nyakubonga
JF-Expert Member
- Apr 5, 2015
- 4,712
- 7,465
Taarifa za uongo hua hazina maelezo ya kutosha.. Taarifa yako haileweki , Ni picha za Aina gani ???, Picha Za uchi?? ,Akiwa anaiba fedha au akiwa ibadani ????
Taarifa za uongo hua hazina maelezo ya kutosha.. Taarifa yako haileweki , Ni picha za Aina gani ???, Picha Za uchi?? ,Akiwa anaiba fedha au akiwa ibadani ????
hatariKumradhi! Kuna changamoto kidogo
Sorry, an error has occurred Numbisa! Your post is too short. It must contain a minimum of 50 characters and above. your curent characters is 12
Hii sio Mbinu ya Makonda na Njamaa za Huyo Wakili kutaka kuwatisha wana Arusha?Jeshi la Polisi limemkamata wakili Yonas Masiaya na kumnyima dhamana. Tukio hilo limetokea jana jioni, Aprili 30, 2024, huku likiwaacha wengi wakijiuliza maswali kuhusu utaratibu wa kisheria.
Wakili Masiaya anatuhumiwa kwa kosa la kusambaza picha ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha katika makundi ya WhatsApp. Hata hivyo, licha ya tuhuma hizo kuonekana kuwa dhaminika, Jeshi la Polisi limekataa kumpa wakili huyo dhamana, wakisema wanangojea maelekezo kutoka ngazi za juu.
Leo, Mei Mosi, 2024, wakili Ngeeyan Oloibormunyei Laizer pamoja na familia ya wakili Masiaya wamejitokeza katika kituo cha Polisi kufuatilia suala hilo. Hata hivyo, jitihada zao zimegonga mwamba baada ya Polisi kudai bado wanangojea maelekezo kutoka kwa viongozi wao.
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umeelekeza mawakili wake mkoani Arusha kuchunguza kwa karibu suala hilo na tayari wameanza maandalizi ya kufungua kesi dhidi ya Jeshi la Polisi kwa kushindwa kumpa dhamana wakili Masiaya.
Wito umetolewa kwa Jeshi la Polisi:
- Kumwachia wakili Masiaya kwa dhamana.
- Kufanya upelelezi kwa kuzingatia Sheria na Amri Kuu za Jeshi la Polisi (PGO), bila kusubiri maelekezo kutoka juu ambayo ni nje ya utaratibu wa kisheria.
- Kufanya upelelezi kabla ya kumkamata wakili Masiaya endapo kuna tuhuma dhidi yake.
- Kudai mabadiliko ya sheria ya makosa ya kimtandao ili kulinda uhuru wa watanzania katika matumizi yao ya mitandao kwa kuzingatia Sheria za ulinzi wa taarifa na faragha.
Nashangaa, mbona picha za makonda zipo nyingi Sana mitandaoni humo 🤔🤔🤔,Taarifa za uongo hua hazina maelezo ya kutosha.
Naunga mkono hoja,Labda amesambaza picha inayomuonyesha mwili mzima halafu amegeukia upande au ni picha imepigwa kwa nyuma.
Kuna watu unatakiwa
😂🙌Kama kawaida waandishi mtaishia kuandika matamko marefuuuuuuu na kutoa matamko alafu imeisha hiyooo.
Yaani Tanzania kada ya waalimu na waandishi habari ukichanganya na binam zao mapolisi sijui mlilogwaga na nani sijui
Labda amesambaza picha inayomuonyesha mwili mzima halafu amegeukia upande au ni picha imepigwa kwa nyuma.
Kuna watu unatakiwa kuwapiga picha mwisho tumboni au kifuani.
Hizo picha zilikuwa na nini kibaya?
Ndio dawa yenu hioKumradhi! Kuna changamoto kidogo
Sorry, an error has occurred Numbisa! Your post is too short. It must contain a minimum of 50 characters and above. your curent characters is 12
Kumbe shida ni CHADEMA?Diwani wakili Yonas Masiaya Laiser (CHADEMA) kata ya Lepurko iliyopo Halmashauri ya wilaya ya Monduli apata dhamana
View attachment 2978595
ORODHA YA MBUNGE NA MADIWA HALMASHAURI YA WILAYA YA MONDULI 2021-2025 source: Madiwani | Monduli District Council
View attachment 2978596
Hivi ndani ya Jeshi lote la Polisi hakuna hata Askari Polisi mmoja ambaye mwenye akili nzuri kidogo wa kuweza kulikwamua Jeshi hilo ili liondokane na majanga kama haya????
Nawapambe nao vipi?Alaaniwe Makonda na kizazi chake.
Siunajua kuna kupitishwa bila kupingwa? Hahaaaa dunia wameipatia lakini kwamola wao hawana utetezi. Midomo yao itapigwa pini. Umbea wao wa majukwaani hautowafaa kituPolisi mmoja hawezi. Kubadilisha jeshi lazima uwe na cheo fulani. RPC, IGP, OCD, Kamishna, Inspekta, Mrakibu Mwandamizi...
Kufika vyeo hivyo lazima uwe umekulia jeshini humo. Na ukikulia jeshini ni lazima uambukizwe uhoro wa typical police wa Tanzania. Kwa sababu ukileta unoko kuanzia chini hupandi. Jeshini unapanda ngazi kwa kuonyesha ukatili, kufata amri, kufata ujinga, hakuna kufikiri fikiri na kufata sheria.
Dawa yake:
Tufanye kama Ulaya na Marekani. Cheo cha IGP, RPC, OCD, aidha unaomba kwa kushindanisha CV na kufanyiwa interview
AU
Unagombea kwa uchaguzi. Kuwa Sherriff Marekani unagombea kwa kura za watu wilayani (county).
Ugali baba ugali mtamuWanasubiri maelekezo kutoka juu wapi? Ni juu mbinguni au juu wapi huko wanakosubiri kupata hayo maelekezo? Hivi dhamana kwa Watuhumiwa inatolewa kwa kujibu wa Sheria au kwa mujibu wa matakwa au maelekezo kutoka kwa mtu fulani?
Hivi ndani ya Jeshi lote la Polisi hakuna hata Askari Polisi mmoja ambaye mwenye akili nzuri kidogo wa kuweza kulikwamua Jeshi hilo ili liondokane na majanga kama haya????