda kutukaribisha katika nyumba zao!

Ninasisitiza kuwa nitavaa majoho ya Kiaskofu wakati wote nitakaoongoza "Matembezi ya Hiyari"! Sambaza ujumbe huu ili uwafikie watu wengi zaidi!

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
 
Utatamdikwa na majoho yako,tena vizuri sana maana kwenye hili serikali itayatumia maandiko yako ya toka awali likiwemo hili pia.
ili kuuthibitishia ULIMWENGU kwamba wewe ni kikaragosi wa kisiasa na huna cha UASKOFU wala nini.

Tunasubiri hiyo siku kwa hamu sana.
Kumbuka kuna ma shekhe wa uamsho wanaozea mdani shauri ya kutaka kutuvurugia amani ya nchi hii.sembuse wewe?

Kama vile wewe unavyofanya sasa. Kunyamaziwa kwako sio kuogopwa bali unasubiriwa uingie kingi nzuri KISHERIA ili ukiminywa uminywe KISHERIA.

ENDELEA.

Sisi wapenda AMANI yetu macho
View attachment 1684132
 
Back
Top Bottom