Asili ya maneno 'Shikamoo' na 'Marahaba' ni utumwa, kwanini tunaendelea kuyatumia?

Good point. Umejibu vizuri na umeeleweka. Ila kwa sababu zisizo na msingi kwenye S umeweka X nimekupuuza.

Mkuu, kwenye Kiswahili hatuna herufi "X" lakini nashangaa matumizi yake ktk Kiswahili yameshamiri sana. Kwa kifupi inakera nami nakereka na matumizi haya.
 
Ukimsalimia mtu aliyekuzidi umri "habari yako "ni kukosa heshima?
 
Kuna rafiki yangu Mmarekani alikuja hapa Tanzania tangu mwaka 1975, Kiswahili anakijua, ukimwakia shikamoo anakasirika sana! na siku moja nilimuuliza kwa nini akasema ni salamu ya kidhalilishaji! inamdhalilisha anaesalimia, ki ukweli sikumuelewa na hadi leo mimi bado naitumia hii salamu hasa kwa walionizidi umri!
 
Kuna rafiki yangu Mmarekani alikuja hapa Tanzania tangu mwaka 1975, Kiswahili anakijua, ukimwakia shikamoo anakasirika sana! na siku moja nilimuuliza kwa nini akasema ni salamu ya kidhalilishaji! inamdhalilisha anaesalimia, ki ukweli sikumuelewa na hadi leo mimi bado naitumia hii salamu hasa kwa walionizidi umri!

Huu ni ukweli mchungu ambao itachukua miaka 5 - 20 kufa. Nakubaliana na mtoa mada na nina uhakika kwa kizazi hichi hii salam inakufa anaebisha alete utafiti ambao umefanyika au unafanyika kuhusiana na salam hii. Binafsi nikiamkiwa shikamoo siitikii labda ibidi kabisa. Wito wangu kwa mamlaka zinazohusika na tafiti za kiswahili walifanyie utafiti suala hili waje na majibu, MBONA NINAIONA PHD THESIS NZURI HAPA????
 
shikamoo sio deal ni bora ingekufa tu kitambo,

Ajabu sana sipendi nipewe sijiskii kuitoa lakini mazoea yana taabu mtoto akiniambia habari gani najihisi vibaya-'amenidharau' nikutana na aliyenizidi umri tena mbali sia amani kumuamkia -'habari gani' mimi binafsi naona tukubali yaishe tuendelee nayo tu kazi ya kuibadili salamu hii ni ngumu na huenda siyo ya lazima kivile. tuweke mkazo kwenye mengine ya muhimu zaidi katika maendeleo yetu
 
Huu ni ukweli mchungu ambao itachukua miaka 5 - 20 kufa. Nakubaliana na mtoa mada na nina uhakika kwa kizazi hichi hii salam inakufa anaebisha alete utafiti ambao umefanyika au unafanyika kuhusiana na salam hii. Binafsi nikiamkiwa shikamoo siitikii labda ibidi kabisa. Wito wangu kwa mamlaka zinazohusika na tafiti za kiswahili walifanyie utafiti suala hili waje na majibu, MBONA NINAIONA PHD THESIS NZURI HAPA????

Ushaona mbunge ana miaka sitini kaolewa na kijana ana miaka 26.

Sasa kama huyo unaweza kumpa "heshima" yake kwa shikamoo akachukia kwamba unamzeesha.
 
Na ife mapema kabisa maana imejaa unafiki na unyanyasaji. Mtu anakuamkia huku nyuma anakudharau na wala hakupi heshima ya kutoka moyoni. Ukimkuta kijana mdogo ni bosi kitendo cha kuwapo shikamoo wasaidizi wako ndo umefungulia njia ya kukudharau na kuku control ni hatari kabisa hii salam.
 
Hamujitambui;- SHIKAMOO ni usemi wakusalim kutok kwa wa rika la chini kuumpa wa mkamu !!
utamaduni na mila hii ipo kiafrika haswa !! nasiyo kama baadhi wasemavyo eti ni ya utumwa !!
Je kwani neno BWANA, MHESHIMIWA,BIBI hutumika?
Shikamoo na marahaba ni connection ya mtu kwa mtu!! au mwataka tutumie miluzii? puuuuzzzz
 
Maana ya Maneno katika lugha hubadilika kimatumizi kadiri muda unavyokwenda. Chukulia neno SILLY lilimaanisha 'deceitful' lakini kwa sasa linamaanisha 'stupidity'; na kuna Maneno mengi yaliyobadilika kimatumizi kutokana na muda. Hiyo perception na study unayorejea inaweza kuwa si kweli kwa sababu wote tunaishi kwenye jamii ile ile. Kwa mtazamo Wangu shikamoo ni salaam inayoiwekea jamii yetu heshima BA 'upekee' wa aina yake kama jamii yenye lugha na utamaduni. Tusilete perception na viutafiti kuharibu lugha yetu adhimu ya kiswahili. Shikamoo ilishakuwa salamu ya heshima kitambo.
 
Angalia Shikamoo ilivokuwa haina Maana. Waweza salimia jimama kumbe lachukuliwa na kitoto kidogo zaidiyo. Hapo mii ndo nachoka. Kilichobaki ni Tumsifu Yesu..... au Assalaamu Ale... Basi.
 
Nianze na kuuliza , nini maana ya neno "shikamoo"?

Kuna sehemu nimeona na kusikia kuwa maana yake ni "nipo chini ya miguu yako". Salamu ambayo watumwa walikuwa wanawasalimia mabwana zao (kama maana niliyotoa si sahihi naomba msaada wenu kurekebisha hapo).

Asa swali langu ni dogo tu, Je mpaka sasa bado kuna utumwa hapa Tanzania?!

Ni kutuko maana mpaka mtu mzima mwenye akili zake bila hata aibu anallilia "shikamoo" alaf baada ya hapo anajisifu kuwa eti 'Tanzania hakuna utumwa'

Hivi hili baraza la Kiswahili wanafanya kazi gani sasa?

Nimejaribu kuchunguza kidogo na kubaini kuwa salamu ni kujuliana hali au kutakiana heri! mfano, kwa Kingereza wanasalimia "Good morning" wakimmaniasha asubuhi njema "Good evening" wakimaanisha jiono njema n.k, kwa Kihaya kuna "Ma' Olailoota" mama umalalaje/umeamkaje (kama sijakosea) najua kuwa kuna salamu za makabila mangine mengi tu wakijuliana hali na kutakiana heri. Lakini Kiswahili chetu kinashangaza, eti shikamoo!

Kwa mimi napendelea zaidi "habari za saa hizi", "za saa hizi" au hata "mambo" inatosha sana kulliko hata shikamoo. Ila kutana na kibabu fulani kiambie "za saa hizi" utasikia "mtoto anajifanya amekua huyu eenh!!"
mimi naishia hapo kwa leo.

Nawasilisha Hoja!!


 
Maana ya shikamoo ni hii ambayo inatumika sasa na Waswahili, hiyo uliyoitoa haipo katika kamusi tunazotumia. Inawezekana ilikuwa inatumika zamani wakati wa utumwa, lakini lugha hubadilika, maneno hubadilika na halikadhalika maana za maneno nazo sio tuli.

Tanzania hakuna utumwa, huu ni mfumo wa maisha na hauwezi kuamuliwa na uwepo wa neno moja tu katika lugha nzima. Kung'amua uwepo wa utumwa ni lazima tuchunguze mifumo ya maisha ya Watanzania na sio kutazama neno moja kisha kuhitimisha.

Watu wazima huwa 'wanalilia' hiyo shikamoo kwa kuwa ndio utaratibu wa jamii kuwa salamu hii itatoka kwa mdogo kwenda kwa mkubwa. Kama ambavyo tu mtu huyu huyu mzima anavyolilia kupishwa siti kwenye daladala wakati haijaandikwa popote.

Baraza la Kiswahili la Taifa hutunga sera ya Lugha pamoja na kuishauri Serikali masuala mbalimbali yanayohusu lugha. Kiswahili hakishangazi, bali kina namna yake ya pekee ya kutazama salamu (Salamu kama kujuliana hali, na salamu kama ishara ya heshima). Wanaofahamu lugha ya kibantu yenye dhana hii pia wanaweza kuja kutufahamisha. Ukishangaa ya Kiswahili inabidi ushangae pia na Kifaransa ambapo majina yake huwa na jinsia (eti kuna gari la kike na la kiume... Inachekesha eeh?)

Kupendelea kutumia aina fulani ya salamu ni haki yako, lakini isije kukugharimu ukweni siku moja (natania tu).

Hoja yako umeiwasilisha vema, karibu sana.
 
Salaam Wana Jamvi!

Nimewahi sikia kuwa baadhi ya ndugu zetu wa Kichagga hasa upande wa wazazi, wana kawaida ya kuwapa heshima sana watoto wao hasa wale wenye pesa (mbesaa)na wako vizuri kimaisha na kinyume chake wale watoto ambao hawana 'mbesaa' uonekana si chochote si lolote mbele ya wazazi!

Kwamba ni kawaida mzazi kumtwanga 'shikamoo' mtoto mwenye 'mbesaa'!
Eti mtoto uamkiwa, 'Shikamoo mwanangu'.

Wachagga, hivi ni kweli kuhusu hili?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom