Apigwa busu kwa mara ya kwanza, Afariki

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
Msichana mmoja wa nchini Uingereza amefariki dunia punde baada ya kupigwa busu kwa mara ya kwanza na mpenzi wake.
Jemma Benjamin msichana mwenye umri wa miaka 18 alikuwa kwenye matembezi na mpenzi wake mwenye umri wa miaka 21, mwanafunzi wa chuo kikuu, Daniel Ross.

Mwisho wa matembezi yao, kwa mara ya kwanza katika uhusiano wao wa miezi mitatu, Daniel alimpiga busu Jemma ambaye ghafla baada ya busu hilo alijinyoosha kwenye kiti huku akitoka mapovu mdomoni na kufariki hapo hapo mbele ya mpenzi wake.

Kwa mujibu uchunguzi wa gazeti la Telegraph la Uingereza, Jemma alifariki kutokana na ugonjwa wa kifo cha ghafla (Sudden Adult Death Syndrome) ambao hupelekea vifo vya watu 500 kila mwaka nchini Uingereza.

Daniel aliwaambia polisi kuwa kwa mara ya kwanza katika uhusiano wake wa miezi mitatu na Jemma, siku hiyo ndio ilikuwa mara ya kwanza kumpiga busu mdomoni.

Akielezea kifo cha mpenzi wake, Daniel alisema kuwa Jemma alifunga macho yake, alianza kutokwa na mapovu mdomoni alijinyoosha kwenye kiti na kufariki dunia.

Familia ya Jemma imesema kuwa imeshtushwa na kifo cha ghafla cha binti yao kwani alikuwa mwenye afya njema na mchezaji mzuri wa mpira wa magongo.
 
Mmh,hapo ipo kazi.tatizo mijanaume mingine unaipa mabusu yenyewe inang'ang'ana na koromeo.mie hayo mambo ya kutiana shombo za mdomo nlishayakataa mapemaaa kuogopa kuwahishwa akhera kabla ya muda
 
Mmh,hapo ipo kazi.tatizo mijanaume mingine unaipa mabusu yenyewe inang'ang'ana na koromeo.mie hayo mambo ya kutiana shombo za mdomo nlishayakataa mapemaaa kuogopa kuwahishwa akhera kabla ya muda
Mweeh!!!
 
kuna wengine unakuta tu cultural yao hairuhusu kupigwa busu so yawezekana ameeta tofauti na mila zao na desturi inawezekana hiyo wajameni!
 
mackin haikuwa bahat yake so valentine hii cjui atashnda na nan cjui
 
Hiyo tunaita coincidence. Yaani hata kama jamaa angechelewa dk 3 kabla ya kumpiga busu huyo binti angekauka tu. Ni kwa vile haiwezekani kurewind
 
alikuwa ajawai kuguswa so ule mshituko akashindwa kuhimili msisimko ndio mana wanasema ucyaamche mapenzi kabla ya mda wake
 
Back
Top Bottom