Wazazi wengi umri umeenda wana watoto wajukuu

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,513
Habari wakuu,

Husika na kichwa cha habari,

Niende moja kwa moja kwa mada yetu ya wazazi wengi wa Sasa kuwa na umri mkubwa na wana watoto wajukuu.

Ukikutana na wababa au wamama wengi wa Sasa wanawatoto wadogo sana, hii imepelekea na hali ya maisha ya kuchelewa kuoa au kuolewa.

Moja kati ya sababu kubwa ya kuchelewa kuoa na kuolewa ni kwakuwa watu wengi Sasa wamekuwa waoga kuoa.

Hii ni kutokana na kuona vitimbi vinavyowasibu baadhi ya wanandoa na kupelekea kuchelewa sana.

Hivyo wanakuwa wanakaa kwanza kusubiria kwanza jua likuchwe ndio wanaingi kwenye ndoa.

Pia sababu kubwa sana ni hali ya maisha kwa ya watu, maisha yamekuwa magumu, hivyo wanaume wanasaka pesa kwanza ndio waingie kwenye ndoa.

Sasa hali hii ya kuchelewa inapelekea kuoa na kuolewa umri ukiwa umeenda na wanazaa watoto ambao kwa umri wao wanaonekana kama wajukuu.

Swala la malezi nalo linakuwa gumu kwao kwakuwa umri umewatupa mkono, wanaona kama wapo na wajukuu.

Hivyo inakuwa ngumu kuwakemea watoto, wanakuwa wanawadekeza, si ndo washakuwa bibi na babu.

Watu wanaochelewa kuoa na kuolewa ndio chanzo Cha mmomonyoko wa maadili kwa watoto waliopo mtaani huko.

Wazazi wao hawajali watoto kwakuwa umri umeshawatupa mkono.

Ni vyema kuzaa watoto mapema ili kupata muda wa kuwalea vizuri.

Donatila
 
Inategemeana umeishi kwenye mazingira gani. Sasa hebu fikiria unagonga miaka 29 bado upo masomoni, 30 unaanza kusaka ajira za maofisini unagonga mpaka miaka 40 ndio unashituka unaona usife bila kuacha mtoto duniani. Ukipata yeyote unazaa naye fasta. Kama una hela unaweza kupata binti mbichi miaka 20 akakuzalia walau watoto wawili vinginevyo itabidi upate mkongwe ambaye bado anaweza kuzaa angalau watoto wawili ndio afike ukomo na mara nyingi hao wamama ni wajane waliokaa muda mrefu tangu wafiwe au waliochwa na na waume zao ila hizo ndoa za wama wenye watoto tayari si nzuri kwa ambaye ndio kwanza anaoa. Kuhusu malezi na makuzi ya watoto wa uzeeni ni mungu tu ndiye ajuaye. Kuzaa uzeeni si ajabu
 
Wakati mwingine ndoa zinazingua sana. Una miaka 20 unamuoa binti wa miaka 18 wengine tunaoa mpaka 14, 15 mradi asiwe mwanafunzi, inafika wakati mnazinguana na kuachana huku mna watoto wawili au mmoja. Unaanza kuona ndoa ni mzigo, ni usumbufu, unaanzaa kuishi maisha ya ubachela mpaka utu uzima unafikisha miaka 40 unakumbuka maisha ya ndoa na unarudi ndoani hata na mwanamke mwingine mradi tu yuko active kwa uzazi anakuzalia watoto chapchap zaidi ya moja kama bado una uhitaji wa watoto wengine zaidi. Nadhani umri wa kuza hauna muda maalumu as long as watu wana mayai na mbegu. Ndio maana haishangazi kuona mama na binti yake, kijana na baba yake bado wanazaa yaani watu wana wajukuu lakini bado wanazaa sambamba na watoto wao. Sasa ukute sikuzaa ujanani na mbegu ninazo sina shida ndio niache kuzaa uzeeni wakati nahitaji mtoto? Kwenye uzazi no limit mpaka mayai na mbegu ziishe au ziwe na changamoto ya kuunda kiumbe
 
Malezi ya watoto je?

Maana umri unakuwa umeenda, nguvu za kukimbizana na watoto kujua wanafanya Nini unakuwa huna...
 
Habari wakuu,

Husika na kichwa cha habari,

Niende moja kwa moja kwa mada yetu ya wazazi wengi wa Sasa kuwa na umri mkubwa na wana watoto wajukuu.

Ukikutana na wababa au wamama wengi wa Sasa wanawatoto wadogo sana, hii imepelekea na hali ya maisha ya kuchelewa kuoa au kuolewa.

Moja kati ya sababu kubwa ya kuchelewa kuoa na kuolewa ni kwakuwa watu wengi Sasa wamekuwa waoga kuoa.

Hii ni kutokana na kuona vitimbi vinavyowasibu baadhi ya wanandoa na kupelekea kuchelewa sana.

Hivyo wanakuwa wanakaa kwanza kusubiria kwanza jua likuchwe ndio wanaingi kwenye ndoa.

Pia sababu kubwa sana ni hali ya maisha kwa ya watu, maisha yamekuwa magumu, hivyo wanaume wanasaka pesa kwanza ndio waingie kwenye ndoa.

Sasa hali hii ya kuchelewa inapelekea kuoa na kuolewa umri ukiwa umeenda na wanazaa watoto ambao kwa umri wao wanaonekana kama wajukuu.

Swala la malezi nalo linakuwa gumu kwao kwakuwa umri umewatupa mkono, wanaona kama wapo na wajukuu.

Hivyo inakuwa ngumu kuwakemea watoto, wanakuwa wanawadekeza, si ndo washakuwa bibi na babu.

Watu wanaochelewa kuoa na kuolewa ndio chanzo Cha mmomonyoko wa maadili kwa watoto waliopo mtaani huko.

Wazazi wao hawajali watoto kwakuwa umri umeshawatupa mkono.

Ni vyema kuzaa watoto mapema ili kupata muda wa kuwalea vizuri.

Donatila
Hiyo sio sababu kubwa,Mimi nilifiwa na mke,nikaoa Tena Nina mtoto na hyu mke anaumri sawa na WA mtoto wangu,Sasa nifanyeje kama alinasa,Niko fit!
 
Back
Top Bottom