DOKEZO Asilimia 80 ya maji ya kopo Dar es salaam ni feki na machafu, hayafai. Kwa hali hii usalama wetu uko wapi?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Mganguzi

JF-Expert Member
Aug 3, 2022
1,032
2,769
Kujali afya ya binadamu mwenzio hata kama unafanya biashara na unatafuta hela ni muhimu sana.

Wafanyabiashara mnatuua bila huruma sisi waja wema. Nimefika Mbezi mwisho barabara inayokwenda Kinyerezi kuna ofisi maalumu ambayo wanakusanya makopo na kupakia maji machafu yasiyofaa hata kidogo.

Wanaweka package na vifuniko wanayatia kwenye friji na kuwauzia wateja kama maji orijino. kwa kuwa yanakuwa baridi sana huwezi kugundua chochote. Hao wamana wanaofanya kazi hapo na mazingira ya eneo ni machafu kupindukia, makopo hayaoshwi na wanayaokota majalalani na kwenye mitaro michafu.

Makopo mengine yanakuwa na mikojo wao hawajali hilo wanachojali ni kupata pesa. Hii ni hatari sana!

Maji haya tunawanywesha watoto na wagonjwa. Ndiyo sababu magonjwa ya kuhara haishi hapa mjini. Jeshi la polisi na wenye viwanda jaribuni kubuni namna nyingine na kufanya misako kwa wenye hizi biashara. Wanatuua bila huruma.
 
Dar es salaam ni sehemu nzuri kibiashara lakini ni PACHAFU SANA. Kuna uchafu wa kila aina kuanzia kwenye vyakula, vinywaji na hata mazingira kwa ujumla

Kunanuka shombo kule ferry, chemba za vyoo vinavyofunguliwa hasa nyakati za mvua, majalala yenye miozo kila kona

Hilo jiji ni chafu mno, haishangaza kuuziwa maji machafu

Nikiwa Dsm kwa siku kadhaa huwa nakuja na carton ya maji ya Kilimanjaro nayouziwa 4500 tu kwa jumla ya 1.5 ltr kwa chupa 6

Dsm hovyo sana
 
Kujali afya ya binadamu mwenzio hata kama unafanya biashara na unatafuta hela ni muhimu sana...
Hii ni kweli inatokana na serikali kuzuia vile karatasi vya plastiki kwenye mifuniko ya chupa za maji.

Sasa hiyo imekuwa fursa kwa wahuni coz sasa hivi huwezi kujua if chupa ilishatumika au hapana sababu chupa iliokwisha tumika na chupa mpya zote zinafanana.

Sasa hivi wanachokifanya wahuni wengi hasa hawa wanaouza maji barabarani wanaokota chupa zilizotumika wanajaza maji then wanauza.

Mimi kuna siku nimenunua maji ya Hill water ubungo maji yanachumvi balaa nilichongudua yule jamaa alieniuzia kachota kwenye kisima. yale maji yalinishinda nikamwaga.

Hapo serikali iangalie uwezekano wa kuweka seal kwenye hizi chupa za maji

Hili tatizo limekuwa kubwa.
 
Kujali afya ya binadamu mwenzio hata kama unafanya biashara na unatafuta hela ni muhimu sana.

Wafanyabiashara mnatuua bila huruma sisi waja wema. Nimefika Mbezi mwisho barabara inayokwenda Kinyerezi kuna ofisi maalumu ambayo wanakusanya makopo na kupakia maji machafu yasiyofaa hata kidogo...
Hiyo ofisi maalumu ni ipo mkuu
 
Mzee. Hayo maji yanakuwa hayapo sealed unalalamika kwa Nini , kwa Nini ununue, Kuna siku napita kko nikaukiza hayo maji wanasema bei mia mbilii nikapita zangu kushoto na kuondoka lakini mtu mwingine akanunua , kwa hiyo kupanga ni kuchagua.
 
Dar es salaam ni sehemu nzuri kibiashara lakini ni PACHAFU SANA. Kuna uchafu wa kila aina kuanzia kwenye vyakula, vinywaji na hata mazingira kwa ujumla..
Kilimanjaro hii hii ya Buza

USSR
 
Back
Top Bottom