JokaKuu
Platinum Member
- Jul 31, 2006
- 30,441
- 55,018
Nyani Ngabu said:Okay, si alikuwa waziri huyu? Kama ni hivyo basi pia alikuwa mbunge. Huko bungeni mchango wake ulikuwa nini? Alisimamia nini? Vipi kuhusu ufisadi? Aliupinga kwa kadri ya uwezo wake? Alipendekeza bill ngapi na zipi?
Nyani Ngabu,
..Dr.Migiro alikuwa mbunge wa viti maalum kupitia CCM. pia baada ya kupata nafasi ya ubunge moja kwa moja aliteuliwa kuwa Waziri wa Maendeleo ya Wanawake na Watoto.
..mchango wa Dr.Migiro kama mbunge ni tofauti na ule wa kina Dr.Slaa,Zitto,Selelii,Kilango, katika masuala ya ufisadi. kama tunataka kumpima kuhusu alivyopambana na ufisadi tuangalie utendaji wake kama Waziri ktk wizara ya wanawake na maendeleo ya Jamii, na wizara ya mambo ya nje.
..mpaka sasa hivi sijasikia kuwa Dr.Migiro alikuwa na kashfa yoyote ile akiwa Waziri wa wanawake na maendeleo ya jamii, au waziri wa mambo ya nje. nadhani huo ni mwanzo mzuri. kitu ambacho nitapenda kukisikia ni mabadiliko gani aliyasimamia akiwa waziri ktk wizara hizo mbili.
..kwa upande mwingine, Dr.Migiro ni mmoja kati ya kina mama wanaharakati waliokuwa wakifanya kazi ya uanasheria wa kujitolea kusaidia wanawake wasiojiweza waliohitaji msaada wa kisheria. nadhani rekodi hiyo inaweza kutoa mwanga, kwamba linapokuja suala la HAKI haswa za wanyonge, UTAWALA WA SHERIA NA KATIBA, mama Migiro atasimamia wapi.
NB:
..nchi za magharibi zinai-undermine UN halafu wanazunguka na kudai it is an irrelevant institution.
..naamini UN imefanya kazi kubwa sana, and it is relevant, katika masuala kama elimu[unicef], afya[who], maji na makazi[habitat], and relief operations[unhcr].