Arsenal (The Gunners) | Special Thread

yaani mi ndo ningekuwa kocha wa hii timu haki ya mungu ningekuwa wapiga watu mitama changing room maana wanaudhi sana wachezaji hawa

Wamecheza vizuri sana Jumapili iliyopita na kuweza kuwasimamisha MANU. Unategemea kwa kujua umuhimu mkubwa wa mechi ya leo basi watajituma sana katika mechi ya leo...wanaishia kufanya madudu! :(
 
ndugu yangu tuna msibaa... hata nafasi ya tatu sina nayo imani.......Ni upuuzi mtupu....Si AW si wachezaji...woye ni uozo....haingii akilini kuifunga man utd then unakuja kuchapwa na Stoke City....

Wenger anawachekea sana wachezaji wake, hayupo serious zaidi ya kutoa frustration zake kwenye chupa za maji kila siku baada hapo anatafuta sababu ambazo sio za msingi.
 
Tusubiri mwakani Wakuu ndoto zetu msimu huu ndio zimefikia ukingoni. Timu hii inabidi ifumuliwe na kujengwa upya ili kuongeza uwezekano wa kutwaa mataji mbali mbali ya soka, lakini kama tutabaki na timu hii basi tutaendelea kusononeka hata msimu ujao. Mie nasubiri mchapo wa MANU VS Chelsea sasa najua hii itakuwa na ushindani wa hali ya juu na si ajabu mshindi ndio akautwaa ufalme wa soka UK. Leo mie nashangilia Chelsea ( I am very sorry BJ & Co) maana kuna Waafrika wenzetu wengi tu Drogba, Essian, Kallou, Malouda & Mikel hahahahaha lol! Sijui kwa nini yule Torres anaanza mechi hii muhimu badala ya kuwa kwenye bench

Mkuu vipi team yako imekuwaje tena???hahaha umeamia chelsea au sio??
 
Poa sana Mkuu, huyu huwa anapunguza sana nguvu ya mashambulizi kwa kushangaashangaa kiwanjani kama vile hajui yuko kiwanjani kufanya nini.

Mkuu kwa nini unataka Chelsea wa win wakati timu yako inafungwa badala ya kutaka mau united a win ili nyinyi mumkute Chelsea???au ndio kila kitu mmekosa???mda bado bana jipe moyo mkuu....
 
Hapana Mkuu hahahahaha lol! Mie GUNNERS damu damu Mkuu :) ila leo katika mechi inayofuata nawafagilia Chelsea.


hapa tupo ukurasa mmoja mkuu ngoja nielekee eneo la tukio, yaani Big Screen manake ndo mida mida hii

poleni kwa kichapo Gunners....
 
Poa sana Mkuu, huyu huwa anapunguza sana nguvu ya mashambulizi kwa kushangaashangaa kiwanjani kama vile hajui yuko kiwanjani kufanya nini.

Mkuu kwa nini unataka Chelsea wa win wakati timu yako inafungwa badala ya kutaka mau united a win ili nyinyi mumkute Chelsea???au ndio kila kitu mmekosa???mda bado bana jipe moyo mkuu....
 
Kama kawaida ya Arsenal, wakicheza na MUFC au CFC wanacheza kwa ajili ya ushindi ikija Bolton na Stoke wanachemsha.. Hahahah another dodgy fixture and you are on the verge of losing again. Need I say more?
 
Huyu Kocha Wenger inabidi atueleze mikakati ya mwakani mapema tena baada ya kuifanyia kazi ya kutosha maana tumechoka kuwa wasindikizaji kila mwaka. Naamini mkakati wake wa sasa unahitilafu na inabidi akubali mabadiliko.
 
yaani hii Arsenal tatizo ni mabeki....hatuna kabisa watu pale nyuma....huwa wanacheza vzr kwenye game za kukamia......3-1...Hatuna uwezo wa kusaka hata sare.....Upuuzi mtupu.....
 
hawa wachezaji bwana watakuwa wamechukua hela ili wafungwe..haiwezekani yaani wamelegea kama mautumbo ya bata bana
 
Back
Top Bottom