Asili ya maneno 'Shikamoo' na 'Marahaba' ni utumwa, kwanini tunaendelea kuyatumia?

Hakuna kitu kama hicho, isipokuwa ukiwa na hela heshima ya ukweli lazima iwepo!! Mzazi hawezi kumpa shikamoo mtoto hata siku moja
 
Hakuna kitu kama hicho, isipokuwa ukiwa na hela heshima ya ukweli lazima iwepo!! Mzazi hawezi kumpa shikamoo mtoto hata siku moja

Chezea pesa wewe!
Hujawahi kuona kijana mdogo tu anaitwa 'mzee' kwa ajili ya pesa?
 
We Mchagga ikiyezaliwa magorofani hata kijiji chenu hukijui ni bora kukaa kimya....

Huo ni mtazamo wako, unajua kwa nini huyu jamaa kasema wanatoa shikamoo kwa watoto wao!! Wachagga wanapenda kutumia lugha yao popote pale walipo (hasa salamu) na shikamoo kwa Wachagga ni salamu ya nadra sana, mfano mimi mtoto wangu (akiwa na mwaka na nusu) nilimpeleka Moshi kukaa na bibi yake mwaka mmoja tu!! Karudi huko neno shikamoo halijui kabisa kabisa sasa kwa wasiojua wakawa wanasema mtoto ana tabia si nzuri!!

Uzuri ni kwamba salamu zao zina jinsia na ukubwa!! Kwa mfano Chamechambe au Shimbonyimbe hizo ni kwa ajili ya mwanaume lakini "mbe" ni baba!! Sasa baba anapoanza kumsalimia mwanae ndipo hapo wanasema anamuamkia sababu ataanza kusema 'chamechambe au shimbonyimbe" coz mtoto wake labda ni wa kiume!! Upo? Ndo hapo wanaposema wanaamkia watoto wao ila ni kumpa heshima ya uanaume tu!!

Kwa mwanamkeni "shimbonyi mae au chamechame" na me ni mama. Utapomsalimia mwanao wa kike ndipo unaonekana unamuamkia but sivyo ndugu ni kama umesalimia kwa kiswahili "habari yako mwanangu wa kike/kiume?"
 
Huwa sitoi shikamoo. Cha muhimu ni kujua hali ya uliyekutana nae. Hivyo,habari za saa hizi inatosha!
 
kila kitu ulichoandika hapo juu umepatia.ni neno la kitumwa kweli lakini ndio hivyo mababu zetu kwa kupenda umwinyi wakaliendeleza tu.mara nyingi mimi huwa nalikuwepa neno hilo kwa kutumia "asalam aleykum".
Refer chei chei kwa watoto na wanawake pande za zenji!
 
Ok inajulikana kuwa shikamoo ni salaam unayompa mtu aliyekujizi umri (sifahamu kama kuna age limit) Ila Kuna wababa wengine especially binti wa kike akimwambia shikamoo humjibu "salama tuu binti hujambo".And why is that?.

Mwana mama;
Mzee Tupatupa siku hizi hushikiki, kwa kupenda uvulana, shikamoo pia huitaki,
Tupatupaee, wazee wenzako tupo tele, hututakieee, kilasiku nawasichanaaaaaaaa.

Tupatupa;
Nimoyo unaotamaniee, namoyo huwa hauzeekieee, na macho hayana mpaka.
Tatizo ni kwamba kila ninachoona moyo wangu unatamani.
 
Na je,wale watu ambao wanatoa hiyo shikamoo kwa mtu ambaye kiuhalisia amemzidi umri,ila ni kwasababu ya kipato(utajiri) ili kupata ajira,na hapo utazungumzia umri?
 
SHIKAMOO - MARAHABA SHIKAMOO MARAHABA.

Shikamoo ilikuwa ni salamu za watumwa kwa mabwana zao. Na ilimpasa mtumwa kupiga magoti na kusema shikamoo Bwana (Maana yake nashika miguu yako Bwana) na Mmiliki wa watumwa au "BWANA" anajibu MARA HABA ( maana yake shika Mara saba).

Kwa sasa nchi karibu zote zinazotumia lugha ya Kiswahili hawatumii salamu hii isipokuwa Tanzania tu ambako salamu hii bado ni maarufu. Mimi najiuliza hivi kuna sababu yo yote ya sisi kuendelea kutumia salamu hii ya SHIKAMOO - MARAHABA ambayo ina historia Mbaya sana kwa nchi yetu???

Rakesh Rajani mkurugenzi na mwanzilish wa Mashirika maarufu ya Kuleana, HAKI ELIM na Twaweza aliwahi kuomba kukutana na mwl JK Nyerere. Yeye hatumii kabisa salamu hii na alishaikataa jumla. Kwa mujibu wa simulizi zake katika gazeti la Raia mwema wiki hii, alipokutana na Mwl Nyerere alimsalimia " HABARI ZA ASUBUHI MWALIMU"

Jambo hilo liliwaudhi sana wasaidizi na walinzi wa Mwalimu na ikabidi ajieleza kabla ya kueleza kilichompeleka kwa Mwl Nyerere. Mwl alimwelewa na kumsifia sana kwamba anahoja nzuri na akakubaliana na Rakesh Rajani.

Narudia tena swali langu, na waswahili wanasema kuuliza siyo ujinga na wala si dhambi je, sisi watanzania tuna sababu ya kuendelea kutumia salamu hii yenye historia mbaya? Aulizaye anataka kujua na ni jambo jema, naombeni msaada wenu.
 
Ukirejea historia, utakataa kila kitu au kila neno. Yapo mambo mengine unapaswa kukubaliana na wakati hasa yanapokuwa hayana maana ile ile.

Maneno kama kupiga bao, kukaza, tigo, masaburi, kihiyo nk yameshageuzwa. Kuifuta shikamoo na marahaba leo ni kazi kweli kweli.

Lakini lugha huzaliwa na kufa. Maneno kama kabwela, bwanyenye, mabeberu, makaburu nk kidogo kidogo yanatoweka. Tusubiri na hii shikamoo-marahaba nayo ipate natural death!!
 
Ina historia mbaya lakini kwa mazingira ya sasa na jinsi tunavyoitumia mantiki yetu si ya kitumwa.Tuendelee tu kuitumia ilimradi tu hatumaanishi anayesalimiwa ni BWANA na anayesalimia ni MTUMWA.Ila dhana yetu iwe kwenye heshima tu
 
Ni tafsiri tu. Kwa sasa maana yake mdogo anaonyesha heshma kwa mkubwa na mkubwa anaipokea. Nchi nyingi kuna hali fulani ya mkubwa kusujudiwa. Mfano China, ukiwa mdogo utamsujudia mkubwa (bowing).

Ni kitambulisho kizuri sana, ikiwa kweli ni tz tu tunaitumia.

Huku Arusha watalii hufundishwa kutoa shikamoo na kupokea marahaba.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom