Apigwa busu kwa mara ya kwanza, Afariki

Msichana mmoja wa nchini Uingereza amefariki dunia punde baada ya kupigwa busu kwa mara ya kwanza na mpenzi wake.
Jemma Benjamin msichana mwenye umri wa miaka 18 alikuwa kwenye matembezi na mpenzi wake mwenye umri wa miaka 21, mwanafunzi wa chuo kikuu, Daniel Ross.

Mwisho wa matembezi yao, kwa mara ya kwanza katika uhusiano wao wa miezi mitatu, Daniel alimpiga busu Jemma ambaye ghafla baada ya busu hilo alijinyoosha kwenye kiti huku akitoka mapovu mdomoni na kufariki hapo hapo mbele ya mpenzi wake.

Kwa mujibu uchunguzi wa gazeti la Telegraph la Uingereza, Jemma alifariki kutokana na ugonjwa wa kifo cha ghafla (Sudden Adult Death Syndrome) ambao hupelekea vifo vya watu 500 kila mwaka nchini Uingereza.

Daniel aliwaambia polisi kuwa kwa mara ya kwanza katika uhusiano wake wa miezi mitatu na Jemma, siku hiyo ndio ilikuwa mara ya kwanza kumpiga busu mdomoni.

Akielezea kifo cha mpenzi wake, Daniel alisema kuwa Jemma alifunga macho yake, alianza kutokwa na mapovu mdomoni alijinyoosha kwenye kiti na kufariki dunia.

Familia ya Jemma imesema kuwa imeshtushwa na kifo cha ghafla cha binti yao kwani alikuwa mwenye afya njema na mchezaji mzuri wa mpira wa magongo.

Waungwana mwanaume si wa kulaumiwa ni bao alilolipata mwanamke (orgasm) ambalo linaweza kusababisha kifo cha huyo demu. Ukichukulia huyo mwanamke hakuwa kuguswa na hio ndio mara ya kwanza kubisiwa inawezekana kabisa bibie mambo yalimzidi na presha ikapanda ndio ikawa ndio mwisho wake!!!!! Ndugu zanguni muwe watafiti kwanza kabla hujambusu mwenza unaweza kumpoteza hivi hivi
 
Back
Top Bottom