Askari ajiua kwa risasi baada ya kumjeruhi mkewe

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Askari Polisi mmoja aliyetambulika kwa jina la Michael Kyalo amejiua kwa kujipiga na risasi baada ya kumjeruhi mkewe kwa risasi huko Kaunti ya Bondo nchini Kenya mapema leo, Polisi wameripoti.

Kamanda wa Polisi wa kaunti hiyo Ibrahim Kosi amesema afisa huyo aliyefariki, aliripoti kazini kama kawaida jana, Ijumaa Julai 7 ambapo baadaye aliondoka na bunduki.

Hata hivyo, badala ya kuelekea eneo alilopangiwa, Kyalo alitembea hadi nyumbani kwake ambapo kisa hicho kilitokea Jumamosi asubuhi.

Mkewe Kyalo, ambaye alipigwa risasi, kwa sasa anauguza majeraha katika hospitali ya kaunti hiyo, huku mwili wa marehemu ukiwa umehifadhiwa katika chumba cha maiti hospitalini hapo.

Polisi wamesema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea huku wakihusisha ufyatuaji huo wa risasi unatokana na msongo wa mawazo kazini.

“Kesi kama hizo zinahusishwa na msongo wa mawazo katika jamii ambao umesababisha matukio mengi ya mauaji na kujiua,” polisi wamesema.

Takribani visa vitatu vya kujitoa uhai vinaripotiwa kila siku nchini humo kwa kasi kubwa.

Visa vya watu kujiua vimeongezeka mwaka huu nchini humo huku viongozi wakilaumu hali hiyo kuwa ni msongo wa mawazo.

Polisi walishughulikia kesi 499 mnamo 2019, na 575 mnamo 2020.

Takriban watu 313 wameripotiwa kujiua kati ya Januari na Julai 2021 huku wengi wa waiuwa wanaume, ripoti za polisi zimesema.

Shirika la Afya Duniani (WHO) linasema visa hivyo vinachangiwa na ukosefu wa ajira, kuvunjika kwa mahusiano au kifo.

Nyingine ni pamoja na matatizo ya kisheria, matatizo ya kifedha, uonevu, majaribio ya awali ya kujiua, historia ya kujiua katika familia, ulevi na matumizi mabaya ya vileo, mfadhaiko na ugonjwa wa msongo wa mawazo.

Ulimwenguni kote, karibu watu 800,000 hufa kwa kujiua kila mwaka huku takribani asilimia 78 ya visa vikitokea katika nchi zenye kipato cha chini na cha kati.

MWANANCHI
 
Duuh
 
Back
Top Bottom