DSC_5689.JPGtt.JPG


MKE WA RAIS WA ZANZIBAR MAMA SHADYA KARUME AKISALIMIANA NA WANAFUNZI WA SKULI YA MSINGI YA UZINI WAKATI KALIPOWEKA JIWE LA MSINGI LA SKULI YA MAANDALIZI YA TUNDUNI WILAYA YA KATI KUSINI UNGUJA LEO


DSC_5638.JPG


MKE WA RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI NA MWENYEKITI WA JUMUIYA YA ZAYEDESA MAMA SHADYA KARUME AKIONDOSHA KIPAZIA KUASHIRIA KUIZINDUWA RASMNI SKULI YA MAANDALIZI YA CHEKECHEA [B][COLOR=Red]TUNDUNI UZINI [/B]JANA[/COLOR]

DSC_5649%5B1%5D.JPG


MKE WA RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI MAMA SHADYA KARUME AKLIPANDA MNAZI BAADA YA KUIFUNGUWA SKULI YA MAANDALIZI WA WATOTO KATIKA KIJIJI CHA TUNDUNI UZINI WILAYA YA KATI JANA. PICHA NA OTHMAN MAULID WA ZANZIBAR LEO

Chanzo: Michuzi Blog
Jamani ``tunduni uzini``si matusi hayo?
 
This is Great Thinking sio ohh Clouds FM ohh hajasoma Kibonde, ohh Kanumba kiinglish kinampita kushoto nk. This is what JF is all about (Historians) n people who can apply their knowledge. Thanks my people. Natamani niwagongee THANKS button everyone on this thread. I SALUTE YOU
 
Jina Kariakoo lilianza tokea enzi kabla ya mjerumani, kijiji hiki kiliitwa "Carrier Corps." Hii sehemu ilipata umaarufu sana kwa sababu ilikuwa frequently raided by slave masters kuja kuchukua watumwa. Kwa mantiki hii, jina halisi ni Carrier Corps ila wenyeji walitamka walivyoweza, hence, Kariakoo.

Wakati wa vita vikuu vya pili, katika sehemu inayoitwa sasa Kariakoo, kulikuwa na kambi kikosi cha mizigo ya jeshi la wakati huo, Kings African Rifkes (KAR) na kikosi hicho kilikuwa kinaitwa Carrier Corps. Kwa sababu Waswahili walishindwa kutamka matamshi hayo, walipaita Karia Koo!!

Duh, mkuu SMU. Hivi na Kariakoo maanake nini?

Mkuu nadhani utapata jibu la swali lako kutoka hizi post za nyuma, japo historia iliyotolewa haifanani sana
 
Msasani maana yake ni kwamba huko aliishi mzee aitwaye MUSA HASANI wazungu walishindwa kutamka vizuri jina hilo na kuita msasani mpaka leo ni msasani,
Mnyamani vilevile aliishi mzee wetu MWINYI AMANI.
VINGUNUTI, Ni kwamba kulikuwa na vijizee vilivyokua vinauza maeneo kariakoo na kukimbilia maeneo ya vinginguti kipindi hicho ni pori sasa hivi vizee vilikua vinatia timu kwa wingi sasa washkaji katitika ile hali ya kuelezea ujio wao waliua wakisema VINGUNGU TII yaani vingungu ni vijizee na tii ni kutia tim. upo hapo kaka?
UBUNGO: palikua na miti ya mibungo mingi.
OSTABEI, ni kutokana na kuwepo kwa samaki waitwao oister. kwa hiyo pakawepo na bandari ya oister. yaani OISTERBAY.
mkuu najua mengi ila kamda ka kukaa net hakanitoshi kwa leo ngoja niiishie hapa.
 
je manzese mnaijua historia yake?
kulikuwa na bi mkubwa akkitwa halima bint Manzese alikuwa kaajaliwa uzuri enzi hizo, akawa akiuza pombe kilabuni basi wasela wote wa dar, hasa maeneo ya magomeni na kariakoo wakawa wakienda kilabuni kwake kunywa,lakini hasa kilichokuwa kikiwavua ni uzuri wa maumbile ya bint manzese hivyo ikifika kila jioni wanajisogeza kwa bint manzese,kwa wao kifupi wanaambia jioni wapi ..! MANZESE... ndio jina likakolea ki hivyo.
 
MANZESE ALIKUWA BINTI AKIITWA HALIMA BINT MANZESE ALIKUWA MZURI kweli kweli SI HABA manake mtoto natural, kutokana na uzuri wake manaume wengi walikuwa wakimmendea hivyo kwa akili aliyojaaliwa akafungua klabu ya kuuza pombe basi midume kibao ikawa inamiminika kwenda kunywa hapo kilabuni kwa minajali ya kumnasa bibie, bi Halima akawa akitengeneza bingo la ukweli kutokana na haiba ya uzuri wake na biashara ikichangamkiwa kila jioni kwa mbaba kumiminika kunywa na kumtaka kimapenzi basi ndio ikawa Gumzo kila mtu manzese..!...!...! manzese manzese ndio mpaka leo eneo limekuwa na jina hilo.
 
Nilipata simuliwa na babu yangu kuwa sehemu inayoitwa Keko magulumbasi kulikuwa na mzee mmoja anaitwa Magulumbasi, mzee huyu alikuwa nafuga mbuzi wengi sana lakini alikuwa hawachungi, na kwa mujibu wa simulizi za babu yangu ni kuwa watu hawakuthubutu kuiba wale mbuzi na walikuwa wanafika hadi maeneo ya SOKOTA, sasa ndio watu wakawa wamepatambua kwa jina la Keko kwa Magulumbasi, na sasa neno"kwa" limetoka panajulikana kama keko magulumbasi

Nilisikia pia ule mtaa wa Wailes uliopo Temeke umetokana na neno wireless, lakini historia yake siipati vizuri msaada!
 
Tanga asili yake ni neno la kizigua, niliwahi ambiwa kuwa kulikuwa na watu fulani walienda pale tanga zamani sana na walifika sehemu ulipo mji wa tanga sasa na walikuta nyumba pale na kulikuwa na watoto nje, wakawauliza wazazi wenu wako wapi wakasema" waita ntanga" yaani wameenda shamba! sasa hiyo ndio asili ya neno TANGA

Ikulu asili yake ni unyamwezi hasa enzi za mtemi Milambo, makao makuu ya ngome ya milambo paliitwa kwikulu, ndio neno ikulu likatoholewa toka hapo
 
Wandugu majina ya maeneo mbalimbali hapa TANZANIA na asili yake hebu tukumbushane machache kati ya haya :-

-KARIAKOO-carrier cool
-MSASANI-musa hasan
-BAGAMOYO-bwaga moyo



eti kuna maeneo mengine mnayoyajua ama ni haya haya au yapo mengine.
 
Mikocheni = Michael Cheni

Uongo.......miaka ya zamani kulikuwa na miti mingi iitwayo Mikoche,ikifanana na minazi ndio asili yake...Gongo la Mboto ni kweli kukiuwa na mtu itwaye Mboto aliyekuwa mataalamu wa kupika gongo miaka hiyo kukiwa porini sana
 
Mwana Nyamala kizaramo ni ''mtoto nyamaza''....miaka hiyo kulikuwa na Simba sana maeneo hayo na kulikuwa na mama akisafiri na mwanawe aliyekuwa analialia hivyo kwa hofu ya kuliwa na Simba mama yake alikuwa akimnyamazisha...wakaliwa na Simba na watu walipofika asubuhi wakatoa ushuhuda wa kumsikia mama huyo akilia ''MWANA NYAMALA'' na jina likaanzia hapo
 
popo bawa,kwa bibi,yemen,tandale,cinza kwa remi,samaki mbezi,fundi kira,naombeni yalivyotokea
 
Uongo.......miaka ya zamani kulikuwa na miti mingi iitwayo Mikoche,ikifanana na minazi ndio asili yake...Gongo la Mboto ni kweli kukiuwa na mtu itwaye Mboto aliyekuwa mataalamu wa kupika gongo miaka hiyo kukiwa porini sana

haha haa mbavu zangu dah.. sijui ni ukweli, sijui ni uingo.. mi sijui, lol
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom