Asiyejulikana amjaza mlemavu mimba 6

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,054
9,957
SERIKALI mkoani Mbeya imeombwa kuingilia kati sakata la binti mwenye ulemavu wa akili anayepewa mimba mfululizo na mtu asiyejulikana.
Hadi sasa amezalishwa watoto watano pasipo baba yao kujulikana na sasa ni mjamzito tena. Wananchi wameomba Serikali imtafute mwanaume anayempa mimba binti huyo.

Wakizungumzia suala hilo,baadhi ya wakazi wa Kata ya Iyela jijini hapa anakoishi mama wa mlemavu huyo ambaye hushinda akirandaranda mitaani wamesema kutokana na malezi duni wanayoyapata watoto kwa kulelewa na bibi yao asiye na uwezo ni vema baba wa watoto akatambuliwa ili aweze kuwajibika kwa malezi.

Wakazi hao wanaeleza kuwa kutokana na malezi duni yanayotokana na ufukara wa wa bibi anayewalea watoto tangu wakiwa wachanga baada ya binti yake anapojifungua yamesababisha watoto watatu kati ya waliozalishwa na mlemavu huyo kufariki dunia.

Mmoja wa wakazi hao Agrey Mkalawa ambaye ndiye anayemuhifadhi bibi wa watoto wa mlemavu huyo,Anna Kipsie kwa kumpa chumba kimoja anachoishi na wajukuu wake alisema umri wake hauendani na kazi ya kutunza watoto hao.

Mkalawa alisema bibi huyo amekuwa akiishi maisha magumu na wajukuu zake kutokana na kukosa msaada wowote zaidi ya ule wanaoupata kutoka kwa majirani hatua inayokwamisha wajukuu zake kuendelea na masomo.

Mkazi mwingine wa Kata ya Iyela Vumilia Nyalusi alisema “Tunaomba huyu mwanaume anayefanya haya atambue kuwa anachokifanya anamkosea hata Mwenyezi Mungu.Ukiangalia hata hapa mtaani maisha ya watoto wa huyu bibi yako tofauti kabisa na wengine. Huyo binti kuna wakati alikuwa kichaa kikipanda tunapokwenda kumsaidia tunajionea kabisa mazingira ya huyu bibi ni magumu wanalala chini yeye na wajukuu zake.”

Akizungumzia maisha yake,ya mwanawe na wajukuu zake, bibi wa watoto hao Anna kipsie aliyataja maisha yake kuwa magumu kwa kuwa anaishi pasipo kujua kesho yake ikoje na hivyo kushindwa kumudu maisha ya kulea wajukuu zake kwa kuwagharamia mahitaji mbalimbali ikiwemo ya shuleni.

“Kinachonisikitisha zaidi ni kwamba nasikia tayari binti yangu ana ujauzito mwingine. Sijajua huyo mtu anayemzalisha ana nia gani na maisha yetu.Maisha yangu ni magumu nahitaji walau kupata mtaji nifanye ujasiriamali wowote pamoja na uzee wangu. Nalala chini,sina pa kuishi,nawategemea tu majirani… wajukuu wanashindwa kwenda shule. Naomba Serikali inisaidie kumpata mtu anayemzalisha mwanangu.”alisema kwa masikitiko Mama huyo.

Mkuu wa dawati la jinsia mkoa wa Mbeya, Jannet Masangano alikiri Ofisi yake kuwa na taarifa za binti huyo na kusisitiza kuwa kinachofanywa kwa vyovyote na mtu anayemzalisha mlemavu huyo ni kitendo cha ubakaji kwakuwa ana imani hakuna makubaliano ya mahusiano ya kimapenzi yanayofanyika kati yao.

HabariLeo
 
Vyombo husika vya dola vingechunguza kwa kina hao watoto wa huyo mlemavu wa akili wanafanana na nani hasa hapo mtaani. Wakamate hata washukiwa watatu tu, wakawapime DNA ili atakaye bainika awajibishwe kwa mujibu wa sheria.
 
Wana uhakika ni mwanamme mmoja?
Nalaani ubakaji huo.
Wanaume wengine akili zenu,chafu sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyo si mwanaume mmoja
Huyo chizi anasikia raha akipigwa Ndio maana akipelekwa chochoroni kupigwa kuni anatulia kimya na uchizi wa kujificha kichochoroni hapigi kelele
Ila kuna mmoja kawazidi wenzake
Chizi hapelekwi guest

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom