Arsenal (The Gunners) | Special Thread

.
1715834952825.jpg
 
Nilikua naangalia press conference ya Ange baada ya mechi jamaa anaonekana amekasirika vibaya mno. Anaongelea juu ya misingi ndani ya timu kua legelege akaulizwa hilo swala kaona nje ya timu au ndani ya timu akajibu kote.

This means Ange focus yake ni ushindi ila timu haina huo utamaduni, kwao mafanikio ya msimu ni kumaliza juu ya Arsenal au Arsenal asipochukua ubingwa. Makocha wawili waliopita Jose na Conte wote waliongelea hilo swala kwamba "Timu haina winning mentality"

Conte alienda mbali akasema labda hii ni historia ya Tottenham. Lakini hili swala la misingi Jose alilisema akiwa na nyumbu pia, mwingine aliyeongelea misingi ya nyumbu ni Zlatan, Pogba na Cristiano.

Kama Bongo, mafanikio ya Simba ni Yanga asishinde kitu bila kujali kama yeye hatoshinda pia and vice versa. Conte alifukuzwa kwa hili alilofanya Ange, so tusubiri kuona ikiwa Tottenham wataona aibu na kujirudi au watamfungashia virago Ange.

Loser mentality zipo kwa midtable teams mara nyingi, atafurahia kusuluhu au usipomfunga magoli mengi. Wewe upo ulimwengu mwingine kabisa yeye yupo busy kufuatilia unacheza na nani next game. Atatoa ubashiri pale, haitakua anavyotaka. Atakunywa K Vant kutuliza hasira, atajichua kidogo. Kisha anarudi tena kuleta ubashiri mpya au kuandika utumbo mpya.

Lolote litakalomjia kichwani muda huo.
Hiyo para ya pili toka mwisho daah...
 
Mkorea baada ya kuaminishwa ujinga na boss wake Masingeli nae akaubebelea vilevile kama ulivyo na kuanza kuwalisha Kima wenzie matango pori
Sijui mkorea anajisikiaje sasa hivi baada ya motivational speaker kumkimbia na kumuachia msalaba wake aubebe mwenyewe.
Masingeli msimu uliopita aliwakimbia mkabakia kuchezea spana peke yenu, na msimu huu kala kona tena lakini hamjifunzi kitu
Ngoja tuanze kufukua makaburi.
1715762208731.jpg
 
Kwa kiasi fulani, ndiyo. Ukiangalia hayo mambo amefanya huku akipambana na mambo ya kukosa wachezaji muhimu kwake, huku akijitahidi kupunguza wasio na manufaa (Ozil, Aubameyang, Tierney, Bellerin, Maitland-Niles...).

Yaani, kama makocha wote tu kwenye ligi, anafanya hayo huku akijitahidi kujenga timu inayomfaa kila msimu.
Mfano, unaona kawaleta Rice na Kai baada ya Xhaka kuondoka. Anajua ana mmoja wa makipa bora kabisa kwenye ligi, Ramsdale, lakini bado akamleta Raya, na Raya kadaka Golden Glove. Hii inaonesha kuwa dogo anataka kuimarisha kila sekta awezayo kadri awezavyo.

Kazi ipo kwenye kuleta wachezaji bora na bora zaidi kila msimu. Akifanya vizuri na kuendelea kuingia michuano ya Ulaya, atazidi kuvutia wachezaji wazuri.

Then linakuja suala la mbinu uwanjani. Ni wazi kwamba kwa mchezaji mmoja mmoja, Arteta hana akina Watkins, Doku, KdB, Olise, nk,. baadhi ambao wangeanza mbele ya wachezaji wake alionao , ila ukiangalia jinsi alivyowatumia alio nao, unaona ni kocha aliye vizuri kidogo kimbinu. Na factor ya mbinu ni muhimu maana ndiyo moja ya vitu vinavyotenganisha mafuta na maji kwenye hili game.

Projects za Timu zetu zisizotumia oil money ni ngumu sana kuwa Complete kwasababu ukiwa katika hatua ya kukarabati upande mmoja basi Mwengine unabomoka, ukienda kukarabati uliobomoka mpaka ukifanikiwa basi utakuta huu uliojenga mwanzo nao unaanza kutoboka.
Cycle inaenda hivyo mpaka unapotomoka kabisa.

Mcheki Klop:
- Alikarabati Forward kwanza (Man + Salah)
Mido na Mabeki akaacha.
- Akakarabati Mido (Kamleta Chamberlain) ikakubali.
Mabeki kaacha.
- Akaanza kukarabati Mabeki (Gomez + VVD + Kipa).
Ghafla Mido ikabomoka kwa kuumia Chamberlain na Henderson kushuka kiwango.

- Akaamua kuirudia Mido kwa kumleta Fabinho/Keita.
Ghafla Beki ikabomoka kwa kuumia Gomez na mpaka leo haijakaa sawa.

- Akiwa anapambana kukarabati Beki iliyobomoka basi ghafla Forward ikabomoka kwa kuondoka (Mane na Firmino kuzeeka).

- Akaachana na Beki akaenda kukarabati Forward (Nunez + Gakpo + Diaz) lakini hakufanikiwa.
Ghafla Mido ikabomoka.

- Akasema wacha akarabati Mido (MacAllister + Wataru + Szobo).
Lakini Mabeki + Forward wameoza.

Hiyo ndiyo Cycle ya Timu zetu ndugu usitegemee kumaliza hizo unazoziita Phase ukiwa kamili kama huna oil money au pesa za kihuni kama za Abramovic.

City alikuwa na Aguero, akaleta Jesus kuziba nafasi ya Aguero, Jesus hakufit akaleta Haaland.
Anarekebisha kila sehemu kwa wakati mmoja.
 
Kwa kiasi fulani, ndiyo. Ukiangalia hayo mambo amefanya huku akipambana na mambo ya kukosa wachezaji muhimu kwake, huku akijitahidi kupunguza wasio na manufaa (Ozil, Aubameyang, Tierney, Bellerin, Maitland-Niles...).

Yaani, kama makocha wote tu kwenye ligi, anafanya hayo huku akijitahidi kujenga timu inayomfaa kila msimu.
Mfano, unaona kawaleta Rice na Kai baada ya Xhaka kuondoka. Anajua ana mmoja wa makipa bora kabisa kwenye ligi, Ramsdale, lakini bado akamleta Raya, na Raya kadaka Golden Glove. Hii inaonesha kuwa dogo anataka kuimarisha kila sekta awezayo kadri awezavyo.

Kazi ipo kwenye kuleta wachezaji bora na bora zaidi kila msimu. Akifanya vizuri na kuendelea kuingia michuano ya Ulaya, atazidi kuvutia wachezaji wazuri.

Then linakuja suala la mbinu uwanjani. Ni wazi kwamba kwa mchezaji mmoja mmoja, Arteta hana akina Watkins, Doku, KdB, Olise, nk,. baadhi ambao wangeanza mbele ya wachezaji wake alionao , ila ukiangalia jinsi alivyowatumia alio nao, unaona ni kocha aliye vizuri kidogo kimbinu. Na factor ya mbinu ni muhimu maana ndiyo moja ya vitu vinavyotenganisha mafuta na maji kwenye hili game.
Kwa sasa arsenal tunahitaji wachezaji walio bora, mchezaji ambae anaweza ingia kwenye kikosi chochote duniani..
Saliba,ben white, partey, odeergad.. wanahitajika wengine wenye ubora mkubwa saana.

Mpaka kufikia hapa ubora wa mbinu za mwalimu ndio umetufikisha hapa, tunahitaji wachezaji bora zaidi, kuwa bora zaidi.
 
Kaka nina ombi moja kwako! Naomba uniwekee na Picha za Alex-Oxlade Chamberlain baada ya kuondoka Arsenal.

Natanguliza Shukurani
Broo nisamehe sana sijui nilighafilika nini mpaka nikasahau kumuweka dogo janja Chamberlain kwenye orodha.
Nina imani hata kesho kina Sakatonge na Ordegard wakiamua kuondoka kwenye hio Academy wanaenda kubeba makombe makubwa.
RVP mpaka kesho akihojiwa hua analaani kwelikweli kupoteza miaka 11 ya career yake kwa kuchezea Gundu Fc.
1715855498703.jpg
 
Nilikua naangalia press conference ya Ange baada ya mechi jamaa anaonekana amekasirika vibaya mno. Anaongelea juu ya misingi ndani ya timu kua legelege akaulizwa hilo swala kaona nje ya timu au ndani ya timu akajibu kote.

This means Ange focus yake ni ushindi ila timu haina huo utamaduni, kwao mafanikio ya msimu ni kumaliza juu ya Arsenal au Arsenal asipochukua ubingwa. Makocha wawili waliopita Jose na Conte wote waliongelea hilo swala kwamba "Timu haina winning mentality"

Conte alienda mbali akasema labda hii ni historia ya Tottenham. Lakini hili swala la misingi Jose alilisema akiwa na nyumbu pia, mwingine aliyeongelea misingi ya nyumbu ni Zlatan, Pogba na Cristiano.

Kama Bongo, mafanikio ya Simba ni Yanga asishinde kitu bila kujali kama yeye hatoshinda pia and vice versa. Conte alifukuzwa kwa hili alilofanya Ange, so tusubiri kuona ikiwa Tottenham wataona aibu na kujirudi au watamfungashia virago Ange.

Loser mentality zipo kwa midtable teams mara nyingi, atafurahia kusuluhu au usipomfunga magoli mengi. Wewe upo ulimwengu mwingine kabisa yeye yupo busy kufuatilia unacheza na nani next game. Atatoa ubashiri pale, haitakua anavyotaka. Atakunywa K Vant kutuliza hasira, atajichua kidogo. Kisha anarudi tena kuleta ubashiri mpya au kuandika utumbo mpya.

Lolote litakalomjia kichwani muda huo.
Sasa unalialia nini mambo ya kawaida haya. Steven Gerrard aliwai kumpa pasi drogba ili Chelsea wasinde na united wakose ubingwa.

Everton waliwahi kumuuzia mechi Guardiola ili Liverpool tusiwe mabingwa. Nyie mlitegemea kabisa mchukue ubingwa kwa msaada wa spazi mnaowatukana kila siku??
 
Ifike hatua tukubaliane Epl walau kuanzia mechi 3 za mwisho kuelekea msimu kuisha ziwe zinachezwa kwa muda sawa.

Hii itasaidia kuongeza ushindani katika ligi na kuepusha uelekea wa maamuzi ya matokea ya baadhi ya mechi.

Waiweke katika kanuni zao kabisa bila kujali hali msimamo wa ligi.

Nawaza pengine hizi game 3 za mwisho zingekuwa zinafanyika kwa namna hiyo, mbali na kuleta msisimko lakini zingweza kuwa na matokeo tofauti.
Mimi nachojua kitendo cha Arsenal kuanza kucheza game harafu mpinzani ndio anafata hio Ni advantage kubwa Sana ....

Pressure inakuwa kubwa Sana Kwa timu ambayo inakiporo ,....cheki kama Ile intensity ya game ya Spurs kama huna experienced player na coach ile game unapoteza ...

Man city tumekuwa na game moja au mbili mkononi Kila msimu tunapotaka kumaliza league kutokana na michuano tunayokuwa tunashiriki .....watu hawajui ila hii inakuwa kama kumdiscourge MTU ....Kwa timu nyingine lazima ipoteze tu
 
Sasa unalialia nini mambo ya kawaida haya. Steven Gerrard aliwai kumpa pasi drogba ili Chelsea wasinde na united wakose ubingwa.

Everton waliwahi kumuuzia mechi Guardiola ili Liverpool tusiwe mabingwa. Nyie mlitegemea kabisa mchukue ubingwa kwa msaada wa spazi mnaowatukana kila siku??
Unawinda visababu vya kua na chuki unavikosa inabidi uwe na gubu sasa.
This is me kwenye webistes zingine nikiongelea juu ya hiyo game. Ni sawa na nilivyojibu wengine humu kwamba acha City ishinde.
1715875636851.png
 
Unawinda visababu vya kua na chuki unavikosa inabidi uwe na gubu sasa.
This is me kwenye webistes zingine nikiongelea juu ya hiyo game. Ni sawa na nilivyojibu wengine humu kwamba acha City ishinde.
View attachment 2991757
Shindeni mechi zenu zote msimu ujao muone kama hamtakuwa mabingwa.

Kabla ya kulaumu flani, jiulize umepoteza points ngapi kizembe dhidi ya timu za kawaida?, mfano umepigwa nje ndani na Villa, hapo ulitegemea maajabu gani ya Spurs kuifunga City wakati Spurs hiyohiyo mechi 5 za mwisho zisizohusisha City alishinda 1 tu?.

Mbona Leicester City alichukua makombe na hao mnaoita watu wenye hela za mafuta wakiwepo?.

Timu tangu 2004 huko hakuna cha maana, kila mwaka janja janja zile zile za kusajili wachezaji wachanga wa mafungu wengi halafu mnataka mchukue ubingwa upi?
 
Back
Top Bottom