Askari polisi ashikiliwa kwa wizi wa mitambo ya IPTL

Kulwa Jilala

JF-Expert Member
Sep 6, 2022
3,510
7,755
Dares Salaam. Baadhi ya mitambo ya kampuni binafsi ya kufua umeme (IPTL) inadaiwa kuibiwa na watu wanne akiwemo askari Polisi aliyekuwepo lindo siku ya tukio.

Mitambo hiyo iliyopo Tegeta jijini Dar es Salaam, ilisitishwa kutoa huduma ya kuzalisha umeme kwa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) mwaka 2013 baada ya kutoelewana kwa wahusika wa mkataba wa makubaliano.

Kulingana na taarifa zilizosambaa katika mitandao ya kijamii, watuhumiwa wa tukio hilo wanashikiliwa na Polisi katika Kituo cha Oysterbay jijini hapa.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amethibitisha tukio hilo.

“Tumezipata taarifa hizo na tunazichunguza katika uchunguzi kuna watu wanahojiwa,” ameeleza kwa ufupi bila kufafanua kwa kina.
 
B760036D-E173-4D20-BEA7-A6E539EE46ED.jpeg
 
"Tuiachie Mahakama ifanye kazi yake" na baada ya muda mfupi tushasahau na lengo la kujitwalia linakamilika bila kutumia nguvu halafu inarudishwa kwa jina kampuni nyingine.


Watanzania kuchakaa ni haki yetu, tunastahili.
 
Imeibwa vipi wakati ukipita pale masaa 24 police wapo lindoni..
 
Gas turbine(s) , uzito maelfu ya tani linaibiwa/yanaibiwa vipi mchana kweupe?
Unakuja.mtambo mkubwa kama winch kuja kunyanua hilo gas turbine lkn wanatushawishi kwamba kazi hii ilifanyika kwa usiri mkubwa Sana....... Tanzania nchi yangu.
 
Police ni majambazi ambao wako kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi.

"Mageuzi ndani ya jeshi la police ni lazima"
 
Back
Top Bottom