Arusha: Yaliyojiri mapokezi ya Godbless Lema, Adai VICOBA ni umasikini, Mama lishe ni utumwa, Samia asitukanwe, Mbowe ampa kazi ya Katiba Mpya

Betting ni worldwide sio Tanzania tu, halafu wanabet kwa pesa zao unasemaje kuwa hawafanyi kazi?Kama hawafanyi kazi hizo pesa wanazobet wanazitoa wapi?
Ajira hakuna,mikopo halmashauri wanatoa kwa kujuana utalalamika watu wasibet?
Waende shamba wakalime kuna shamba la 500 au 1000?
 
Betting is a worldwide issue, hata huko Canada alipokuwa akilelewa watu wanafanya Betting, kwenye makasino nk. Tatizo ni pale watu wanabweteka hawataki kufanya kazi, wanashinda vijiweni tu.


Kingine, Lema anajisahau kuwa hata huo ubunge wa kila mara anaogombea anafanya kamari tu, anakopa ili kufanya campaigns, akiupata ubunge analipa wadeni wake, akikosa ubunge inabidi auze some of his assets ili alive mkopo.

Asidanganye watu hapa, the little exposure he has kusimfanye alewe.
 
Kuna jambo limeshtua wengi sana na ningependa kujua upande wa pili wa chama wao wanaonaje kuhusiana na hilo suala. Sote tunajua baibui huvaliwa na kina nani..

Lema amekiri Amewahi Kuvaa Baibui mara kadhaa, hii kwa chadema wanaichukuliaje? Ni kawaida au chama kimeingia doa? Ikumbukwe lema ni kiongozi mkubwa wa chama.

Ningependa kujua viongozi wa chadema wanachukuliaje hili? Wanaona kawaida? Au wamefedheheka? Vipi wafuasi wa chama nao wanaona kawaida au wamefedheheka?

Swali pia ambalo ningependa kujua, Kama alikua akivaa mabaibui na Madera, ni mangapi amefanya akiwa kwenye mavazi hayo?

Ni maswali ya kupenda kujua zaidi, pia Kama tukijulishwa hakuna ubaya wowote basi itakua vizuri.

..kwa kitendo hicho tunaweza kumfananisha na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.


..Mwalimu alivalishwa baibui na kwenda kufichwa Kigamboni ili asikamatwe na askari wa jeshi la Tanganyika walioasi.
 
Sijazifuatilia hizo lkn nimefuatilia kuhusu betting. Wengi wanaanza betting for fun/enjoyment kisha viwango vya kushiriki vinaongezeka na kuwa habitual bettors, hapo ndio tunasema ni insanity.

Vv
Mie nabeti since 2013 na sijaona nikiwa addicted
 
Lema kaja na moto wa kigeni, kaanza kuwapa za uso bodaboda na vicoba, kawashukia na betting. Ccm wanazidi kujipatia point za kumnyukia, yule ni mwanasiasa mjanja sana, ccm isipende sana kurukia hoja zake na kuanza kumpondea kwa kujipendekeza kwa makundi hayo itaingizwa king na kujikuta imetetea kitu cha hovyo ikaaibika. Lema aendelee kutoa za uso kwa makundi mengine yaliyonasa kwenye mambo ya hovyo
 
Usicheze na defamation kesi ya shauri ya madai. Nataka kuwasaidia bodaboda msaada wa bure wa kisheria defamation. Hii lawsuit ni ya kufidiwa na Mwamba wa kaskazini God bless Lema baada ya UVCCM kukazania eti Lema kuwatukana kazi yao ni ya laana.

Nitashirikiana bega kwa bega na Mataga pamoja na LB7 kuhakikisha bodaboda wanapata haki yao ya msingi.

Mheshiniwa Lema amesababisha taharuki na kuwahathiri bodaboda kisaikolojia na kupelekea utendaji wao wa kazi kushuka.

Wakishinda kesi ya fidia dhid ya Lema mimi wanipe tu asilimia 10%

Kamanda Asiyechoka
 
Back
Top Bottom