Arusha pamenuka: Karatu sec wagoma! Mabomu yalipuliwa, Shule yafungwa, haijulikani itafunguliwa lini

RGforever

JF-Expert Member
Apr 3, 2011
6,878
5,424
Shule ya Sekondari karatu ambayo ni Advance, imeingia katika mgomo baada ya kutopata suluhisho la kupatikana kwa maji, Kwa takribani miezi 5 toka mwezi wa 6 mwaka huu..

Wanafunzi pamoja na serikali yao waliamua kuongea na bodi ya shule pamoja Na D.O wa Karatu tarehe 7 siku moja kabla ya 2kio, wakaahidiwa maji yatakuwepo siku hiyo kuanzia saa 11 jioni pia kesho. Imefika sa 11 maji hayakuwepo kesho yake tareh 8 maji hakuna..

Wanafunzi viongozi wote na Wanafunz wengne ndipo walipoandamana kwenda kwa Mkurugenzi. Ndipo wanakutana na vugu la polisi na kupigwa mabomu ya machozi, kutokana na wingi wa wanafunz ambao walijigawa katik makundi mawili, polisi wakashindwa kuwadhibiti mana hawakuwa wengi [defender 1 ya polis ndo ilikuja].

Wanafunzi walikuwa 600 na ushee, ambao baadh walifanikiwa kufika kwa mkurugenzi baada ya Polisi kuchanganywa na makundi mawili tofauti, walipofka ofisini, ndipo baadhi ya wanafunzi wakashikwa na kupigwa na polisi pale ofisini na kurundikwa kituo kidogo cha polisi pale Karatu, hawakufanikhwa kuongea na mkurugenzi ndipo wakaamrishwa kurudi shule wakisindikizwa na polisi.

Ndipo Mwenykiti wa Bodi ya shule kaamua kuifunga shule kwa mda usiojulikana.. Wanafunzi sasa hivi tunaondoka mwisho saa mbili asubuhi leo hii.

Matatiz mengine ni pamoja na boharia kuchakachua chakula cha shule na Wizi wa sukari na Mafuta ya kupikia.

Mimi mwenyewe mhanga wa tukio hili kama mwanafunzi.
 
Duh!! Poleni sana!! Yaani wanachakachua hadi misosi duh!!?? Huyo mkurugenzi ninaimani atakuwa na element za ki-magamba!!
 
Poleni sana ndugu zangu. Naamini Mungu yuko upande wenu na atawasaidieni kwani mnadai haki yenu ya msingi kabisa...!!!
 
Duh!! Poleni sana!! Yaani wanachakachua hadi misosi duh!!?? Huyo mkurugenzi ninaimani atakuwa na element za ki-magamba!!
Poleni sana! Siku nyingine mjigawe makundi 3,kundi la kwanza linapita barabara kuu,la pili mnapitia boda la bashay kuna chochoro la kutokea town,kundi la tatu mnapitia shamba la shanglai! Kwa idadi ndogo ya askari mtafanikiwa kufikisha ujumbe!
 
hii inanikumbusha mwaka 1995 tulipo funga shule kwa miezi 5

hii ndiyo elimu ya bongo inavyo patikana no body cares we ona hawa wanafunzi wanapigwa ofisini kwa ded sehemu ambayo waliona ni kimbilio la matatizo yao kumbe ni kinyume chake na siajabu ded ndiye aliye watuma polisi ili wakawapige

hongereni sana munao someswa ughaibuni
 
Hongereni sana vijana.Maana hata mi nina mdogo wangu hapo alishaniambia kuhusu tatizo hilo la maji!mmefanya jambo la kijasiri ambalo hata rais hawezi kufanya!nyinyi ni binadamu sio ngamia bwana,iweje mlazimishwe kuishi sehemu isiyo na maji?
 
Poleni sana! Siku nyingine mjigawe makundi 3,kundi la kwanza linapita barabara kuu,la pili mnapitia boda la bashay kuna chochoro la kutokea town,kundi la tatu mnapitia shamba la shanglai! Kwa idadi ndogo ya askari mtafanikiwa kufikisha ujumbe!

Umenifurahisha sana! Utadhan ulikuwepo, tulipita Shaghrira na Barabara ya Rami.. Na 2li2ma watu wakuchunguza njia rahisi za kuwaponyoka.. Lengo kuu ni kufika wilayani tu, tunamshukuru Mungu tulifanikiwa ingawa wachache waliumia.
 
Uandishi wako mbovu. Jitahidi kufuata kanuni za uandishi.
 
hii inanikumbusha mwaka 1995 tulipo funga shule kwa miezi 5

hii ndiyo elimu ya bongo inavyo patikana no body cares we ona hawa wanafunzi wanapigwa ofisini kwa ded sehemu ambayo waliona ni kimbilio la matatizo yao kumbe ni kinyume chake na siajabu ded ndiye aliye watuma polisi ili wakawapige

hongereni sana munao someswa ughaibuni

We acha tu.. ndugu yangu! Miaka 10 ijayo Tanzania itanyooka tu, mana ukiangalia Maandamano ye2 yalikuwa ya Amani tu, ila walicho2fanyia uwez amini.. HATUJAHARIBU KITU CHOCHOTE,HATUJARUSHA MAWE,HATUJAMPIGA MTU..Ila wilayani tumefika kwa vipigo.
 
Mbona mnapotezea?
Mmesahau kuwa karutu ni Jimbo alilokuwa akiliongoza Slaa kwa zaidi ya miaka 15? Alishindwa kabisa kutengeneza infrastructure nzuri ya maji?
Na sasa hivi huyu magwanda mwenzake aliyekuja, bado kashindwa kabisa kupata suluhisho la maji ndani ya karatu?
 
Kwani mbunge ndio anapanga bajeti ya wizara ya maji? Yeye kazi yake kubwa ni ku-influence na kuiomba serikali ipeleke huduma ya maji tena kwa kutumia kodi za wananchi.
 
Mbona mnapotezea?
Mmesahau kuwa karutu ni Jimbo alilokuwa akiliongoza Slaa kwa zaidi ya miaka 15? Alishindwa kabisa kutengeneza infrastructure nzuri ya maji?
Na sasa hivi huyu magwanda mwenzake aliyekuja, bado kashindwa kabisa kupata suluhisho la maji ndani ya karatu?

sehemu kubwa ya karatu kuna maji japo siyo mengi kutokana na nature ya eneo. Hakuna mto, ziwa wala bwawa. Kabla upinzani haujashika hatamu kulikuwa hakuna maji kabisa so wamepiga hatua japo sio kubwa.
 
Uandishi wako mbovu. Jitahidi kufuata kanuni za uandishi.

Ha ha ha haaa! Sipati picha siku CCM ikianguka utakua ktk hali gani... Asante kwa mtoa taarifa, mkirudi shule msisite kutujuza.. Usimuogope MZEE, huyu ni Gamba sugu.
 
Mbona mnapotezea?
Mmesahau kuwa karutu ni Jimbo alilokuwa akiliongoza Slaa kwa zaidi ya miaka 15? Alishindwa kabisa kutengeneza infrastructure nzuri ya maji?
Na sasa hivi huyu magwanda mwenzake aliyekuja, bado kashindwa kabisa kupata suluhisho la maji ndani ya karatu?

hilo jimbo lipo nchi gani??
 
Back
Top Bottom