Arusha: Yanayojiri kwenye Mapokezi ya Godbless Lema

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,703
218,246
Wakuu natanguliza salamu , poleni kwa Ugumu wa Maisha unaowakabili nchini Tanzania kwa sasa , , basi baada ya pole hizo naingia moja kwa moja kwenye mada

Ile siku iliyosubiriwa kwa hamu kubwa na Wananchi wa Arusha , imekwisha wadia , Unaambiwa usiku wa deni hauchelewi , yaani ukieagama tu kumekucha !

Taarifa kutoka kwenye kamati ya Mapokezi inaonyesha kwamba ndege ya ETH 815 aliyopanda Lema ambaye pia anatambulika kama Nabii wa Mungu , kutokana na unabii wake wote kutimia , imeondoka Addis Ababa , Ethiopia saa 4:40 asubuhi hii na inatarajiwa kutua KIA saa 6:39 mchana .

Tayari njia zilizotangazwa kutumika kwa ajili ya msafara huo Mkubwa na unaotarajiwa kuvunja rekodi , zimekwisha furika Wananchi , huku wengi wakiwa wanapeperusha bendera za Chadema na matawi ya miti , kiukweli shamra shamra ni kubwa kiasi ambacho kimewafanya baadhi ya WATALII KUAHIRISHA KUTEMBELEA MBUGA ZA WANYAMA , huku wakijawa na Shauku ya kutaka kumuona mtu anayesubiriwa kwa kiasi hicho .

Kama kawaida Erythrocyte atawaleta kila kinachojiri .

Usiondoke JF

==========
UPDATES :

Inasemekana Rais Samia naye ametua Arusha , ila bado haijajulikana kama naye atashiriki Mapokezi hayo au ana shughuli nyingine .

Watu ni wengi mno , barabara zimefurika , Vikundi vya ngoma vinaburudisha

Baba Askofu Mwamakula na Profesa George Wajakhoyah wapo Uwanjani

View attachment 2533711

Bendera za Chadema kila kona

Hatimaye Godbless Lema Amewasili Nchini mwake alimozaliwa , baada ya kukimbilia uhamishoni ili kuokoa maisha yake , baada ya vitisho vya kuuawa na viongozi wa Tanzania wa Awamu ya 5 mara baada ya Uchaguzi wa 2020 .

View attachment 2533726

UTUKUFU WA MUNGU NI WA AJABU SANA !

===================

GODBLESS LEMA ATUA ARUSHA AKIWA NA FAMILIA YAKE
Mwanasiasa na Mbunge huyo wa zamani wa Arusha Mjini, ametua Nchini, leo Jumatano Machi Mosi, 2023 akitokea Canada na kupokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) akiwa na familia yake.

Amepokelewa na mamia ya Wanachama na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Lema aliondoka Nchini baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 kwa kile alichodai kuhofia usalam wake.

=============

Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA na aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Jonathan Lema amerejea Tanzania leo March 01, 2023 na kupokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).

Taarifa ya kurejea kwa Lema ambayo ilitolewa na CHADEMA January 31,2023 ilisema “Lema aliondoka nchini na kuelekea Kenya tarehe 8 November 2020 ambako alikaa kwa mwezi mmoja na kisha tarehe 8 December 2020 alielekea nchini Canada ambako alipata hifadhi ya kisiasa, kutokana na kuwepo kwa tishio la kuuawa yeye na Familia yake."

“ Lema atapokelewa uwanja wa ndege (KIA) na Viongozi wa Chama, Wanachama na Wananchi watakaojitokeza kumpokea na kisha atakwenda moja kwa moja kwenye mkutano wa hadhara utakao fanyika Arusha Mjini”

“Lema, baada ya kurejea atakuwa na vikao ya kazi ya kuongoza kikao cha Kamati ya Utendaji ya Kanda na Baraza la Uongozi la Kanda ya Kaskazini na kisha ziara za mikutano ya hadhara na vikao vya ndani kwenye Mikoa yote ya kanda ya Kaskazini (Tanga, Kllimanjaro, Arusha na Manyara), pia atashiriki kwenye mkutano Mkuu wa Jimbo la Arusha Mjini na atakuwa na ratiba ya ziara kwenye Kata mbalimbali za Jimbo la Arusha Mjini.”
 
Wakuu natanguliza salamu , poleni kwa Ugumu wa Maisha unaowakabili nchini Tanzania kwa sasa , , basi baada ya pole hizo naingia moja kwa moja kwenye mada

Ile siku iliyosubiriwa kwa hamu kubwa na Wananchi wa Arusha , imekwisha wadia , Unaambiwa usiku wa deni hauchelewi , yaani ukieagama tu kumekucha !

Taarifa kutoka kwenye kamati ya Mapokezi inaonyesha kwamba ndege ya ETH 815 aliyopanda Lema ambaye pia anatambulika kama Nabii wa Mungu , kutokana na unabii wake wote kutimia , imeondoka Addis Ababa , Ethiopia saa 4:40 asubuhi hii na inatarajiwa kutua KIA saa 6:39 mchana .

Tayari njia zilizotangazwa kutumika kwa ajili ya msafara huo Mkubwa na unaotarajiwa kuvunja rekodi , zimekwisha furika Wananchi , huku wengi wakiwa wanapeperusha bendera za Chadema na matawi ya miti , kiukweli shamra shamra ni kubwa kiasi ambacho kimewafanya baadhi ya WATALII KUAHIRISHA KUTEMBELEA MBUGA ZA WANYAMA , huku wakijawa na Shauku ya kutaka kumuona mtu anayesubiriwa kwa kiasi hicho .

Kama kawaida Erythrocyte atawaleta kila kinachojiri .

Usiondoke JF
Wake makini na magari yao maana jamaa karudi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom