Askofu amkaanga Makinda

Naye askofu wa kanisa moja kubwa nchini ambaye aliomba kuhifadhiwa jina ili kuepusha malumbano, alisema kuwa Spika Makinda na Naibu wake, Job Ndugai, wanayumba na wanaliyumbisha Bunge.

Akizungumza na gazeti hili kwa simu, askofu huyo alisema kuwa viongozi hao wawili wametumwa na wanatumika. Na kwamba wale waliowatuma wanaona kuwa wanafanya vizuri kwani ndilo hasa lengo.

Alisema ni juhudi za wabunge pekee, tena wenye maono ya kizalendo, ndizo zinaweza kuwaondoa madarakani kwani ni vibaraka.
“Ukimlinganisha huyu Spika na wenzake waliowahi kuongoza Bunge, huyu ni balaa. Amevaa itikadi zaidi Lakini tunatafsiri kuwa anatumika na Rais.

“Huwezi kuwa na Bunge imara kama una serikali dhaifu. Ndiyo maana katika nchi yetu sasa, mtu hawezi kuwa Spika kama Rais hajamkubali,” alisema.

Alisema hayo tunaweza kujifunza kutokana na kauli ya Makinda ya hivi karibuni alipotoa maoni yake kwenye tume ya kukusanya maoni ya Katiba, pale aliposema kwamba anapendekeza Spika asitokane na chama cha siasa.

Hiyo ina maana anashinikizwa na chama chake kufanya mengi ambayo kama si shinikizo, asingeyafanya. Hata haya yanayotokea ni shinikizo la chama chake.

“Hali ni hiyohiyo hata katika mahakama. Serikali inaingilia sana uhuru wa mahakama. Ndiyo maana hata Jaji Mkuu alipotoa maoni yake katika Tume ya Marekebisho ya Katiba alisema angependa mahakama iwe huru.

“Maana yake anajua kuwa kwa sasa kuna shinikizo kutoka serikalini au chamani katika uendeshaji wa maamuzi ya mahakama nchini. Hii ni hatari,” alisema.

Askofu alibainisha kuwa Makinda ni tofauti na Spika aliyepita Samuel Sitta; kwamba Sitta alikuwa na mwelekeo, alisimamia ukweli, japo mwelekeo wake haukupendwa na watawala.

Aliongeza kuwa Sitta alikuwa mpigania haki, mpenda mabadiliko na aliweza kuonyesha kuwa anawajali wanyonge. Hakuliyumbisha Bunge na aliweza kusimamia maamuzi.

“Bunge haliongozwi kitaasisi, bali linaongozwa kwa matashi ya mtu binafsi au kikundi cha watu.

“Sisi tunapaswa kuwa makini katika kuchagua watu wa aina hii na tunapaswa kuwaelimisha Watanzania ili wapambane kuondoa mfumo wa aina hii,” alisema.

source: Tanzania daima[/QUOTE


HII NDO TANZANIA....Kama inafika mahali mpaka viongozi wa kidini kama maaskofu wanahofu kutaja majina yao hadharani hali ni mbaya.Mungu pekee tu ndiye atakayelinusuru Taifa hili.
 
Bishop Anonymous anamwogopa LOWASSA na michango yake ya mamilioni.....na ujenzi wa "kanisa" umesimama

church.jpg
 
Huyu askofu kwanini anaogopa kutaja jina lake?hawa ndo wanachelewesha ukombozi kwa kujifichaficha.
 
Kanisa kubwa lipi hizi habari zimetoka kwenye gazeti la udaku Tanzania Daima. Wanataka kuwachonganisha Askofu na Makinda.

Askofu kasema ukweli wake.

Nasangaa watu wanalaumu oh sijui hakutaja jina,sijui wa kanisa gani mara anataka kuchonganishwa na Makinda............!
Mwe, hivi watu wazima na akili zenu hamuoni jinsi Anne Makinda na Job Ndugai wanavyochemsha Bungeni?????

Hebu kama tuna akili timamu tuache hii biashara ya unafiki.
 
Askofu kasema ukweli wake.

Nasangaa watu wanalaumu oh sijui hakutaja jina,sijui wa kanisa gani mara anataka kuchonganishwa na Makinda............!
Mwe, hivi watu wazima na akili zenu hamuoni jinsi Anne Makinda na Job Ndugai wanavyochemsha Bungeni?????

Hebu kama tuna akili timamu tuache hii biashara ya unafiki.

Askofu gani huyo tupe jina lake.
 
Back
Top Bottom