Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,890
- 6,898
Mwanaharakati na Mwanasiasa
Mchungaji Mtikila
Kesi inayounguruma Arusha ambayo ilifunguliwa na Mchungaji Mtikila dhidi ya serikali ya Tanzania ukiukwaji wa haki za binafsi kuhusu mgombea binafsi inaelekea Ukingoni huku Majaji wakiwabamiza ukutani mawakili wanaoitetea serikali dhidi ya usawa na haki za binadamu juu ya uhuru wa mtu binafsi kugombea nafasi za uongozi wa kisiasa Tanzania.
- Majaji wa haki za binadamu Afrika katika kesi iliyofunguliwa na Mchungaji Mtikila waliuliza kama kuna usawa kwenye siasa Tanzania kwa wagombea wa vyama vyote kwa nyakati za chaguzi mbalimbali.
- Majaji walidadisi kama Tanzania kuna haki ya raia wa kawaida ana fulsa ya kwenda bungeni kudai ya marekebisho ya sheria inayokiuka haki yao.
- Majaji walitaka ufafanuzi wa hoja za watetezi wa serikali kwamba uamuzi wa kuzuia mgombea binafsi ni mahitaji ya umma.
- Majaji waliwakaba watetezi wa serikali waliposema hoja hiyo imepitwa na wakati kwa vile serikali ipo kwenye mchakacho wa kufanya marekebisho ya sheria, majaji waliwauliza kwa nini tangu hukumu hiyo ilipotolewa na mahakama ya rufaa hadi leo bunge halijafanyia marekebisho ya sheria hiyo kama ilivyoamuliwa na mahakama ya rufaa.
- Majaji hao waliwauliza mawakili wa serikali kama bunge linaweza kutunga sheria inayofuta nyingine wakati uzoefu unaonyesha wabunge huunga mkono yaliyomo kwenye katiba hata kama wananchi wanalalamikia kukiukwa haki zao.
- Mtikila kwa upande wake aliulizwa kwa nini ana anadai haki za mgombea binafsi wakati yeye ana chama chake cha siasa.
Source: Habari Leo