Askari polisi wa usalama barabarani ampiga raia na spana kichwani

Lucchese DeCavalcante

JF-Expert Member
Jan 10, 2009
5,471
734
Askari polisi wa usalama barabarani huko Mbeya leo asubuhi amempiga na kumjeruhi raia kwa spana baada ya mabishano ambapo askari alimsimamaisha jamaa na kudai leseni. Jamaa alidai hana leseni na akamuomba askari amuandikie kosa halafu ataenda kuripoti kituoni baada ya kufuata leseni aliyoicha nyumbani. Swali hivi ni sawa kweli kwa polisi kumthibiti raia kwa kupika na kumjeruhi vibaya kichwani? Afande Mwema na Afande Adv. Nyombi mpo?
 
Tukio lenyewe katika picha....

attachment.php
attachment.php
attachment.php
 
Attachments

  • slide0372_image005.jpg
    slide0372_image005.jpg
    74 KB · Views: 232
  • slide0381_image011.gif
    slide0381_image011.gif
    33.7 KB · Views: 213
  • slide0383_image015.gif
    slide0383_image015.gif
    20.9 KB · Views: 210
duu haw jamaa mbona hawafuati sheria si wangempeleka kituoni?
 
Hili ni tatizo Kubwa ambapo Polisi wamekuwa hawazingatii sheria Kabisa!! Unakuta polisi anakupa Notification paper kama risiti ya Faini uliyolipa!! Huu ni wizi wa Mchana kweupe ndani ya Vyombo vya dola!! Polisi, Sijajua kama Mpinga ndio Kawaagiza Hivyo ili kuchanga Posho za Kujikimu!! Hata Vifaa sensitive kama Tochi unakuta askari anakwenda navyo nyumbani kwani unakuta amefanyia makusanyo hadi Giza Linamkuta na pia kulazimika kufanya makusanyo siku inayofuata mapema Kabisa, au Jumapili!! Duh jamani tunakwenda wapi? Huyu Mwema ameshindwa kabisa kuwasimamia askari wake wamefanya kama biashara ya Sandakalawe!!
 
Unajua hawa police wa Tanzania wanajiona wao kama wapo juu ya sheria, yaani wamejaa kiburi kweli kweli.... sasa embu cheki hizo picha hapo raia ni salama kweli kuendana na maadili ya kazi yao..
 
si lazima uwe na leseni yako kwenye gari...sheria inasema kama umeisahau nyumbani or anywhere unatakiwa kuiwakilisha kituon ndani ya masaa 48 ama kitu kama hicho. sasa haya mambo ya kujeruhi yanatoka wapi....hi ni kutokana na askari vilaza.
 
Polisi jamii

Huyu jamaa angefuata sheria

Polisi wamefanya kitu kizuri

wewe unaijua sheria inasemaje? Road trafic act inasema hivi for your information:

"77-(I) Every person driving a motor vehicle..... shall carry his driving licence....on being so required by police officer, produce it for examination.
......a person shall not be convicted on an offence under this section by reason only of failure to carry, or produce his driving licence, if he produce it to the police within the following threee days at such police station within tanganyika as may be specified by the police office at the time its production is required"

Huwa natembea na hii act kwenye gari yangu and no one has ever niletea shida. Infact nikikaa nao mpaka wanafurahi wenyewe. sito hata senti moja. Wengine wako vizuri ila wengine ni vilaza tu.

So JeyKey usiongee ongee tu ovyo.
 
asante, nashangaa anaeuliza source, kumbe kina tomaso bado wapo.
Kuna watu wako tayari kuitetea serikali ya CCM hata kwenye makosa ya wazi kbisa hivyo inapotokea issue kama hizi huko sa la kusema sana sana atakimbilia kuuliza source...
 
Nanyi madereva mzidi,yaani hamna heshima ktk kazi zenu.Acha mpasuliwe vichwa mpate akiri.Leseni ndo karamu yako kwanini usitembee nayo japo copy?
 
wewe unaijua sheria inasemaje? Road trafic act inasema hivi for your information:

"77-(I) Every person driving a motor vehicle..... shall carry his driving licence....on being so required by police officer, produce it for examination.
......a person shall not be convicted on an offence under this section by reason only of failure to carry, or produce his driving licence, if he produce it to the police within the following threee days at such police station within tanganyika as may be specified by the police office at the time its production is required"

Huwa natembea na hii act kwenye gari yangu and no one has ever niletea shida. Infact nikikaa nao mpaka wanafurahi wenyewe. sito hata senti moja. Wengine wako vizuri ila wengine ni vilaza tu.

So JeyKey usiongee ongee tu ovyo.

Road Traffic Act No.30 of 1973
Wadau zijueni sheria za barabarani pamoja na haki zenu. Naomba kuwasilisha. Shukrani za dhati ziuendee Umma wa Wapanda Baiskeli Dar es Salaam(UWABA) kwa nakala ya hii.

http://www.uwaba.or.tz/30-1973.pdf
 
Tatizo ni lile lile la Polisi kutozijua sheria za nchi yenu na raia ni mbumbu wa sheria. sasa kipofu anamuongoza kipofu mwenzie.

Dereva ana haki kabisa ya kufungua kesi. msingi apate karatasi ya Polisi ili akachekiwe hospital na kupata taarifa ya daktari kisha kufungua kesi dhidi ya polisi.

Siku zote napenda kuwauliza wa TZ ni asilimia ngapi ya Traffic wenu wanajuwa kuendesha magari? Itawezekana vipi mtu asiyejua kuendesha gari akaongoza wanaojua kuendesha gari? Ni sawa na Padre ambaye hajaoa akaitwa kusuruisha kesi za wanandoa.
 
Back
Top Bottom