tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 22,378
- 19,213
Habari wakuu! Naingia kwenye mada moja kwa moja bila kuwachosha wala kuwapotezea muda. Leo nimeona waraka mzuri sana kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (MoEVT) unaoruhusu wanafunzi wenye imani ya Rastafali kuruhusiwa kuvaa kofia kufunika nywele zao kwani hiki kimekuwa kilio cha muda mrefu tangu serikali zilizotangulia. Hili limewezekana tu katika awamu hii ya sita inayoongozwa na Jemedali, Chifu Hangaya, Rais Samia Suluhu Hassan. Nakupongeza sana kwa kujali imani za watu unaowaongoza. Mama anaupiga mwingi jamani! Wenye roho mbaya mkajinyonge au msage sumu mnywe, tutakuatana mbinguni.
Lakini pamoja na pongezi hizi, nakuomba mama yangu Rais Samia uwaruhusu vijana wa kiislamu nao waweze kuvaa kanzu na baragashia ili kuondoa dhana ya upendeleo. Sio kwamba waislamu hatuna shukrani, la hasha! Tunakupongeza sana kwa kuruhusu mabinti wa kiislamu kuvaa hijabu wawapo mashuleni na vyuoni lakini tunasikitika watoto wa kiume hawaruhusiwi kuvaa kanzu na baragashia kwanini? Tatizo liko wapi?
Najua huenda wasaidizi wako wa chini ndio wanakushika miguu lakini nafahamu una uwezo wa kutoa amri leo na kesho Waziri wa Elimu akaandika waraka wa kuruhusu jambo hili kutekelezwa. Tunajua hushindwi kitu mama yetu kwani huwa unahakikisha watu wa imani zote wanatimiziwa matakwa yao bila kuathiri maslahi ya watanzania wengine. Kwa kuanzia nawaomba BAKWATA wapigie chapuo jambo ili liweze kufanikiwa haraka kuliko wanavyokaa kimya kana kwamba hawaoni tatizo.
Nina hakika baada ya waislamu kutimiziwa matakwa yao pia utatazama makundi mengine ya kijamii kama vile wamasai ili nao waruhusiwe kuvaa lubega na katambuga shuleni na vyuoni. Pamoja na kuwa utakuwa umewatendea haki wapiga kura wakao bila ubaguzi wowote, nina imani uvaaji wa vazi hili la kitamaduni utachangia kwa kiasi kikubwa kutangaza utalii wa kiutamadani (cultural tourism) kwani sekta ya utalii huliingizia taifa hili fedha nyingi za kigeni ambazo hutumika kujenga miundombinu ya umma kama vile SGR, Bwawa la Umeme la Nyerere, barabara na miradi mingi yenye manufaa kwa wananchi wote.
Nawasilisha.