Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,483
- 40,010
- Thread starter
- #141
Mahakama inaweza kusema "hapana."
Kama hakunufaika na alikuwa hana nia ya kunufaika au kuwanufaisha ndugu, jamaa na rafiki zake, basi hayo ni makosa mengine ya kiutendaji kazi, ambayo yanaweza yasiitwe ufisadi.
Lakini hii haisemi lolote kuhusu uzito au wepesi wa hayo makosa mengine ambayo siyo ufisadi. Nayo yanaweza kuwa ni makosa mabaya kama ufisadi, japo hayaitwi ufisadi.
Katika mifumo ya Common Law, mtu ambae ameua, kwa mfano, bila kuwa na nia ya kuua, anaweza kupotelea jela, kama ikigundulika kwamba kitendo chake ni cha kizembe na kilionyesha kutokujali thamani ya maisha ya mtu (recklessness plus extreme indifference to the value of human life (P + EIVHL). Kwa hiyo, japo kosa halita itwa Murder, hiyo haita maanisha kwamba hilo kosa lingine ni jepesi (Manslaughter/Involuntary Homicide... n.k.)
Na hapa pia, kama Lowassa kasababishia taifa hasara ya mabilioni bila kuwa na nia ya kunufaika au kuwanufaisha ndugu, jamaa na marafiki, basi hajatenda ufisadi, isipokuwa makosa mengine ya kiutendaji ambayo yanaweza kukaribia, au kuwa mabaya kama, ufisadi mbele ya sheria.
haahhahaha I give up... I know spin when I see one.. HAKUNA kosa la UFISADI kisheria.