Askari wa Kituoni Ubungo Simu 2000 kilichowatokea leo kiwe ni Fundisho Kwenu na muache kuonea Madereva mtakuja Kufa Kipuuzi

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,646
109,034
GENTAMYCINE nilikuwa naambiwa hakuna Madereva Waliodata na Wasioogopa lolote, Wathubutu na Majasiri kama wa Masafa Marefu ( Malori ) ila kwa nilichokishuhudia Mubashara leo Ubungo SIMU 2000 nimekubali na Kuwanyooshea mikono.

Ilikuwa ni mida ya Saa 7 Mchana ambapo Askari wa Ubungo SIMU 2000 walimkamata Dereva Mmoja wa Lori kwa Kosa la Kipumbavu la kwanini kasimamisha Lori lake pembeni ili ashushe Mzigo na hajaenda kupaki Kwingineko.

Hivyo Askari Wawili wakapanda ndani ya Lori husika huku Mwanamume ( Dereva ) akiwa Kifua wazi Keshajichokea zake baada ya Kuingia leo kutokea Congo DR.

Wakaja nae hadi Ndani Kituoni Ubungo SIMU 2000 ili wamwandikie Faini ya Kosa lake na kwa Upumbavu ( Upopoma ) wa wale Askari Wawili baada ya Mmoja kushuka na mwjngine abakie Kumdhibiti Dereva yote Miwili ikashusha huku ikiwa na Mikogo mingi ya hapa na pale.

Kudadadeki Kitendo cha Wao Kushuka Kipopoma ( Kipumbavu ) vile Mwanamume ( Dereva wa Lori ) alilitoa Lori kwa Spidi ya hali ya Juu na Kuwakimbia wale Askari ambapo GENTAMYCINE niliona akikata Kona Kiufundi na Kiuweledi za mule ndani Kituoni Ubungo SIMU 2000 na kutoka hadi nje na kutokomea kwa Spidi ile ile ya Kutukuka.

Wakati Dereva huyo wa Lori akiwakimbia Askari wale Kibabe niliona Askari Mgambo akiwa ametumwa na Kiherehere chake kumuwahi / kuliwahj kwa mbele Lori husika kwa kulipiga mkono ili lisimame ambapo Dereva wa Lori akampelekea ( mazima mazima ) Lori lake Yule Askari Mgambo Kiherehere ambapo nilimshuhudia akisema....Oya Unaniua Nisamehe nina Familia inanitegemea....kisha akajirusha katika Beseni Kubwa lililokuwa na Chips pembezoni mwa Barabara ndiyo ikawa pona yake ya Kutokufa ila upande wa Kuzivamia Chips za Watu ukiwa unamsubiria azilipe au nae akubali Kuunganishwa na zile Chips ili akaangwe na aliwe kisha Wamalizane kwa Uharibifu wake wa Sifa, Kiherehere na Kujitakia.

Baada ya Tukio hili kama kawaida yangu GENTAMYCINE sikutaka niishie pale na nikaanza Kuhoji baadhi ya Madereva wa DalaDala wa Ubungo SIMU 2000 kuwa Kulikoni ile hali cha Kushangaza Wengi wao Walifurahja na Kumsifia Dereva wa Lori lile kwa alichowafanyia wale Askari waliomkamata wakidai kuwa Askari wa Ubungo SIMU 2000 wanapenda mno Kuonea Madereva, Kulazimisha na Kubambikia Makosa na Kuomba Rushwa ( Hongo ) kubwa kubwa kutoka Kwao.

Nilitamani mno Kumjua yule Dereva wa Lori kwani kwa Ujasiri, Uthubutu, Uzoefu na Umahiri wa Uendeshaji Gari ( Lori ) ningempendekeza achukuliwe ama na Umedani ( ZTWJ ) au Idarani ( SSIT ) na aweze kutumika Kiutendaji zaidi huko kwani alinifurahisha na Kuniaminisha rasmi kuwa Madereva wa Masafa Marefu ( Lori za kwenda Mataifa ya Mbali ) siyo wa Kuwachukulia Poa na kwamba Ukijipendekeza na kuingia katika 18 zao wanaweza hata Kukuua njiani na ukaiacha Familia yako na Majonzi pamoja na Umasikini wa Kudumu.
 
Ni watu kubadilika tu, amefanya kosa mwandikie faini na namba ya malipo basi inatosha; haya mambo yakusimamishana na kuanza kufanya majadiliano au kuweka mazingira ya takrima hayana tija.
Uhai muhimu zaidi, hela tunaziacha; tusiwe watumwa wa hela.​
 
Screenshot_20231001_002722.jpg
 
Ni watu kubadilika tu, amefanya kosa mwandikie faini na namba ya malipo basi inatosha; haya mambo yakusimamishana na kuanza kufanya majadiliano au kuweka mazingira ya takrima hayana tija.
Uhai muhimu zaidi, hela tunaziacha; tusiwe watumwa wa hela.​
Cc Askari Wapuuzi Kituoni Ubungo SIMU 2000.
 
Back
Top Bottom