ARUSHA: Watoto wawili kati ya wanne waliokuwa wametekwa wapatikana wakiwa wamekufa

Polisi tena wala usiwataje ataa .huyu kijana mtekaji ambae Leo ni muaji alikuwa anaishi ndani nyumba moja na Polisi wanakula na kulala .sana sana ni Mwenye nyumba ndio alimshtukia maana alianza uwizi Wa kuku na pesa za majirani ,Polisi alivyojulishwa kwamba kijana mwizi .akawajibu waongeze ulinzi Wa vitu vyao na kuku,
bado mimi nawalaumu sana polisi kwa tukio hili haikupaswa kabisa habari za utekaji zianze kusambaa mitaani wakati watekwaji bado wanashikiliwa na mtekaji.....wangemuwekea mtego wangemnasa bila madhara kwa hao watekaji
 
Lakini mtu kama huyo aliyekiri na ushahidi uko wazi bado anapelekwa mahakamani? Inauma sana
Mahakamani ni sawa kupelekwa ili hiyo hukumu ikapate uhalali wa sheria (maana mtu mwenyewe anaweza kuwa mwendawazimu wa msimu) , sema inakuwa ni kituko kufanya upelelezi kwa muda mrefu wakati mtuhumiwa ashakiri na kuthibitika.
 
Nina hasira,
sijui hata niandike nini.
MUNGU KWA NINI UNARUHUSU MAMBO MAGUMU KAMA HAYA?
 
Watanzania tujichunguze. Katika jamii yetu yanaanza kujengeka mawazo kuwa unaweza kuwa tajiri au unaweza kupata pesa nyingi bila kufanya kazi, bali kwa kudai au kwa miujiza.

Tunaambukiza mawazo mabaya kwa jamii yetu. Serikali inafanya blackmailing na watu wanafanya blackmailing. Hili lisipodhibitiwa mapema, litatupa shida kubwa huko mbeleni.

Mungu Baba yetu mwenye huruma azipokee roho za viumbe hawa wasio na hatia. Nayafikiria mateso yao kabla hawajakifikia kifo - difficult to imagine!

Poleni sana wazazi wenzetu wa watoto hawa. Ni vigumu kuyapokea haya lakini kwa msaada wa Mungu mjawe na nguvu wa kuyakubali yaliyotokea. Poleni sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Za jioni wakuu,
View attachment 582152
Wananchi wakishuhudia zoezi la uopoaji wa miili ya watoto wawili
Wale watoto Ikram na Maureen waliokuwa wametekwa wamepatikana katika shimo la choo ambalo bado halijaanza kutumika. Muda huu askari ndio wanafanya utaratibu wa kuwatoa.

Chanzo cha uhakika kinasema mtekaji aliwatumbukiza ndani ya shimo hilo wakiwa hai kabla ya kuondoka na kuelekea Geita kabla ya kukamatwa na kusema walipo watoto hao.

Inaumiza sijui viumbe hao walimkosea nini mtu huyo.

Inna lillah wainna illah rajiun.

=======
UPDATE
=======
Mwenyekiti wa Mtaa wa Olkerian huko Olasiti jijini Arusha, Daudi Safari amethibitisha kutokea kwa tukio hili ingawa yeye kasema ni kisima.

=======

Hapo awali Usiku wa tarehe 2 Septemba kijana mwenye umri wa miaka 18, Samson Petro alishikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuteka watoto katika mkoa wa Arusha na Geita.

Kamanda wa Polisi mkoani Geita, Mponjoli Mwabulambo alithibitisha taarifa hizo za kukamatwa kwa mtekaji huyo.

Mwabulambo alisema kuwa kijana huyo alikamatwa katika nyumba ya kulala wageni ya Shitungului iliyopo mji mdogo wa Katoro akiwa na mtoto mdogo nmwenye miaka miwili.

Alisema mtuhumiwa alimficha mtoto huyo katika chumba namba 11 cha kulala wageni iitwayo Shitungulu wakati akisubiri mpango wake wa kutaka alipwe shilingi milioni nne na wazazi wa mtoto huyo Omben Mshana na Elizabeth Ombeni.

Kuhusu utekaji/watekaji soma:

=> Kukithiri kwa vitendo vya Utekaji wa watoto/kidnapping katika Jiji la Arusha

=>GEITA: Mtekaji wa watoto Arusha, Geita anaswa na Polisi
Haya Majitu ya GEITA buana... yameona haitoshi kumteka Lissu, Ben Saanane na Roma Mkatoliki sasa yameanza kuteka watoto na kuwaua, duh
 
Mkiambiwa hukumu ya kunyogwa hadi kufa itekelewe haraka wanakuja hao wanaojiita watetezi wahaki

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapo ndipo mnapokosea ndugu zangu. Unaweza kuwa na uchungu sana lakini kuwasema au kuwakashifu WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU ni makosa zaidi. Kila binadamu ana haki zake za msingi ambazo anakuwa nazo kwa sababu yeye ni binadamu. WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU kazi yao ni kutetea pale ambapo HAKI ya binadamu yeyote inavunjwa pamoja na wewe unayewakashifu. Hili swala la hawa watoto kuuliwa linahuzunisha mno. Haki itendeke na aliyewaua apate hukumu stahiki ambayo italeta majuto makuu maishani mwake akiwa hai au maiti. Yes, hata akiwa maiti aendelee na majuto makuu.
 
Tunahita 'firing squad' kwa ajili ya vijitu kama hivi. Inauma sana. Pole sana wazazi Mungu awatie nguvu.
 
Ben sanane maskini. Alitekwa na majambazi wakubwa sasa hawa ni watoto wa majambazi
 
So sad kwa kweli, Ulaya mtu akitekwa na watekaji wakadai kiasi cha pesa police watashauri pesa ilipwe kisha mtekaji atafutwe baadae (yani uhai kwanza mengine yanafuata), huku utashauriwa usilipe pesa kwanza hadi akamatwe mtekaji (pesa kwanza uhai baadae).
 
so sad. wapumzike peponi InshaAllah

bunge la tanzania ni "rubber stamp" ya serikali ya magufuli
 
Watoto wasio na hatia wanauliwa bila sababu zozote za msingi. Siku ya mwisho yaja.
 
Kuna watu huwa wanasema hukumu ya kunyonga haifai ni ukatili ,ukiukwaji wa haki za binaadamu

Je mtu kama huyu akihukimiwa kunyongwa utamuoneaje huruma

Wengi haijawakuta hii nyie mnaotetea hukumu ya kunyongwa

Sent using Jamii Forums mobile app
Anyongwe kwasababu gani? Unataka ulaumiwe na mama Wa haki za binadamu pamoja na mwanasheria nguli
 
Back
Top Bottom