VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
Niko hapa Arusha tangu juzi. Nimetembea viunga mbalimbali vya Arusha kuongea na kujionea hali ilivyo hapa. Nimesikia na kuona. Jana, name nilikoswa na mabomu ya machozi pamoja na risasi (za mpira na moto)pale Soweto.
Leo, nilikuwa Mahakamani kushuhudia kufikishwa na kusomewa mashtaka viongozi kadhaa waandamizi wa CHADEMA Taifa pamoja na watu wengineo waliokamatwa jana Soweto.Wamo Mbunge Said Arfi na Mawakili Wasomi Tundu A.M. Lissu na Mustafa Akoonay. Wamesomewa mashtaka tuliyoyazoea. YALE YALE. Kufanya kusanyiko lisilo halali. Nimeacha maombi ya dhamana yakiwasilishwa.
Wana-Arusha wanataka CHADEMA. Wanaishi na kuiamini CHADEMA. Mioyo yao inaongozwa na CHADEMA. CHADEMA inapendwa kwakuwa inahoji,inaahidi,inafanya pamoja na wananchi,inazungumza nao na kushiriki nao kijamii.Wako hivyo. Kwa hapa Arusha, 'chama tawala' ni CHADEMA. Hali hii inakera watawala-CCM. CCM wanajiona wanapuuzwa Arusha. Hawasikilizwi.Hawaheshimiwi. Hawashangiliwi. Hawasindikizwi. CCM inataka 'kutawala' Arusha.Ni jambo linalowezekana.
CCM ifanye mema na kuishi na wanachi wao vile wapendavyo.CHADEMA wanaweza kuzidiwa kwa ukarimu na utekelezaji na usimamiwaji wa Ilani ya CCM tu. Si vinginevyo. Ni dhahiri kuwa wana-Arusha walishachagua Madiwani wao hata kabla ya kuahirishwa uchaguzi kufuatia mlipuko wa bomu pale Kimandolu.Wanawajua na kujulikana. Ni wa CHADEMA.
Siasa safi inatoa nafasi ya kujipanga na kujiuliza kuelekea kujiboresha. CCM yaweza kujipanga,kujiuliza na kujiboresha hata kama hakitapata hata Kata moja ya Arusha. CCM bado ina wanachama wengi tu watiifu hapa Arusha.Iwatumie hao kuimarisha chama hapa. Siasa ina matunda yake. Matunda ya ushindi kwa CCM yaweza kupatikana. Penye nia,pana njia!
Lakini kwa namna ilivyo sasa, CHADEMA waachwe 'watese' katika jiji la Arusha.
Mzee Tupatupa (kwasasa Arusha)